Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoUvuvi

Sekta ya Uvuvi ni miongoni mwa Sekta ndogo muhimu za kiuchumi kwa ajili ya uchumi wa Tanzania.  Sekta hii inatoa kiasi kikubwa cha ajira, kipato, kujipatia riziki, fedha za kigeni na mapato kwa Taifa. Tasnia hii inaajiri zaidi ya watu 4,000,000 wanaojishughulisha na uvuvi na shughuli zinazohusiana na uvuvi, wakati zaidi ya waendesha uvuvi 400,000 wameajiriwa moja kwa moja kwenye sekta hii.  Mwaka 2009, Sekta ya uvuvi ilichangia 1.3% ya Pato la Taifa (GDP), ulaji wa samaki kwa kila mtu nchini ni kilo 8.0 na kiasi cha 30% ya ulaji wa protini ya nyama nchini Tanzania ni kutokana na Samaki (utafiti wa Kiuchumi wa Taifa 2009).

Katika sehemu hii, utapata taarifa kuhusu kimkakati afua mbalimbali inayolenga kuboresha Sekta ya Uvuvi.  Tanzania imejaaliwa sana kuwa na maliasili nyingi za majini.  Jumla ya eneo la maji la bara ni kakriban kilomita za mraba 61,500 au kiasi cha 6.5% ya jumla ya eneo la ardhi.  Jumla ya eneo la maji ni kilomita za mraba 62,000 linalogawanyika kama ifuatavyo: kilomita za mraba 35,088 ziwa Viktoria, kilomita za mraba 13,489 ni ziwa Tanganyika, kilomita za mraba 5,760 ni ziwa Nyasa, kilomita za mraba 3,000 ni ziwa Rukwa, kilomita za mraba 1,000 ni Ziwa Eyasi na kilomita za mraba1,000 ni maeneo mengine ya maji.  Maeneo mengi haya ya maji yana samaki wengi.  Kwa upande wa bahari, nchi ina bahari ya kilomita za mraba 64,000 na ukanda wa pwani wenye urefu wa kilomita 1,424.  Ukanda Maalum wa Kiuchumi (EEZ) unafika maili za baharini 200 katika eneo la kilomita za mraba 223,000 na kuipa nchi eneo la bahari la nyongeza na maliasili za uvuvi.  Kwa maelezo ziadi, tembelea tovuti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Kukuza Teknolojia ya Uvuvi
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-16 06:00:00
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page