HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA
Ndugu
Wananchi;
Ninayo furaha kwa mara nyingine tena
kuzungumza nanyi kupitia utaratibu huu mzuri wa mawasiliano baina ya Rais na
wananchi wa nchi yetu.
Jambo la kwanza ninalopenda
kulizungumzia linahusu uzingatiaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na kuishi
nchini.
Ndugu
Wananchi;
Tarehe 23 mwezi huu, nilimaliza
ziara ya siku kumi Mkoani Kagera. Jambo moja nililoliona kwenye ziara hiyo
ambalo sikufurahishwa nalo, ni ukiukwaji wa sheria na taratibu za uhamiaji na
uingizaji mifugo nchini.
Kwa muda sasa, raia wa nchi jirani
zinazopakana na Mkoa wa Kagera wamekuwa wakiingia na kuishi nchini mwetu kwa
vibali vya viongozi na watendaji wa vijiji na kata. Baadhi ya watu hao pia wamekuwa wakiingiza
mifugo kwa vibali vya viongozi hao hao.
Wageni hao wamekuwa wanaingia na
kuishi nchini isivyo halali. Sheria na taratibu za uhamiaji zinatoa mamlaka
hayo kwa Maafisa Uhamiaji tu na si vinginevyo.
Viongozi na watendaji wa vijiji na kata hawana mamlaka hayo. Hivyo basi,
vibali vyote walivyotoa viongozi hao si halali na havitambuliki. Napenda kurudia kauli yangu niliyoitoa Mkoani
Kagera kwamba ni marufuku kwa kiongozi au mtendaji wa ngazi yoyote ile nchini
kutoa kibali cha mgeni kuingia au kuishi nchini
Ndugu
wananchi;
Wageni wanaoishi nchini kwa kutumia vibali
ambavyo havikutolewa na Idara ya Uhamiaji wanaishi isivyo halali. Wenzetu hawa wanatakiwa kufanya yafuatayo.
Nilipokuwa Mkoani Kagera niliwaagiza
Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya kufuatilia utoaji wa vibali unaofanywa na
viongozi na watendaji wa vijiji na kata katika maeneo yao. Nimewataka
wawachukulie hatua zipasazo za kinidhamu watumishi hao wa umma pamoja na
kuwabana wahamiaji haramu kufuata sheria za uhamiaji za nchi yetu au warudi
makwao. Napenda kusema kuwa maagizo hayo
ni kwa Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya nchini kwani inawezekana matatizo haya
yanaweza kuwepo katika mikoa mingine.
Najua kwamba kuna Watanzania wenzetu
wanaohifadhi wahamiaji haramu kwa kuwa wananufaika kwa kuwafanya vibarua au
wafanyakazi wao. Ukweli unabaki pale pale kwamba wanatakiwa waingie na kuishi
nchini kwa kufuata taratibu zinazotambulika kisheria. Sheria za nchi, na sio
manufaa ya mtu au watu binafsi, ni lazima zizingatiwe.
Ndugu
Wananchi;
Jambo lingine baya linalofanyika
katika mpaka wetu na nchi jirani Mkoani Kagera ni kuruhusu mifugo kuingia
nchini holela. Hiki ni kitendo ambacho
kinakiuka taratibu zinazotawala uingizaji wa mifugo kutoka nchi za nje. Pia ni kitendo cha hatari kwani kinaweza
kupelekea mifugo yenye maradhi kuingia nchini bila kudhibitiwa na kusababisha
maafa makubwa nchini. Kanuni na taratibu zimewekwa kisheria kutawala mifugo
kuvuka mipaka na kuepusha hatari za namna hiyo zisitokee.
Jambo linalonishangaza ni kwa nini
viongozi wetu hawa hawajifunzi kutoka kwa majirani zetu. Wakati wote
tulipofanya zoezi la kurudisha makwao wakimbizi au wahamiaji wasiokuwa halali
na mifugo
Aidha, nimeelezwa juu ya kufahamika
kuwepo vivuko haramu kadhaa mpakani.
