| .
Majaliwa
ya rasilimali ya madini
§
Almasi
§
Dhahabu
§
Metali za besi na kundi la
platinamu
§
Metali za chuma
§
Bati
§
Vito
§
Kaboneti
§
Makaa ya mawe
§
Madini ya viwanda
§
Sera ya sekta ya madini
§
Marekebisho ya sekta ya madini
§
Vyama vya wataalamu
Sekta
ya madini inachangia takribani asilimia 2.3 ya pato la Taifa,
ambayo inakadiriwa kufikia asilimai 10 ifikapo 2025. kama ilivyo
kwenye dira ya maendeleo 2025. madini ni sehemu muhimu inayoongoza
katika pato la kigeni kati ya mauzo yasiyo asilia.
Aidha ina uwezo mkubwa wa ajira na inayongoza katika kuupa
nguvu uchumi wa Tanzania.
Rasilimali
ya madini
Tanzania
ina madini mengi, na hasa dhahabu, metali za besi, almasi, madini
ya chuma na aina kadhaa za vito, vingi vikiwa vya aina ya pekee
kama tanzanaiti. Mengine
ni makaa ya mawe, urani na madini ya viwandani kama magadi, kauri,
jasi, fosfati na mawe mbalimbali yanapatikana kwa bei nzuri.
Yafuatayo ni madini yanayovutia wengi:
§
Dhahabu hupatikana katika ukanda
wa mawe kijani uliopo mashariki na kusini mwa Ziwa Victoria, na
mfumo wa miamba iliyopo kusini na kusini magharibi mwa Tanzania.
§
Metali za bezi zinapatikana
ukanda unaoanzia Kagera kupitia Kigoma hadi Mikoa ya Mbeya, Rukwa
na Mtwara.
§
Vito vinavyopatikana ukanda wa
mashariki na magharibi kutoka mpakani mwa Kenya, kaskazini mwa
Msumbiji, na Mikoa ya Mbeya na Rukwa.
§
Dhahabu na almasi ndiyo madini
makuu nchini.
Almasi
Tanzania
ni mzalishaji mkubwa wa almasi kwa miongo kadhaa kutoka machimbo
ya Williamson, Mwadui ambako uchimbaji wa kibiashara ulianza 1925.
Miamba 300 ya kimbalaiti ipo Tanzania na asilimia 20 yake
ina sifa za kuwa na almasi.
Dhahabu
Dhahabu
ni eneo zuri sana la kuwekeza. Wasaa wa sasa upo kwenye machimbo ya zamani katika mfumo wa
miamba ya ukanda wa Archaean Greenstone kando kando ya ziwa
Victoria, na miamba michanga ya proterozoki. Uchimbaji wa dhahabu
umeongezeka kwa kasi miaka ya 90 kwa kutumia teknolojia ya kisasa
na mbinu mpya.
Mashapo
makubwa ya dhahabu
yamegundulika eneo la Ziwa Victoria na yapo katika hatua
mbalimbali za uchimbwaji. Dhahabu pia imegunduliwa kusini
magharibi mwa Tanzania.
Metali
za Bezi na Kundi la Platinamu
Kijiolojia,
miamba ya Archaean na Proterozoki ina uwezekanao wa kuwa na metali
za bezi na kundi la platinamu.
Ugunduzi wa hivi karibuni kaskazini magharibi mwa Tanzania
umeonesha kuwepo kwa hazina kubwa ya madini ya nikeli, kobati na
shaba iendanayo na mfumo wa miamba ya Karagwe-Ankole.
Zaidi
ya hapo, kundi la metali za kroniumu na platinamu limeonekana.
Hazina kubwa ya nikeli iliyo na ngegu pamoja na kobati
imebainika. Kuna
akiba ya shaba, fedha na urani mkoani Shinyanga.
Metali
za chuma
Mawe
yenye madini ya chuma yametambulika kwenye miamba ya proterozoki
huko Liganga kusini magharibi mwa Tanzania karibu na makaa ya mawe
ya Ketewaka-Mchuchuma. Madini
ya titani yanapatikana kwenye mchanga wa pwani ya bahari pia.
Bati
na madini ya kutengeneza chuma cha pua
Bati
na madini ya kutengeneza chuma cha pua na filameni za taa za umeme
yanapatikana Karagwe kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Vito
Tanzania
imejaliwa aina nyingi za vito ikiwemo Tanzanaiti inayopatikana
kwenye mfumo wa miamba ya Usagara na Ubendi. Tanzanaiti inachimbwa
Mererani.
