Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoSheria

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 katika utangulizi wake inaeleza kuwa Tanzania inakusudia kujenga jamii ya kidemokrasia inayozingatia misingi ya uhuru, haki, kutokuwa na upendeleo wa dini na ukabila, ambapo Mamlaka ya Utendaji itawajibika kwa Bunge lenye wabunge waliochaguliwa na wawakilishi wa wananchi, pia mahakama iliyohuru inayosimamia haki bila woga wala upendeleo, na hivyo kuhakikisha kuwa haki za binadamu zote zinalindwa na kutetewa.

Kwa miaka mingi iliyopita, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inajishughulisha na marekebisho makubwa ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa kuzingatia kupanua zaidi dhima ya nguvu za soko katika uchumi, kuimarisha haki za binadamu ndani ya muktadha wa utaratibu wa kikatiba ulio huru, na kuhimiza demokrasia, utawala bora, kulinda na kuhifadhi mazingira. Sifa kuu ya marekebisho haya ni kuundwa kwa mazingira wezeshi kwa shughuli za kiuchumi za sekta binafsi na kuimarisha kwa jumla dhima  ya sekta binafsi. Serikali ya Tanzania imechukua hatua ya kufanya marekebisho ya kikatiba na kisheria kwa kuhuisha na kufufua taasisi zinazosaidia ufanisi wa sekta ya sheria.

Pata taarifa za kina kuhusu sekta ya sheria ikiwa ni pamoja na sera, programu za maboresho, muundo, mipango mikakati, shughuli za maendeleo na taasisi zinazohusiana na sekta hii. Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya Wizara ya Katiba na Sheria

Vyombo vya Sheria vya Wizara Mahakama za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Huduma ya Huduma za sheria kwa Umma Udhibiti na Uratibu wa Msaada wa Kisheria
Mpango wa Maboresho wa Sekta ya Sheria
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-02 12:14:08
Kufaa
3.0
3 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 1
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 1
Urahisi wa kutumia
5.0
1 Jumla
Rahisi Sana 1
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page