Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliKatiba

Katiba ya nchi inatambuliwa kuwa ni sheria kuu au ya msingi inayoweka mihimili mikuu mitatu ambayo ni Dola, Bunge na Mahakama. Inafafanua majukumu ya kila mhimili na kutoa mgawanyo wa madaraka miongoni mwa mihimili hiyo.  Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakidhi tafsiri hiyo na ina jumla ya sura kumi.

Sura ya Kwanza inaeleza misingi mikuu ya Sera ya Taifa; Haki za Msingi  na Wajibu wa Watanzania. Sura ya pili hadi ya sita inatoa masharti ya uanzishaji wa Serikali ambayo inajumuisha Dola, Bunge na Mahakama na kufafanua mgawanyo wa madaraka na kazi miongoni mwao.

Sura ya Saba inaeleza masharti kuhusu fedha za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sura ya Nane inaunda Mamlaka ya Serikali za mitaa, majiji, manispaa na wilaya za vijijini. Sura ya Tisa inatoa masharti ya kuwepo na udhibiti wa majeshi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sura ya mwisho ambayo ni Sura ya Kumi  inatoa masharti  mengineyo yanayohusu utaratibu wa kujiuzulu watu wanaoshika nyadhifa zilizotajwa ndani ya Katiba, pia inatoa ufafanuzi wa baadhi ya masharti yanayotumika ndani ya Katiba . Haya ndio yaliyomo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Utayarishaji na Urekebishaji wa Katiba.

Utungaji wa Katiba mpya ya nchi au dola ni mchakato tofauti na wa pekee na ule wa urekebishaji wa Katiba iliyopo. Mwenendo uliopo nchini Tanzania na nchi nyingine za Jumuiya ya Madola barani Afrika ni kwamba katiba mpya inatungwa na Bunge linalojulikana kama Bunge la Katiba; wakati  urekebishaji wa katiba iliyopo unafanywa na Bunge lenyewe linalotumia taratibu maalum katika kutekeleza kazi maalumu za Bunge. Kwa maelezo zaidi tembelea Tume ya Mabadiliko ya Katiba


No Katiba Mwaka Faili / Anuani Miliki
1 Majina ya Wajumbe wa Katiba 2014 442.2 KB
2 Rasimu ya Pili ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano 2013 1.0 MB
3 Rasimu ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano 2013 395.2 KB
4 Katiba ya Zanzibar ya 1984 2010 245.6 KB
5 Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 262.1 KB
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-01 11:27:22
Kufaa
4.4
14 Jumla
Inafaa Sana 9
Inafaa Kiasi 3
Sina Hakika 1
Haifai Sana 1
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
4.3
13 Jumla
Rahisi Sana 6
Rahisi Kiasi 5
Sina Hakika 2
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page