Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiUtaliiSehemu za kutembeleaHifadhi za TaifaHifadhi ya Taifa ya Serengeti

Nyumbu milioni moja kila mmoja akifuata mwenendo ule ule wa kale, na kutimiza dhima yake ya silika katika mzunguko wa maisha usiokwepeka: wakiwa na mhemuko wa wiki tatu za kusafiri na kupandana: mwenye nguvu mpishe, wakati misururu yenye urefu wa kilomita 40 (sawa na maili 25) inapojitosa kwenye mito yenye mamba  wengi katika msafara wa kuhama kwa wingi kuelekea kaskazini kila mwaka; kujaza upya spishi katika ongezeko la muda la wanyama linalozalisha zaidi ya ndama 8,000 wa nyumbu kila siku kabla ya kuanza tena msafara wa kila mwaka wa kilomita 1,000 (sawa na maili 600).

Hifadhi hii ni kongwe zaidi na maarufu, pia ni eneo la urithi duniani, na hivi karibuni imetangazwa kuwa maajabu saba ya dunia, ipo umbali wa kilomita 335 (sawa na maili 208) kutoka Arusha, imeenea kaskazini hadi Kenya na kupatikana na Ziwa Viktoria upande wa magharibi. Ina ukubwa wa kilomita za mraba 14,763 (sawa na maili za mraba 5,700).

Serengeti ni maarufu kwa uhamaji wa wanyama wa kila mwaka ambapo wanyama wenye kwato milioni sita wanakanyaga uwanda wa wazi, wakati zaidi ya pundamilia 200,000 na swala wa Thomson 300,000 wanajiunga na safari ndefu na ngumu ya nyumbu kutafuta malisho mapya. Hata kama uhamaji huo umetulia, hakuna ubishi kwamba Serengeti ina mandhari ya kuvutia ya kuangalia wanyama barani Afrika: makundi makubwa ya nyati, vikundi vidogo vya tembo na twiga na maelfu kwa maelfu ya pofu, topi, kongoni, swalapala, na swala wa Grant.

Kuhimili kama ilivyo utazamaji wanyama ni hisia ya ukombozi wa nafasi ambayo ni sifa bainifu ya Uwanda wa Sengereti, unaoenea kwenye savana inayopigwa na jua hadi katika upeo wa dhahabu unaometameta jua linapokuchwa. Hata hivyo, baada ya mvua kunyesha, eneo hili kubwa la rangi ya dhahabu, linageuzwa kuwa zulia la kijani lililonakshiwa mauapori. Aidha kuna milima yenye miti na vichuguu vya mchwa vilivyochomoza, mito ikiwa na kingo zenye miti ya mitini na mapori ya mijohoro yenye rangi ya njano kutokana na vumbi.

Bila ya kujali umaarufu wa Serengeti, bado inabaki kuwa hifadhi kubwa ambapo unaweza kuwa binadamu pekee kuona, wakati samba anapofikiria kuzingira kwa fahari, bila ya kutetereka kwenye mlo wake unaofuata.

Kwa taarifa zaidi fungua tovuti yetu: http://www.serengeti.org

Jinsi ya Kufika Serengeti

Kupanda ndege za kawaida na za kukodi kutoka Arusha, Ziwa Manyara na Mwanza. Kusafiri kwa gari kutoka Arusha, Ziwa Manyara, Tarangire au Ngorongoro Kreta.

Wakati mwafaka

Kufuatilia uhamaji wa nyumbu ni Desemba hadi Julai kuangalia wanyama wanaokula nyama, Juni- Oktoba.

Malazi

Nyumba nne za kupanga, kambi sita za mahema za anasa na kambi za kupiga mahema zimeenea kwenye hifadhi, nyumba moja mpya ya kupanga itafunguliwa msimu ujao (Bilila Lodge), kambi moja ya anasa, nyumba ya kupanga na kambi mbili za kupiga mahema ziko nje kidogo ya hifadhi.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-20 06:46:46
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page