Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoArdhi, Nyumba na Makazi

Tanzania ina eneo la ardhi la hekta milioni 94.3, kati ya hizo, hekta milioni 22 (23%) zipo kwenye hifadhi (ni kiasi kikubwa cha rasilimali ya ardhi kutengwa na nchi yoyote katika Nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara), zinazojumuisha Hifadhi za Taifa (hekta milioni 4.2), Mbuga za Wanyama (hekta milioni 7.7), na Hifadhi za Misitu(hekta milioni 10.1). Jumla ya eneo linalolimwa/kupandwa mazao kila mwaka ni kiasi cha hekta milioni 5.1; ambalo ni kiasi cha asilimia 5 ya jumla ya eneo la ardhi la Tanzania. Ardhi nyingine ya kilimo, lakini hailimwi, ni kiasi cha hekta milioni 10, sehemu kubwa ya ardhi inatumiwa kama malisho. Ndani ya hifadhi kuna hekta milioni 4 nyingine zinazofaa kwa kilimo.

Sheria ya Ardhi na Sheria ya Ardhi ya Vijiji kwa pamoja zinatoa Sheria ya Msingi kuhusiana na usimamizi na utawala wa ardhi, kutatua migogoro na masuala yanayohusiana na ardhi. Utekelezaji wa Sheria za Ardhi utaongeza haja ya kuwaarifu wadau wote kuhusu haki zao na wajibu, ili waweze kushiriki kwa ukamilifu katika utekelezaji wao. Kwa taarifa zaidi tembelea Tovuti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi

 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-06 09:07:04
Kufaa
3.3
3 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 1
Urahisi wa kutumia
4.0
1 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 1
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page