Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoUjenzi

Tasnia ya ujenzi ni sekta ya kiuchumi ya msingi sana inayowezesha utendaji na kuimarisha biashara ya ndani na baina ya sekta kama vile kilimo, viwanda n.k. Sekta hii inatawaliwa na Sera ya Ujenzi ya Mwaka 2003 na Sheria nyingi ikiwemo, Sheria ya Ununuzi Na 21 ya Mwaka 2004, Sheria ya Usajili  wa Wahandisi Na. 15 ya Mwaka 1997, Sheria ya Usajili wa Wasanifu na Wakadiriaji Majengo Na. 16 ya 1997, Sheria ya Usajili wa  Makandarasi No. 17 ya Mwaka 1997, Sheria ya Baraza la Ujenzi la Taifa Na. 20 Mwaka 1979, Sheria ya Wapimaji Na. 2 mwaka 1977 na Shirika la Viwango Na. 3 ya Mwaka 1975. Nyaraka hizi zote zinatoa sheria za ufuatiliaji na tathimini za sekta ya ujenzi nchini Tanzania.

Lengo la Sera ya Maendeleo ya  sekta ya ujenzi ni kukuza sekta inayomudu ushindani wa kimataifa, inayoweza kufanya miradi mingi ya ujenzi nchini Tanzania na kuuza nchi za nje huduma zake na bidhaa. Sekta hii ni muhimu  kwa sababu inaweza kubadilisha rasilimali nyingi halisi kuwa miundombinu ya kijamii na kiuchumi iliyojengwa ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na jamii. Sekta hii ina majengo, ujenzi na taasisi zinazoshughulika moja kwa moja na shughuli za Ujenzi. Taasisi zilizo chini  ya tasnia ya ujenzi nchini Tanzania ni pamoja na Bodi ya Usajili wa Makandarasi(CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Bodi ya Wasanifu na Wakadiriaji Majengo (AQSRB)Baraza la Ujenzi la Taifa (NCC), Bodi ya Usimamizi wa Vifaa (NBMMM), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Wakala wa Barabara Tanzania  na Wakala ya Ufundi na Umeme (TEMESA).

Pata  taarifa  za kina zinazohusu sekta ya ujenzi, maendeleo yake, sera, sheria, programu, miradi na taarifa za mwaka. Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya Wizara ya Ujenzi.

Wakala wa Barabara Tanzania Bodi ya Mfuko wa Barabara
Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme Tanzania Bodi ya Usajili wa Wahandisi
Bodi ya Usajili wa Makandarasi Baraza la Ujenzi wa Taifa
Wakala wa Majengo Tanzania Bodi ya Usajili wa Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Ujenzi
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-12 20:01:48
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page