HOTUBA YA SHUKRANI YA RAIS MPYA WA
JAMHURI YA MUUNGANO WA
MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE,
UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM,
21 DESEMBA 2005
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi na
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa;
Mtukufu
Mfalme Letsie III wa Ufalme wa
Waheshimiwa
Viongozi Wakuu wa Nchi;
Makamu
wa Rais,
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein;
Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Mheshimiwa Amani Abeid Karume;
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili,
Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi;
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Mheshimiwa Pius Msekwa;
Spika
wa Baraza la Wawakilishi,
Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho;
Jaji
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Mheshimiwa Barnabas Samatta;
Jaji
Mkuu wa
Mheshimiwa Hamid Mahmoud Hamid;
Rais
Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Mheshimiwa Dkt Salmin Amour;
Waziri
Kiongozi wa
Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha;
Mawaziri
Wakuu Wastaafu;
Wakuu
wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama;
Viongozi
wa Serikali;
Viongozi
wa Vyama vya Siasa;
Viongozi
wa Dini;
Wageni
Waalikwa;
Ndugu
Wananchi;
Mabibi
na Mabwana:
Nimeelemewa na imani kubwa ambayo
ninyi Watanzania wenzangu mmeionyesha kwangu, na kwa Chama changu, Chama Cha
Mapinduzi (CCM). Kwa bahati mbaya, lugha
yetu ina mapungufu. Haina neno la shukrani linaloweza kubeba ujumla wa hisia za
shukrani nilizo nazo leo. Naomba kila
mmoja wenu aridhike tu nikisema: Ahsanteni
Nitapata fursa ya kuelezea jinsi
nitakavyojitahidi kutafsiri shukrani zangu kwa vitendo – kwa mipango na mikakati
ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi – nitakapohutubia
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Shukrani za kwanza kabisa ni kwa Chama
changu, CCM, kwa kunikabidhi usukani wa kuendesha utekelezaji wa sera
zake. Maana, Chama Cha Mapinduzi
kisingeridhika na uwezo wangu wa kutekeleza sera zake kisingenichagua niwe
mgombea wake wa Urais miongoni mwa wenzangu wengi wenye uwezo ndani ya Chama
chetu. Ninawashukuru wana-CCM wenzangu
wote waliojitokeza pamoja nami kugombea kuteuliwa. Walitumia haki
Ni vigumu kuwataja viongozi wa CCM, na
wana-CCM wenzangu, tulioshirikiana kufanya kampeni nchi nzima. Nawashukuru wote, kuanzia Mwenyekiti wa CCM,
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa; Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed
Shein; Rais Mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi; Makamu Wenyeviti wa CCM, ndugu yangu
Rais Amani Abeid Karume, na mzee wangu Mhe. John Samuel Malecela; Rais Mstaafu wa
Nyote nasema ahsanteni
Kwenye kundi hili la shukrani siwezi
kuisahau familia yangu – familia ya karibu, na familia ya mbali. Wamekuwa chemchem ya nguvu yangu, na nanga
iliyonituliza kwenye dhoruba. Nakushukuru
Shukrani za pili ni kwenu wananchi kwa
kukubaliana na Chama Cha Mapinduzi kuwa Jakaya Mrisho Kikwete ametosha na
anastahili kukabidhiwa usukani wa Serikali ya Awamu ya Nne. Kote nilikopita wakati wa kampeni wananchi
walinisubiri, wakati mwingine kwenye jua kali, na hata nilipochelewa
hawakuondoka; na nilipofika, walinisikiliza kwa makini na kunitia moyo. Watanzania wenzangu, ahsanteni
Shukrani zangu za tatu ni kwa viongozi
wakuu wa nchi rafiki, au wawakilishi wao, waliokubali mwaliko wa Rais
anayeondoka madarakani kuja kushuhudia Tanzania ikibadili awamu za uongozi wa
taifa, kwa mara nyingine, kwa amani na utulivu, baada ya uchaguzi huru na wa
haki. Na hawakuja kushuhudia tu. Ninaamini wametuletea baraka kwa kuja
kuungana nasi katika tukio hili la kitaifa, tukio la kihistoria. Ahsanteni
Ninamshukuru Rais aondokaye
madarakani, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, kwa busara zake, na kwa kuona
mbali, pale aliponikabidhi uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa kwa miaka kumi, Wizara ambayo ni sura ya nchi yetu nje ya nchi. Na hakunikabidhi Wizara tu; alikuwa pia mwalimu
wangu. Leo viongozi hawa waliokuja kutuunga
mkono si wageni kwangu, na mimi si mgeni kwao.
Ni mahali pazuri pa kuanzia kuongoza nchi. Ninayo maandalizi ya kutosha kutimiza azma ya
Sera ya Mambo ya Nje ya taifa letu ya kudumisha mahusiano mazuri na ushirikiano
na nchi zote zenye nia njema nasi, iwe ziko jirani au ziwe mbali nasi.
Juzi, wakati akiagana na Mabalozi
wanaowakilisha nchi zao hapa
Watanzania hatubomoi yale yaliyojengwa
na waliotutangulia, maana waliotutangulia ni miamba kweli kweli: Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere; Mzee Ali Hassan Mwinyi; na kaka yangu mpendwa, Benjamin William
Mkapa. Nikiwa nimetanguliwa na miamba kama
hii, nikiwa nimesimama juu ya mabega yao, kwa nini mimi Jakaya Mrisho Kikwete
nisitembee kifua mbele, kwa kujiamini; na kuendeleza yote mema yanayotokana na uongozi
thabiti wa miamba hawa walionitangulia?
Ndugu
Wananchi,
Mmenikabidhi wajibu huu, ni wajibu
mkubwa
Nilisema wakati wa kampeni, na leo
baada ya kuapishwa narudia. Serikali ya
Awamu ya Nne si ya kubeza au kupuuza yaliyoanzishwa na awamu za uongozi wa
taifa zilizopita. Haturudi nyuma;
tunaendelea mbele. Wanaotazamia
mabadiliko ya ajabu ya sera na mwelekeo wamepotea. Serikali ya Awamu ya Nne ni
ya kujenga juu ya yaliyofanywa na awamu zilizotangulia na kuendeleza yote mema
kulingana na mahitaji ya dunia ya leo, yenye heri kwa taifa letu, na kwa dunia yetu, tena kwa kasi
mpya, ari mpya na nguvu mpya. Na tushirikiane
sote kuhakikisha kuwa hatimaye juhudi tutakazoziongoza zitaleta maisha bora kwa
kila Mtanzania.
Kwa watani wetu kutoka vyama vingine
vya siasa, ninazo shukrani kwa kutuchangamsha wakati wa kampeni. Lakini sasa uchaguzi umekwisha, na ninawaomba
tushirikiane kuijenga nchi yetu. Ndugu
zetu, kabila la
Shukrani zangu za mwisho ni kwa wote walioandaa
shughuli hii, akiwemo Jaji Mkuu, na Kamati mbalimbali. Nayashukuru majeshi yetu yote kwa kutulinda,
na kwa gwaride zuri ajabu. Umakini na
umahiri wenu ni dhahiri. Mwenye macho haambiwi
tazama. Naona fahari kukabidhiwa uongozi
wa nchi, nikijua ninao watu hodari, na majeshi mahiri,
Watanzania
Wenzangu:
Kwa leo sina mengi zaidi ya kusema.
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki
Ahsanteni