Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiUtaliiMambo ya kufanyaKupiga Mbizi na Kuogelea Chini ya Maji

Kupiga Mbizi

Tanzania inawapa wazamiaji miamba mingi na makundi makubwa ya samaki wa tropiki karibu sana na fukwe maarufu na maeneo yaliyotengwa.

Mafunzo ya kupiga mbizi yanatolewa kwenye hoteli nyingi na nyumba za kitalii kwenye mwambao wa bara, pamoja na visiwa vya Zanzibar, Pemba na Mafia na ni stadi inayolipa kujifunza ukiwa kwenye mapumziko, lakini waogeleaji wa juu ya bahari  wasikate tama kwa sababu miamba mingi ilipita kwa waogeleaji chini ya maji na vifaa vinapatikana kwa urahisi kwa kukodi kwenye maduka ya kupiga mbizi na nyumba za kitalii. Kupiga mbizi kunaweza kuwa mwaka mzima, hata hivyo majira ya masika si rahisi kuona vizuri.

Fukwe za Zanzibar

Mchanga mweupe wakuvutia uliyosongwa na minazi hushawishi mapumziko mazuri ya ufukwenihuko Zanzibar. Nyumba nyingi za kupumzikia (kuanzia mabanda ya kawaida ya ufukweni hadi ya anasa yenye nyota tano), hukupa shughuli nyingi kama vile michezo ya majini, kupiga mbizi na kuogelea chini ya maji, usafiri wa majini jua linapotua kwa kutumia mashua zenye matanga meupe- bila ya kusahau chakula kitamu kwenye migahawa mizuri ya vyakula vya baharini.

Mzamiaji kwa Kutumia Vifaa vya Kupumulia

Mandhari ya rangi za kuvutia zinayozunguka visiwa vya Matumbawe vya Zanzibar na Pemba yanakuwa mahali panapofaa kujaribu uzamiaji kwa kutumia vifaa vya kupumulia na kuogelea chini ya maji. Kuna maeneo mengi ya kupiga mbizi visiwani yaliyolindwa kama hifadhi za bahari na maeneo tengefu. Bahari ya Hindi yenye joto inakupa fursa ya kuona waziwazi aina zote za matumbwe, samaki wenye rangi mbili angavu za kuvutia, pomboo, taa na nyenga, kasa na papa.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-26 08:20:18
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page