Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiUtaliiMambo ya kufanyaHuduma ya maduka

Nunua sanaa za Kiafrika au sanaa zozote za thamani kutoka kwenye vituo maarufu vya kitalii.  Dar es Salaam, Arusha na Mji Mkongwe wa mawe, Zanzibar kumetapakaa maduka ya sanaa za thamani, masoko na mitaa yenye maduka ya bidhaa mbalimbali pamoja na barabara kuu karibu ya hifadhi na maeneo tengefu, na barabara za pwani nyuma  ya mahali pa mapumziko ya fukweni kote kuhna magenge ya kando ya barabara.  Vitu vya kununua ni pamoja na ngoma za Kiafrika, batiki, vitu vya kufumwa kama vikapu, vikorokoro vya kuwekea sabuni vya mawe, masanduku ya nakshi yaliyochongwa kwa mkono, michoro ya Kimasai na mandhari ya Serengeti kwa mtindo maarufu wa Tingatinga na michongo mikubwa  ya wanyama ya miti au mabakuli ya saladi vilivyochongwa kutoka mti mmoja wa mtiki/mninga.

Vitu vya Kimasai kama vile vitu vilivyonakshiwa shanga, vibuyu vyenye nakshi na mablanketi mekundu yanayovaliwa na wanaume wa Kimasai ni zawadi za ukumbusho.  Kanga na Vikoi ni saruni zinazovaliwa na wanawake na wanaume kwa mfuatano huo na mara nyingi ni za rangi na maumbo ya kuvutia.  Nguo hizo hutengenezwa vitu vingine yakiwemo mavazi, foronya za mito ya makochi na mabegi.  Zanzibar utapata vigae vya zamani, mabakuli ya kale na seti za masanduku ya kuchongwa  kwa mbao ya Zanzibar (zamani yalitumiwa na Masultani kuhifadhi vitu vyao, lakini siku hizi yameigwa kwa wingi), pamoja na pakiti za viungo vya Zanzibar kwenye mji mkongwe na mawe pamoja na wakati wa ziara za kutembelea viungo na marashi.

Kito chenye thamani ya wastani kinachopatikana nchini Tanzania tu ni Tanzanite, chenye rangi ya bluu iliyoiva hadi zambarau iliyopauka, na kupatikana Arusha.  Vitu vya Tanzanite vinapatikana maduka makubwa ya sanaa za thamani na maduka ya vito mjini Arusha, Dar es Salaam na Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Wakati bei takriban kwenye maduka yote zimepangwa isipokuwa kwenye maduka ya sanaa za thamani ambako mapatano ya bei ya kiungwana yanaruhusiwa, hasa iwapo hakuna biashara au umenunua vitu vingi.  Mapatano ya kupunguziwa bei kufanyika sana kwenye masoko ya mtaani.

 

Saa za kununua vitu

Jumatatu hadi Ijumaa saa 2.00 asubuhi – 11:30, Jumamosi 2:30 asubuhi hadi 6:30 mchana.  Baadhi ya maduka ya kitalii hufunguliwa Jumamosi, wakati baadhi ya maduka makubwa ya Kiislam na biashara nyingine hufungwa Ijumaa mchana, lakini yanaweza kufunguliwa Jumapili.  Zanziba baadhi ya maduka hufungwa mchana kwa mapumziko kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:00, lakini hubaki wazi mpaka saa 1:00 usiku kwenye miji mikubwa masoko yako wazi kila siku kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 12:00 jioni.

ZINGATIA:

CITES (Uhifadhi wa Biashara ya Kimataifa kwa spishi zilizohatarini kutoweka za wanyama na mimea) ilianzishwa kuzuia biashara ya spishi zilizohatarini kutoweka.  Majaribio ya kupitisha kwa magendo bidhaa zilizopigwa marufuku kunaweza kusababisha kunyang’anywa/ kutaifishwa, kupigwa faini au hata kufungwa.  Biashara ya Kimataifa ya pembe za ndovu, pembe za faru, bidhaa za kasa na ngozi za wanyama kama simba, chui, chita n.k ni haramu.

Burudani za Usiku nchini Tanzania

Burudani za usiku ni chache sana Tanzania lakini Dar es Salaam kuna Klabu za starehe nyingi, kumbi za dansi ya kabareti na sinema.  Kwa ujumla burudani za usiku ziko kwenye vituo vya kitalii kama vile hoteli na migahawa kwenye mwambao hasa Zanzibar, hoteli na baa za fukweni.  Mara nyingi dansi na ngoma za kiasili huchezwa kwenye hoteli za kitalii na hoteli za fukweni.  Tafrija zenye ghasia wakati wa mwezi mpevu ni maarufu sana kwenye fukwe za kaskazini Zanzibar zinazowalenga watalii.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-26 16:07:58
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page