Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
 • Mwl. Julius K. Nyerere
 • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiUtaliiSehemu za kutembeleaSehemu za Kihistoria

Tanzania ni nchi yenye historia ya pekee iliyosababisha kuwapo kwa maeneo mengi ya historia.  Miongoni mwa vivutio vingine maarufu vya Tanzania ni Zanzibar, yenye historia kubwa ya biashara ya watumwa na fukwe za kuvutia.Hapa chini kuna orodha ya baadhi ya maeneo muhimu sana ya historia nchini Tanzania yanayofaa kutembelea wakati wa safari za mapumziko ya likizo nchini Tanzania ili uweze kupata japo kwa muhtsari historia ya kale ya Tanzania.

Baadhi ya Minara ya Historia ya Tanzania

 • Mapango ya Amboni
 • Bagamoyo
 • Kisiwa cha Changuu (Kisiwa cha Gereza)
 • Hamamu za Waajemu za Kidichi
 • Vyumba vya watumwa vya Mangapwani
 • Magofu ya Kasri ya Sultani ya Maruhubi
 • Magofu ya Kasri ya Mbweni
 • Magofu ya Mvuleni
 • Olduvai George
 • Mji Mkongwe (wa Mawe)
 • Bet L. Jaibu
 • Ngome Kongwe

 

Mapango ya Amboni

Mapango ya Amboni yako umbali wa kilomita 8 Kaskazini ya Tanga.  Mfululizo wa Mapango ya Amboni unasemekana kuundwa Zama za Jurossic kiasi cha miaka milioni 150 iliyopita, ni mfumo mkubwa zaidi wa mapango Afrika Mashariki.  Kwa mujibu wa watafiti, eneo hilo lilikuwa chini ya maji miaka milioni 20 iliyopita.  Na inakadiriwa kuwa katika eneo la zaidi ya kilomita za mraba 234

Bagamoyo:

Mji  wa Bagamoyo ulikuwa miongoni mwa bandari muhimu sana za biashara katika pwani ya Afrika Mashariki na kituo cha pili kutoka mwisho cha  misafara ya watumwa na  pembe za ndovu iliyosafiri kwa miguu kutoka Ziwa Tanganyika kuelekea Zanzibar.  Wamishionari waliokomesha biashara ya watumwa waliufanya mji wa Bagamoyo wenye jina la Kiswahili “Jisikie  kufarijika” kituo cha shughuli zao.

Bagamoyo ni mji uliokimya wenye majengo ya Mkoloni wa Kijerumani ambayo bado mazima. Zamani mji wa Bagamoyo ulikuwa miongoni mwa bandari za  biashara muhimu sana katika pwani yote ya Afrika Mashariki. Bandari yake ilikuwa kituo cha pili kutoka mwisho cha misafara ya watumwa na pembe za ndovu iliyosafiri kwa miguu kutoka Ziwa Tanganyika. Baada  misafara kufika Bagamoyo, watumwa   na pembe za ndovu walisafirishwa kwa majahazi kwenda Zanzibar, ambako baadaye walisafirishwa duniani kote. Siku hizi, Bagamoyo ni kitovu cha ujenzi wa majahazi katika ukanda wa mwambao wa Tanzania.

Kisiwa cha Chaguu (Kisiwa cha Gereza):

Kisiwa cha Chaguu pia kinafahamika kuwa ni Kisiwa cha Gereza, kilikuwa kikimilikiwa na Waarabu waliokitumia  “Watumwa waasu” Miaka michanche baadaye, 1893 aliuziwa Jenerali, Methews, Mbritoni aliyekigeuza kuwa Gereza. Hata hivyo  hakijawahi kutumiwa kama gereza na baadaye kilitumiwa kama kituo cha karantini cha Afrika Mashariki katika kipindi cha ukoloni. Baadhi ya majengo ya gereza bado mazima, aidha Kisiwa cha Chaguu kinatumiwa mahali pa kuogelea chini ya maji, mchezo wa kuleleza juu ya mawimbi na kutweka matanga ya mashua.

Hawamu za Wageni za Kidichi:

Zikiwa zimejengwa kwenye ncha ya mwinuko wa juu kabisa wa Kisiwa cha Zanzibar na Sultani Sayyid Said mwaka 1850, zilikuwa kwa ajili ya mke wake aliyekuwa Mwajemi, na yamenakishiwa kwa lipu ya mtindo wa Kiajemi, yapo kaskazini – mashariki ya mji wa Unguja kiasi cha kilomita 15. Unafika huko kwa urahisi ukipanda basi la njia’B’ la Daladala kuelekea Babubu, na kuanzia hapo  kiasi cha kilomita 5 mashariki kwenye barabara isiyojengewa. Hii tofauti ya pekee ikilinganishwa na hawamu za kawaida karibu ya Kizimbani, zilizojengwa ndani ya viunga vya minazi na barafu vibarafu vya enzi ya Said.

