Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo BiasharaBiashara na Utozaji Kodi

Sheria ya Kodi ya Mapato ya Tanzania, 2004 ilianza kutumika Julai, 2004. Sheria hiyo inaunda upya mfumo wa kodi ya mapato kulingana na mahitaji ya kisasa na kubatilisha Sheria ya Kodi ya Mapato, 1973. Kodi inatozwa kwenye mapato ya ajira, mapato kutoka kwenye biashara na mapato kutokana na uwekezaji. Watu wanaostahili kulipa kodi ni pamoja na vyombo na watu binafsi. Chombo kinaweza kuwa shirika au mfuko, udhamini na shirika linaelezwa kwa muhtasari kuwa ni chombo chochote kilichosajiliwa au kisichosajiliwa cha watu au chama. Kwa ubia, ni watu binafsi ndani ya ubia wanatozwa kwenye hisa zao za mapato. Kodi ni kwa mapato ya kimataifa ya wakazi (au watu binafsi, au wakazi wa zaidi ya miaka miwili). Wakati utozaji kodi kwa wasio wakazi ni kwa chanzo cha mapato ya Tanzania tu. Kiwango cha Kodi ya Shirika/Kampuni ni 30%. Kiwango cha kuanzia kutoza kodi binafsi ni Tsh.960,000 kwa mwaka na viwango vinaanzia 18.5% hadi kiwango cha juu cha 30%. Kodi mbalimbali za muda  na za zuio za mwisho zinatumika kwa kurahisisha ukusanyaji wa kodi.

Zaidi ya hayo, Tanzania inatoa motisha nzuri iliyowianishwa na ya ushindani katika biashara ya fedha hasa katika sekta za kipaumbele kama vile utengenezaji bidhaa, kilimo, utalii, mafuta ya petroli, gesi na madini. Katika sekta zote hizi, isipokuwa sekta za petroli na gesi, utwaaji wa bidhaa zote za mtaji na spea zimepewa kiwango cha sifuri kwa madhumuni ya ushuru wa bidhaa zinazoagizwa na VAT kucheleweshwa mpaka baadaye. Gharama za utafiti wa kilimo zinaruhusiwa kwa madhumuni ya kodi ya mapato, utwaaji wa mtaji unatozwa 100%. Unaweza pia kuagiza bidhaa zote za mtaji, spea, vifaa vya hoteli, vitu vya kulipuka kwa ajali ya gesi na utafutaji wa mafuta bila ushuru. Tanzania pia imetia saini mikataba ya kodi mbili na Denmark, India, Italia, Norway, Sweden, Kenya, Uganda, Zambia na Finland. 

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-05 16:07:58
Kufaa
3.8
6 Jumla
Inafaa Sana 3
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 2
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
4 Jumla
Rahisi Sana 4
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page