Nimesema nilipokuwa Kagera na narudia tena leo kwamba, maadamu vivuko hivyo
vimejulikana lazima tuvidhibiti. Kadhalika tuanzishe vituo mpakani vya
kupokelea mifugo na kila anayeingia na mifugo lazima apitie hapo na kupata
idhini husika. Nimetaka viongozi wenzetu
hao wasimuonee haya mtu yeyote anayeingiza mifugo nchini kinyume cha sheria na
taratibu zilizopo. Kadhalika viongozi na
watendaji wanaozembea wachukuliwe hatua kali za kinidhamu mara inapobainika kuwa
mifugo imeingia kinyume na taratibu
katika maeneo
Ndugu
Wananchi;
Jambo
la pili ninalopenda kulizungumzia ni matatizo yanayoukabili uchumi wa dunia
hivi sasa. Bado bei ya mafuta iko juu
Wakati huo huo tunaendelea na juhudi
za kuzalisha nishati mbadala kutokana na mimea hususan miwa, mawese na
mbono-kaburi (jatropha). Juhudi hizo
zikifanikiwa zitatusaidia kupunguza mzigo wa mafuta tunayoyaagiza kutoka nje. Nafurahi kwamba juhudi zetu zina muelekeo
mzuri na katika miaka michache ijayo tutaanza kunufaika na matunda yake. Pamoja na hayo tunaendelea na juhudi za
utafutaji wa mafuta na gesi asilia hapa nchini.
Mpaka sasa leseni 22 za utafutaji mafuta na gesi asilia zimetolewa na
kazi inaendelea katika hatua mbalimbali.
Tuzidi kumuomba Mwenyezi Mungu atujaalie rehema zake na sisi tujaaliwe
kugundua mafuta mengi hapa nchini yatakayotosheleza mahitaji yetu na ziada ya
kuuza nje.
Ndugu
Wananchi,
Tatizo lingine kubwa linaloukabili
uchumi wa dunia sasa linatokana na matatizo yanayoukabili uchumi wa Marekani. Uchumi wa taifa
Nimeelekeza wachumi wetu wafanye
uchambuzi wa kina juu ya athari hizo na kushauri hatua za kuchukua kupunguza
makali yake. Moja ya jambo ambalo liko
wazi ni lile la kushuka kwa thamani ya dola ya Kimarekani. Sisi tunaweka sehemu
kubwa ya akiba yetu ya fedha za kigeni katika dola za Kimarekani. Ni dhahiri kwamba kushuka kwa thamani ya dola
za Kimarekani kunatupunguzia uwezo wetu wa kuagiza bidhaa nchi za nje.
Uchunguzi wa Akaunti ya EPA
Ndugu
Wananchi;
Jambo
la tatu ambalo nimepanga kuliongelea leo
ni hili suala la ukaguzi wa Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje na hatua
zinazoendelea kuchukuliwa baada ya taarifa ya ukaguzi kutolewa.
Ndugu
Watanzania wenzangu;
Kwa
mara nyingine tena nawapongeza na kuwashukuru wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and
Young kwa kazi nzuri waliyoifanya na kutoa taarifa ya kina kuhusu matatizo
yahusuyo matumizi ya fedha za Akaunti hiyo. Nawashukuru pia Watanzania wenzangu
kwa kuunga mkono hatua tulizochukua na tunazoendelea kuchukua kuhusu suala la
Benki Kuu. Hata hivyo, nasikitishwa na taarifa ninazozipata kuhusu kuwepo uvumi
mwingi unaoenezwa na baadhi yetu kuhusu suala hili. Baadhi ya uvumi huo umekuwa unapotosha ukweli
na kuwachanganya wananchi. Napenda
kutumia nafasi hii kuwaomba wanaoeneza uvumi na uongo kuacha kufanya
hivyo. Aidha, nawasihi wananchi wawe
watulivu na wavumilivu.
Napenda kuwahakikishia kuwa,
Serikali inayo dhamira ya dhati ya kulifuatilia suala hili mpaka mwisho wake
ujulikane. Mwisho ambao utakuwa na maslahi kwa taifa letu. Pamoja na yote
yatakayofanywa, tunataka kuhakikisha kuwa fedha zilizolipwa kinyume cha
utaratibu zinarudishwa. Mwanasheria Mkuu
wa Serikali na wenzake, yaani Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU wameanza kuchukua hatua.
Nimewataka watoe taarifa kwa wananchi mara kwa mara kadri inavyowezekana
pamoja na haja ya kuwa waangalifu kutokutoa mengi yahusuyo uchunguzi wanaoufanya
ili ushahidi usiharibike.
Nawaomba Watanzania wenzangu tuwe na
subira. Naamini kazi hii itakamilika ndani ya kipindi cha miezi sita
tuliyowapa. Napenda kurudia ombi la Serikali kwa wananchi wenye taarifa
zitakazosaidia katika uchunguzi na hatua katika suala hili waisaidie kamati
yetu hiyo.
Ujio
wa Rais Bush
Ndugu Wananchi;
Natumai mmesoma na kusikia taarifa
katika vyombo vya habari kuhusu ziara ya Rais George W. Bush wa Marekani katika
nchi yetu kunako katikati ya mwezi Februari, 2008. Tunaendelea kukamilisha ratiba na itakapokuwa
tayari tutawapeni taarifa.
