Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuWasifu wa Tanzania

Tanganyika ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961 na kuwa Jamhuri  tarehe 9 Desemba 1962. Zanzibar ilipata uhuru  19 Desemba 1963 chini ya utawala wa kisultani na kuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar baada ya Mapinduzi tarehe 12 Januari 1964. Dola mbili hizi ziliungana na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili 1964.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi iliyopo Afrika Mashariki inayopakana na Uganda na Kenya upande wa kaskazini; Rwanda, Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya  Kongo upande wa  magharibi; Zambia, Malawi na Msumbiji upande wa kusini. Upande wa Mashariki nchi imepakana na bahari ya Hindi.

Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ina mikoa 30. Makao makuu ni Dodoma na Dar es salaam ni Mji Mkuu wa kibiashara. Aina ya fedha inayotumika Tanzania ni Shilingi ya Tanzania na lugha ya taifa ni Kiswahili wakati huohuo Kiingereza hutumika kama lugha rasmi ya mawasiliano.

Jina Tanzania limeunganishwa kutokana na majina ya Tanganyika na Zanzibar baada ya Muungano wa nchi hizo mbili mwaka 1964  lilipozaliwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Tanzania ni miongoni mwa nchi changa zinazoendelea ambayo ina uwezo na matarajio makubwa ya kuendelea kukua. Ni nchi yenye utajiri mkubwa wa maliasili, sera nzuri za uchumi na uwekezaji zinazovutia. Tanzania inatekeleza demokrasia kwa vitendo na imedhamiria kutimiza utawala bora kwa kufuata misingi ya sheria na kufuata misingi ya haki za binadamu.Endelea kusoma zaidi ujue wasifu wa Tanzania kwa Jiografia , Watu ,Dini ,Uchumi,Lugha na Siasa.

Jiografia Watu
Dini Uchumi
Lugha Siasa
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-05 06:46:46
Kufaa
3.0
4 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 2
Sina Hakika 1
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 1
Urahisi wa kutumia
4.5
4 Jumla
Rahisi Sana 2
Rahisi Kiasi 2
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page