Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiUtaliiSehemu za kutembeleaUtalii wa Kitamaduni

 Utalii wa Utamaduni

Utalii wa Utamaduni umekuwa ukiendelea tangu mwaka 1996, chini ya usimamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii (MNRT) na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV).  Utalii wa Utamaduni ulianzishwa  na vijana katika vijiji vya Kaskazini mwa Tanzania.  Shughuli hiyo ni matokeo ya kikundi cha vijana wa Kimasai kilichokuwa kikitumiwa kucheza ngoma kwenye barabara ya Safari ya Kaskazini inayoelekea kwenye vivutio vikuu vya utalii  vya eneo la Ziwa Manyara, Ngorongoro na Serengeti.  Wakati ngoma hizi za kujitolea zilipokuwa zinaendelea walipewa fedha kidogo kama asante kwa kutoa huduma ya kusisimua safarini.

Kadiri vilivyopata umaarufu, kikundi hiki kilitambua  kuwa wanapata hasara kwa kukosa njia rasmi ya kuuza bidhaa yao ya Utamaduni.  Kikundi kiliamua kutafuta msaada kutoka SNV ambao wakati ule walikuwa wakifanya miradi mingi ya maendeleo katika ardhi ya Wamasai.  SNV iliwasiliana na Wizara ya Maliasili na Utalii na TTB ili kuona namna ya utakavyofanyiak ushirikiano wa kuendeleza shughuli hiyo.  Wakati huo huo Sera ya Taifa ya Utalii imeeleza ushirikishaji wa jamii katika shughuli za utalii ili kutoa fursa kwa juhudi mbalimbali za utalii zilizoanzishwa na jamii kusaidiwa ziwe rasmi.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-22 16:54:44
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page