Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoElimu

Huduma ya elimu ni huduma muhimu ya kijamii na kiuchumi. Uwezo wa kiakili na kimwili wa binadamu ni masharti ya msingi ya maendeleo ya uchumi ya Taifa lolote. Utoaji wa huduma za elimu nchini Tanzania unafanywa chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi. Sekta zinazohusika kwa ukamilifu katika usimamizi na uongozi wa huduma za elimu nchini Tanzania ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Jamii, Asasi zisizo za Serikali (AZISE) na wananchi chini ya uratibu wa Serikali Kuu.

Mfumo rasmi wa Elimu Tanzania ni njia kuu ya kutoa huduma za masomo ya elimu kuanzia elimu ya awali hadi Chuo Kikuu. Kwa kuzingatia kwamba miaka ya awali ya maisha ni muhimu kwa ukuaji wa uwezo wa akili wa mtoto na uwezo wake mwingine, Tanzania imeamua kutekeleza muundo wa elimu wa 2-7-4-2-3+. Miaka miwili ya kwanza ni elimu ya awali ya shule za msingi, ambayo ni kwa watoto wenye umri wa miaka 5-6 (chekechea), miaka 7 ya elimu ya msingi, miaka 4 ya elimu ya sekondari ya kawaida, miaka 2 ya elimu ya sekondari ya juu, miaka 3 ya mwisho na kuendelea ni kwa vyuo vikuu na vyuo.

Sehemu hii inakupa taarifa kamili zinazohusu mfumo wa elimu na mafunzo wa Tanzania  ambao una miundo miwili na mfuatano wa ngazi za elimu na mafunzo kwa njia tatu ambazo ni  mafunzo ya Utaalamu, Ufundi Stadi na yasiyo-rasmi. Kwa maelezo zaidi tembelea  Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Elimu ya Chekechea Elimu ya Msingi
Elimu ya Watu Wazima na Elimu Isiyo Rasmi Elimu ya Sekondari
Elimu ya Ualimu Ukaguzi wa Shule
Elimu Maalum Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi
Elimu ya Juu
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-06 06:46:46
Kufaa
4.3
7 Jumla
Inafaa Sana 5
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 1
Urahisi wa kutumia
4.0
7 Jumla
Rahisi Sana 3
Rahisi Kiasi 3
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 1

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page