Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoUzalishaji Viwandani

Sekta ya Uzalishaji Viwandani nchini Tanzania inachangia kwa kiasi  9.9% (mwaka 2008). Utendaji wake katika miaka ya hivi karibuni umeonyesha mwenendo mzuri, viwango vya ukuaji haraka wa kila mwaka, uuzaji nje kwenye jumla ya mauzo umeongezeka kutoka 6.9% (2003) hadi 24.6% (2008). Mchango wake katika ajira inakadiriwa kuwa theluthi moja ya ajira binafsi isiyokuwa ya kilimo (viwanda na huduma). Ingawa kwa sasa sekta hii ni ndogo ina uwezo mkubwa wa ajira zenye malipo mazuri zaidi kuliko yale ya kilimo.

Muonekano wa maendeleo wa kuvutia zaidi umetokea kwenye bidhaa za matumizi ya chakula, vinywaji, mafuta ya kupikia, nguo na mavazi na metali. Katika baadhi ya shughuli ndogo, kumekuwa na kushuka kiasi  hasa mbao, karatasi, samani, mashine na mitambo. Bidhaa za kuuza nje kwa jumla zimebaki kuwa na uelewa mdogo na kiwango cha teknolojia na hivyo kuwa na thamani ndogo. Hii ni changamoto halisi wakati nchi inajitahidi kutimiza ajenda yake ya maendeleo. Kwa mujibu wa Program endelevu ya Maendeleo ya Viwanda(SIDP), Sekta ya Uzalishaji Viwandani inatarajia kuchangia kiasi cha 23% ya GDP ifikapo 2025 na mauzo ya nje kuongezeka hadi Dola za Marekani billion 5.2. Zaidi ya hayo kuna fursa mbalimbali katika sekta ya uzalishaji viwandani  nchini Tanzania.

Fursa hizo ni pamoja na: (i) Kuwapo kijiografia kwa nchi, kunakorahisisha kufikia masoko nje na masoko ya nchi za jirani zisizo na bandari (kama vile Burundi, Kongo, Malawi, Rwanda, Uganda na Zambia (ii) Kuanzishwa kwa Mipango ya Maeneo Maalum ya Kiuchumi, (SEZ) na Utengenezaji wa Bidhaa za Kuuza Nje (EPZ) itakayoongeza maendeleo na uwekezaji wa sekta, na (iii) Ukweli kwamba nchi ni mshiriki kwa ukamilifu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) unaohakikisha hufikia kwa urahisi masoko ya kanda. Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya Wizara ya Viwanda na Biashara

Sekta ya Viwanda Sekta ya biashara
Sekta ya Masoko Sekta ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati [SMES]
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Wakala wa Vipimo
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-06 06:00:00
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page