Napenda kutumia nafasi hii kuwaomba
Watanzania tumpokee mgeni wetu huyu kwa mujibu wa mazoea na desturi za ukarimu
wa Kitanzania. Huu ni ugeni mkubwa na wa
heshima kubwa kwa nchi yetu. Rais
Gerorge Bush ameipa heshima kubwa nchi yetu kwa kuamua kutumia sehemu kubwa ya
ziara yake ya Bara la Afrika hapa kwetu.
Ameonyesha upendo mkubwa kwetu nasi tumuonyeshe hivyo hivyo. Nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi siku
hiyo kumpokea mgeni wetu huyo mashuhuri.
Ziara hii ni uthibitisho wa kuimarika
kwa mahusiano kati ya Marekani na
Ndugu
Wananchi,
Wakati
wa ziara yake hapa nchini, Serikali ya Marekani inatarajia kutiliana sahihi
msaada mkubwa wa maendeleo unaoelekezwa katika kuboresha miundo mbinu ya
barabara, umeme na maji. Kwa msaada huo
utakaotolewa kupitia Programu ya Mfuko wa Changamoto ya Millenia utatusaidia
kutatua baadhi ya matatizo yaliyoonekana sugu katika baadhi ya maeneo hapa
nchini.
Pamoja
na hayo, ziara ya Rais George Bush nchini mwetu itasaidia kuitangaza nchi yetu
na kuinufaisha
Ndugu
Wananchi,
Wapo
watu miongoni mwetu na hata nje wanajaribu kueneza uvumi wa uongo na kuihusisha
ziara hii na masuala ya Makao Makuu ya Kamandi ya Afrika ya Jeshi la
Marekani. Ni uongo na uzushi mtupu. Ziara
hii haihusu hayo. Masuala hayo si agenda na wala Marekani haijaiomba
Hali
ya Kenya
Ndugu
Wananchi;
Jambo la tano ninalotaka
kulizungumzia ni hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi jirani na rafiki ya
Tunaahidi kuendelea kuiunga mkono
Kamati ya Mhe. Kofi Annan (Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa), Rais Mstaafu, Mhe. Benjamin Mkapa na Mama
Graca Machel. Viongozi wetu hao wanaifanya
kazi hiyo kwa niaba ya Umoja wa Afrika wanastahili msaada wetu na kuungwa mkono
nasi. Aidha, tutaendelea kushirikiana na
viongozi wenzetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kusaidia juhudi za
upatanishi. Napenda kutumia nafasi
kurudia tena yale maombi yangu kwa viongozi wa PNU na ODM na wananchi wote wa
Tutenganishe Uongozi na
Biashara
Ndugu
Wananchi;
Jambo la mwisho ninalotaka
kulizungumzia linahusu maadili ya uongozi nchini. Hususan napenda kulizungumzia suala la
viongozi wa siasa Mawaziri na Wabunge kuwa pia watu wanaojihusisha na shughuli
za biashara moja kwa moja. Upo ushahidi
wa kuwepo migongano ya maslahi kwa baadhi.
Lakini, pia, hata pale ambapo hakuna dalili za wazi, hisia za kupata
manufaa yanayotokana na nafasi zao hutawala.
Matokeo ya yote hayo ni watu kupoteza imani na kutilia shaka uadilifu wa
viongozi wetu.
Ndugu
Wananchi;
Nchi za wenzetu hasa zile za
kibepari zinazo taratibu nzuri za kushughulikia hali hizo. Wenzetu wanao utaratibu unaomtaka mtu mwenye
shughuli za kibiashara anapokuwa Mbunge au Waziri kuacha kujishughulisha na
biashara zake. Unakuwepo utaratibu rasmi
unaotambuliwa kisheria wa wadhamini wanaoendesha hizo shughuli bila ya yeye
kujihusisha nazo. Anapoacha uongozi wa
siasa kama atapenda atachukua tena
Ni makusudio yangu kuwa utaratibu
huu tuuanzishe hapa nchini. Viongozi
wetu wachague kufanya jambo moja kwa wakati mmoja ama biashara au Ubunge na
Uwaziri. Kwa ajili hiyo ni makusudio
yangu kuanzisha mchakato wa kufanya marekebisho ya Sheria ya Maadili ya Uongozi
ili tuingize utaratibu huo.
Ndugu
wananchi;
Ni jambo lenye maslahi kwa nchi yetu
na litasaidia
Mwisho,
nawatakia kila la heri kwenye shughuli zenu. Tuendelee kushirikiana kuijenga na
kuiendeleza nchi yetu.
Asanteni