Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoKilimo

Kilimo ni msingi wa uchumi wa Tanzania. Kinachangia kiasi cha nusu ya pato la taifa., robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nchi za nje, kinachangia asilimia 95 ya mahitaji ya chakula nchini, kinachangia 25.7% ya GDP na 30.9% ya fedha za kigeni, hutoa ajira kwa 75% ya watanzania, bajeti ya serikali inayotengwa kwa kilimo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, hivi sasa imefikia zaidi ya asilimia 7.

Marekebisho ya kiuchumi kwa jumla yamekuwa na yanaendelea kuwa na matokeo makubwa katika sekta ya kilimo. Marekebisho ya kiuchumi yamesaidia kufungua sekta hii kwa uwekezaji binafsi katika uzalishaji na usindikaji, uagizaji pembejeo kutoka nje na usambazaji na utafutaji masoko ya kilimo. Kazi nyingi za uzalishaji, usindikaji na utafutaji masoko zimepangiwa sekta binafsi. Serikali inashughulikia maswala ya usimamizi wa kisheria na msaada kwa umma au uwezeshaji. Wakulima wako huru kuuza mazao yao kwa vyama vya ushirika au wafanyabiashara binafsi. Kutokana na ushindani bei za kawaida za mzalishaji kwa ajili ya chakula na mazao ya kuuza nchi za nje zimeongezeka sana kiasi kwamba hivi sasa mkulima anaweza kuuza mazao yake haraka sana. Hivi sasa wakulima hawalazimiki kutegemea chanzo kimoja cha pembejeo muhimu kwa ajili ya mazao na mifugo.

Pata taarifa za kina zinazohusu uboreshaji wa  sekta ya kilimo kama mhimili kwa upande wa ukuaji wa uchumi na upunguzaji umaskini katika sehemu hii ambapo umwagiliaji maji ni muhimu zaidi katika uzalishaji thabiti wa kilimo nchini Tanzania katika kuboresha uhakika wa chakula na kuongeza tija na mapato ya wakulima na pia kuzalisha mazao yenye thamani kubwa kama vile mboga na maua.

Sera Mipango ya Maendeleo
Ardhi ya Kilimo Teknolojia, Tafiti na Maendeleo
Elimu na Utafiti wa Kilimo Taasisi za Umma za Utafiti wa Kilimo
Umwagiliaji Kilimo cha kutumia mashine
Uzalishaji Mazao Mbegu
Mazao ya Bustani Masoko ya Kilimo
Usindikaji wa Mazao ya Kilimo
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-06 08:20:18
Kufaa
5.0
1 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
1 Jumla
Rahisi Sana 1
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page