Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliMipango ya Maendeleo

Tanzania imetangaza Dira ya Maendeleo ya 2025. Chimbuko la Dira ya 2025 ni kwamba, ifikapo mwaka 2025, Tanzania itakuwa imepitia katika marekebisho ya kiuchumi na maendeleo yasiyoepukika ili kufikia hadhi ya pato la kati; likiwa na viwanda vya kisasa zaidi, ushindani, maisha bora, utawala wa sheria na kuwa na jamii iliyoelimika na inayopenda kusoma.  Kwa usahihi zaidi, Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya 2025 imeeleza kwa muhtasari matarijio ya kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa robo ya kwanza ya karne ya 21; kwa lengo la msingi la kufikia hadhi ya nchi yenye uchumi wa kati (MIC), yenye wastani wa pato la kila mtu la Dola za Marekani 3,000 (kwa makadirio tu) ifikapo mwaka 2025.

Dira ya 2025 ilipangwa itekelezwe kupitia mfululizo wa mipango ya maendeleo ya miaka mitano mitano. Serikali imeanzisha sera za uchumi kwa jumla na programu za maendeleo kwa lengo la kuwawezesha  watu na kukuza ukuaji  wa uchumi nchini. Sera na mikakati  mbalimbali ilitungwa kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi Watanzania  ili wamiliki, waendeshe na wanufaike na uchumi  wao  kufikia dira ya 2025.

Katika sehemu hii utapata taarifa kuhusu mipango ya maendeleo ya sekta  mbalimbali zikiwemo kilimo, elimu, afya, uvuvi, maji, usafirishaji, sheria,ardhi, utalii, nishati na madini.

Dira 2025 Elimu
Kilimo Maji
Utumishi wa Umma Uchumi
Afya Jinsia na Watoto
Uchukuzi Ardhi
Uvuvi Utalii
Mifugo Nishati na Madini
viwanda Sheria
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-05 07:33:32
Kufaa
4.7
3 Jumla
Inafaa Sana 2
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
1 Jumla
Rahisi Sana 1
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page