Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiUtaliiSehemu za kutembeleaMiji na majijiZanzibar

Uvamizi wa Wareno na kutamalaki mwambao wa Waswahili mwishoni mwa karne ya 16 ulimaliza ustawi wa funguvisiwa, ingawa Waarabu wa Oman walirudi kutawala chini ya karne moja baadaye.  Hivi sasa, mitaa mingi inayopindapinda na majengo marefu ya nyumba ya Mji Mkongwe wa mawe hayabadilishwa na wageni wanaweza kutembea kati ya kasei ya Sultani, Bet-El-Jaibu, Gome Kongwe ya Wareno na bustani nyumba za wafanyabiashra na mabafu ya waturuki ya Mji Mkongwe.  Safari ya siku moja kwenye mashamba ya kazi ya marashi ya karafuu,  huwapa wageni fursa ya kujionea kilimo cha karafuu, vanilla, popoo, mdalasini na viungo vingine vilivyokipa umaarufu kisiwa hicho.

Mwambao wa Zanzibar una fukwe bora zaidi duniani lakini mchanga na mawimbi hutofautiana hutegemea ni upande gani wa kisiwa ulipo.  Katika mwambao wa mashariki, mawimbi yanapiga kwenye miamba tumbawe na matuta ya mchanga yako ufukweni na maji kupwa yanaonyesha madimbwi madogo ya kiti cha pweza, minnows wadogo na anemones. Upande wa kaskazini,kuogelea baharini hakuna hatari kubwa ya maji kupwa-kujaa na fukwe laini na mchanga mweupe hufanya siku zinazong’ara jioni.

Bandari ya Mji Mkongwe imeenea Pwani ya Magharibi, na ingawa fukwe za Mangapwani, ambako mapango ya watumwa yanaonekana wakati wa maji kupwa na karibu ya Bububu ni umbali wa chini ya mwendo wa nusu saa kwa gari, kulala siku moja au mbili upande wa mashariki au pwani ya kaskazini kuna thamani kubwa ya muda wa saa moja zaidi inayotumika kufika kule kwa gari.  Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Chole nje ya Mji Mkongwe wa Mawe pamoja na Gereza lililo karibu, kaburi na visiwa vya nyoka hukupa safari ya siku moja ya kujiburudisha na mapumziko mazuri baada ya kupita kwenye mitaa myembamba inayopindapinda kwenye mji mkongwe.

Kwenye pwani ya kusini ya Zanzibari kuna enao la hifadhi la Menai Bay, eneo linalolindwa la kaba kwa spishi zilizo hatarini wanaokuja kutaga kisiwani.  Barabara za Pwani ya kusini – magharibi zinawafikisha wageni kwenye Msitu wa Jozani, maskani ya mbega wekundu adimu wa Zanzibar na Jamii nyingine ya  kima na spishi za paa.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-23 18:28:16
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page