Vyumba vya Watumwa vya Mangapwani:

Karibu ya kijiji cha Mangapwani, Kaskazini ya mji wa Unguja kuna pango la asili na pango la  watumwa lililotengenezwa na binadamu. Pango la asili la matumbawe lina njia mwembemba wa kuingilia na bwawa la maji baridi kwenye kina chake. Pango la Watumwa, chumba cha pembe nne kichochongwa kwenye matumbawe, lilitumiwa kuhifadhi watumwa baada ya biashara ya utumwa kukomeshwa, mwaka 1873. Pango la asili linaweza pia kuwa limetumiwa kuficha watumwa; ingawa hakuna uhakika.

 

Magofu ya kasri ya Sultani ya Marahubi:

Magofu haya yapo umbali wa kilomita nne kaskazini mwa Unguja. Yapo kando ya barabara ya Babubu na yalijengwa mwaka 1882 na Sultan Barghash kwa ajili ya wanawake maharumu wengi (inasemekana walikuwa 99) . Kasri hiyo ilinusurika kuteketezwa kwa moto mwaka 1899. Zilizobaki ni nguzo tu na mifereji iliyoleta maji kwenye kasri kutoka kwenye chemchemi ya karibu. Eneo limekua sana na marumaru kwenye hamamu zimeibwa tangu zamani.

 

Magofu ya Kasri ya Mbweni:

Kasri hii ilijengwa mwaka 1871 na Universities Mission to Central Africa kwa ajili ya kuwaokoa watumwa. Mwaka 1882 Kanisa la matakatifu John (St. John’s Church) mahali hapo kwa kutumiwa na watumwa walio achiwa huru. Kuna mlango wa nakshi nzuri na mnara. Zamani ilikuwa mahali pa mapunziko pa Sultani Seyyid Barghash, na ilikuwa mahali pa zuri mno pa kuangalia pwani.

 

Magofu ya Mvuleni:

Magofu haya yapo kaskazini mwa Kisiwa, ni mabaki ya Wareno hujaribu kuitawala Zanzibar.

Olduvai Gorge:

Ipo kati ya Ngorongoro Crater na Serengeti, ina visukuku vingi vya kale, yakiwemo mabaki mengi ya wake wa kale, yaligunduliwa hapa na Dkt. Louis Leakey. Kuna makumbusho madogo na jukwaa linaloangalia kutoka juu ya Gorge. Ziara za mihadhara inayoelekezwa ipo.

Mji mkongwe (wa Mawe)

Mji Mkongwe (wa Mawe) ni mji Mkonge zaidi wenye historia ndefu na muhimu, pamoja na urithi wa utamaduni wa kina na ndiyo maana ukawa eneo la Urithi wa Utamaduni wa Dunia. Mji huu ulikuwa kama mji mkuu wa biashara kwenye mwambao, kitovu cha wavumbuzi wengi, na wamishionari kama vile David Livingstone. Inavichochoro vinavyopindapinda, maduka yenye bidhaa na vikorokoro, misikiti na nyumba kubwa za Waarabu. Maeneo ya kuvutia ni pamoja na mitaa ya mji mkongwe wa mawe, Bet l Jaibu, Kasri ya Wananchi, Nyumba ya Daktari Livingstone na Ngome Kongwe na mengineyo.

Bet l Jaibu:

Bet l Jaibu ni jengo kubwa la umbo la pembe nne, lenye ghorofa nyingi na kuzungukwa na safu za nguzo na roshani, na mnara mrefu wa saa. Ilijengwa mwaka 1883, kama kasri ya sherehe za Sultani Barghash na ilikuwa ya kwanza Zanzibar kuwa na taa za umeme na lifti ya umeme. Haishangazi wakati ilipojengwa, wenyeji waliita Bet l Jaibu iliyomaanisha Nyumba ya Maajabu. Hadi sasa ni miongoni mwa majengo makubwa sana, Zanzibar.

 

Ngome Kongwe:

Ngome Kongwe ya Waarabu ni maajabu ya usanifu ujenzi. Waarabu wa Omani walijenga ngome hii juu ya kifusi cha Kanisa la mareno. Ilimalizika mwaka 1710 na hatimaye ilitumiwa kama gereza kwa wahalifu wa kivita, halafu kambi ya jeshi, na wakati wa ukoloni, kama ghala na karakana ya  reli ya Babubu (urefu wa kilomita 15/maili 9 iliyotoka nje ya Unguja ambayo haikuendelea zaidi na kutumiwa vibaya). Uwanja wa ngome ilijengwa mwaka 1949 ili kiwe kiwanja cha kuchezea tenisi mwanawake. Imefanyiwa ukarabati na uwanja umekuwa ukumbi wa maigizo na kituo cha utamaduni.

 

 

Mapango ya Amboni Bagamoyo
Kisiwa cha Changuu (Kisiwa cha Gereza)
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-22 16:07:58
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page