Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Taifa LetuHistoria

Historia ya Tanzania ilianza na wakoloni wa Ulaya. Karne ya 18 ilikuwa na dola ndogo za miji katika mwambao baada ya kukaliwa na waarabu kutoka Oman. Ilikuwa karne 7 baadae mwaka 1499 wakati  baharia wa Kireno Vasco da Gama alipotembela visiwa vya Zanzibar. Baada ya takribani miaka 100 au kabla ya karne ya 16 Wareno waliichukua Zanzibar. Wareno hawakukaa muda mrefu sana na mwaka 1699 walipinduliwa na waarabu wa Oman waliorudi kuitawala Zanzibar. Kwa hiyo katika karne ya 18 Sultan wa Oman aliimarisha utawala wa waarabu katika mwambao wa Afrika Mashariki na kuufanya uwe sehemu ya Zanzibar.

Mwaka 1840 wakati Sultan Seyyid bin Sultan alipohamisha mji wake mkuu kutoka Oman kuja Zanzibar, biashara ya utumwa na pembe za ndovu ilistawi. Mwaka 1861 utawala wa Sultan wa Zanzibar na Oman ulitengana baada ya kifo cha Seyyid. Katika karne ya 19 wazungu walianza kuvumbua bara, wakafuatiliwa kwa karibu na wamishionari wa kikristo. Mwaka 1884 German Colonization Society ilianza kutoa ardhi bara kwa kuipinga Zanzibar na mwaka 1890 Uingereza ilichukua hadhi ya kuilinda Zanzibar, ikakomesha biashara ya utumwa na kutambua madai ya Ujerumani kwa bara. German East Africa ilianzishwa rasmi kama koloni mwa 1897.

Mwaka 1905-1907 Vita ya Majimaji ilizimwa kikatili na majeshi ya kijerumani. Matukio ya duniani yakajitokeza kwa kutokea Vita vya Kwanza vya Dunia, na kama ilivyokuwa huko Ulaya, German East Africa haikukwepa vita hivyo, ingawa vita vikali havikuchukua muda mrefu kutokana na kushindwa kwa German East Africa na Waingereza 1916. Mwaka 1919 iliyokuwa Umoja wa Mataifa ndio iliipa Uingereza mamlaka kutawala sehemu ya German East Africa aliyojulikana kama Tanganyika. Mwaka 1946 Tanganyika ilikuwa nchi iliyo chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa.

Baraza la kutunga sheria liliundwa mwaka 1926, likaongezwa mwaka 1945 na kuundwa upya mwaka 1955 na kutoa uwakilishi sawa kwa waafrika, waasia na wazungu, kuwa na viti 30 vya wasio rasmi na 31 walio rasmi. Mwaka 1954 Mwalimu Julius Nyerere alianzisha chama cha Tanganyika African National Union (TANU) kilichohimiza utaifa wa waafrika na kuleta mabadiliko ya katiba ya kuongeza sauti ya waafrika na kutenga viti kwa ajili ya jumuiya ndogondogo.

Uchaguzi ulifanyika mwaka 1958 na 1960. Matokeo ni ushindi mkubwa kwa TANU ambayo wakati huo ilikuwa ikifanya kampeni kubwa kwa ajili ya uhuru pamoja na utawala wa wengi. Serikali mpya na serikali ya Uingereza walikubaliana katika mkutano wa katiba mjini Uingereza kuipa Tanganyika uhuru kamili Desemba 1961. Zanzibar ilipata uhuru 1963 kama nchi ya pekee na dola chini ya Sultan al-Busaidy .

Tanganyika imekuwa Jamhuri Desemba 1962 mwaka mmoja baada ya kupata uhuru na uchaguzi wa urais uliofanyika ilimwezesha kiongozi wa TANU Mwl. Julius Nyerere kuwa rais. Mwaka 1965 katiba ilibadilishwa na kuanzisha mfumo wa chama kimoja. Wakati huohuo huko Zanzibar mapinduzi yaliyofanyika Januari 12, 1964 yalimwangusha Sultan. Mwezi mmoja baada ya uhuru katiba ilisitishwa; Abedi Amani Karume alitangazwa kuwa rais wa kwanza wa kiafrika wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na nchi ikawa ya chama kimoja cha Afro-Shirazi Party.

Tarehe 26 April 1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwl Julius Nyerere akiwa rais na mkuu wa dola na Karume akawa makamu wa rais na wakati huohuo akiwa rais wa Zanzibar. Mwaka 1971 Karume aliuawa huko Zanzibar na Aboud Jumbe alichaguliwa badala yake kuwa rais wa Zanzibar na makamu wa rais wa Tanzania. Muungano huo wa kisiasa kati ya Zanzibar na Tanzania Bara umedumu kwa zaidi ya miongo mine ya mabadiliko. Zanzibar ina bunge na rais wake.

Katika jitihada ya kujenga usawa katika jamii na maendeleo ya haraka Tanzania ilianzisha ujamaa wa kiafrika. Ujamaa, (ina maana kuwa pamoja) ulizinduliwa mwaka 1967 kwa tamko la Azimio la Arusha na utaifishaji wa mabenki, shughuli za fedha, viwanda, biashara kubwa, masoko kuendeshwa na bodi na wakulima kuishi katika vijiji vya ujamaa vilivyotengwa kutoka mashamba makubwa. Mwaka 1977 vyama viwili tawala - TANU na AFRO SHIRAZI PARTY viliungana na kuunda Chama cha Mapinduzi(CCM).

Tanzania ilirudisha mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na uchaguzi wake wa kwanza wa vyama vingi ulifanyika mwaka 1995 na Chama Cha Mapinduzi kilishinda na kinaendelea kutawala kutokana na kushinda chaguzi mfululizo.

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-05 09:53:50
Kufaa
4.9
7 Jumla
Inafaa Sana 6
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
6 Jumla
Rahisi Sana 6
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page