Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiUtaliiMambo ya kufanyaUpandaji Milima

Hifadhi na maeneo tengefu mengi ya Tanzania yanampa aina mbalimbali za kupanda mlima mtalii mwenye shauku ya kupanda. Wengi hupenda kupanda mlima Kilimanjaro na milima Meru, hata hivyo kuna mahali pengine kama vile Nyanda za Juu za Kreta. Kampuni za Safari za kupanda mlima zitakupangia kwa furaha sana ratiba itakayofaa uchaguzi wako. Sehemu inayokueleza “Unavyotakiwa kuchukua” itakusaidia kuhakikisha kuwa unajiandaa vya kutosha. Unashauriwa, hasa unapopanda miinuko mrefu zaidi kuchukua vitu polepole na kuuwezesha mwili wako kuzoea hali ya hewa.

Kwa maelezo zaidi:, angalia Milima na Volkano katika sehemu ya “mahali pa kwenda

Kupanda Mlima Kilimanjaro

Mlima Kilimanjaro ambao ni kilele kirefu zaidi barani Afrika wenye urefu wa mita 5,895 (futi 19,341) umewavutia watalii wengi wenye shauku kwa miongo mingi. Safari ya kupanda mlima Kilimanjaro ni ngumu na inahitaji bidii kufika kileleni, lakini mtu yeyote mwenye afya njema anaweza kufika. Kupanda mlima hadi kileleni kunaweza kuchukua siku tano hadi sita iwapo imepangwa vizuri na hujumuisha waongozaji, wabebaji mizigo, chakula, na vifaa. Kuangalia jua hasa linapochomoza ukiwa  juu ya kilele ni jambo la kuvutia mno.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-26 09:07:04
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page