Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoMaji

Maji  yamekuwa sehemu muhimu sana ya maisha, shughuli za binadamu na maendeleo. Ni muhimu sana kwa rasilimali ya maji itumiwe kwa uangalifu mkubwa.Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na wingi wa maji hasa maji kwa ajili ya uzalishaji na vyanzo vya kudumu vya maji (kama vile maziwa, mabwawa na mito).

Serikali imeendelea kuweka mpango mkakati kwa ajili ya utekelezaji wa Sera ya Maji ya Taifa ya 2002. Sera hiyo inazingatia zaidi utawala wa maji wenye ufanisi kupitia usimamizi wa rasilimali za maji wa uwiano kwa ajili ya maendeleo ya uchumi-jamii ambapo ushiriki wa wadau wote unasisitizwa. Mwelekeo wa sera kwa ajili ya ugavi maji na huduma za maji taka unahusu ulipaji gharama zote katika maeneo ya mijini, na wajibu wa usimamizi wa uendeshaji kwa wanaopewa huduma kwa ajili ya kuimarisha uendelevu wa huduma kwenye maeneo ya vijijini.   

Pata taarifa kamili zinazohusu Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji(WSDP)2006-2025, ambayo utekelezaji  wake ulianza mwaka 2007/2008 chini ya maelekezo ya Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Maji; imekusudiwa kudumisha mafanikio, kushughulikia changamoto na kukidhi mahitaji ya sekta mbalimbali kwa uwiano. Kwa taarifa zaidi tembelea  Tovuti ya Wizara ya Maji.

Miradi ya Maji ya Taifa Mradi wa Usimamizi wa Rasilimali Maji
Miradi ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Mradi wa Huduma Majisafi na Majitaka Mijini
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-02 13:47:40
Kufaa
5.0
1 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page