Vito
vingine vinavyochimbwa nchini ni rubi, rodolaiti, johari ya rangi
ya samawati, zumaridi, ametisti, krisoprase, peridoti na
tormalini. Hivi
karibuni ugunduzi ulifanywa Mkoani Ruvuma, Mtwara na Lindi wa
krisoberi, spineli, zumaridi, ganeti, zikoni na almasi.
Mauzo
nje ya vito yalikaribia US $ 10 millioni mwaka 1996, na vingi
vikiwa ghafi. Kuna
nafasi kubwa ya kuwekeza katika usanifu na unakishaji wa tasnia ya
vito.
Kaboneti
Zaidi
ya kaboneti 20 zinazohusiana na volkano zimebainishwa nchini, na
ambazo zimekuwa chanzo cha elementi adimu kama nibimu na fasfati.
Makaa
ya mawe
Hazina
ya makaa ya mawe iliyo na ubora sawa na ile ya Gondwana Afrika ya
Kusini, inapatikana Ruhuhu na Songwe-Kiwira Kusini-Magharibi mwa
Tanzania. Jumla ya
tani za akiba 1.5 billioni zimegunduliwa.
Machimbo pekee ya mkaa wa mawe yapo Kiwira, yenye kuzalisha
tani 35,000 kwa mwaka, na yote yakitumiwa hapa nchini kwa
kuzalisha umeme.
Madini
ya viwandani
Chokaa
ya mawe yenye usafi mkubwa inapatikana kama marumaru nyeupe Mkoani
Morogoro.
Udongo
wa mfinyanzi aina mbalimbali kama bentonaiti, kauri na mfinyanzi
wa kutakasia vitambaa unapatikana kwa vingi, na umetumiwa kidogo
sana. Amana kubwa ya
kauri iiliyopo Pugu, kilomita 30 magharibi mwa Dar es Salaam, ina
nafasi kubwa ya kuendelezwa.
Chumvi
na madini mengine yanayoyeyuka yenye umuhimu kiuchumi inahusiana
na maziwa ya bonde la ufa. Uchunguzi
wa magadi Ziwa Natron umeonyesha kuna uwezekano wa kupata zaidi ya
tani milioni moja kwa mwaka.
Uzalishaji wa chumvi hivi sasa ni tani 105,000 kwa mwaka.
Grafati
ya gredi ya juu inapatikana kwenye mfumo wa mwamba wa Usagara.
Akiba ya kutosha imebainishwa Mererani, Tanzania kaskazini,
yenye kuweza kuchimbwa kwa miaka 40 kwa kiasi cha tani 15,000 kwa
mwaka, na iliyo na usafi wa 97-98%. Machimbo hayo hutoa pia tanzanaiti ambayo hupatikana kwa
pamoja na grafati.
Fosfati
inachimbuliwa Minjingu Mkoani Arusha, na takribani tani 48,000 kwa
mwaka hutumiwa katika uzalishaji wa mbolea. Kutokana na kufungwa
kiwanda cha mbolea cha Tanga, matumizi ya sasa ni ya moja
kwa moja mashambani.
Sera
ya Sekta ya Madini
Sera
ya Madini Tanzania ya mwaka 1997 inasisitiza juu ya sekta binafsi
kuendeleza madini, na wakati huo huo Serikali ikiwa na jukumu la
kuidhibiti, kuikuza na kuiwezehsa kuendelea.
Jukumu la umma, pamoja na mengine ni:
¨
Utungaji wa sera itakayojumuisha
mfumo mzima wa Sera za Serikali
¨
Kushauri juu ya sheria, taratibu
na masuala ya fedha yahusyo sekta.
¨
Kukusanya mapato kutoka mirabaha,
pango la mwaka, haki za uchimbaji na leseni.
¨
Kufuatilia shughuli za uchimbaji
madini .
¨
Kukusanya na kuweka takwimu za
kiufundi za kijiolojia, kwa madhumuni ya kujitangaza, na kutoa
huduma za ugavi kwa wachimbaji wadogo
¨
Kusimamia na kukagua shughuli za
uchimbaji madini.
Malengo
ya Sera za Madini ni:
§
Kuhamasisha ugunduzi na uchimbaji
madini.
§
Kudhibiti na kuboresha uchimbaji
mdogo mdogo.
§
Kuhakikisha kuwa utajiri utokanao
na madini unasaidia uchumi endelevu na maendeleo ya jamii, kuondoa
au kupunguza athari mbaya ziwezazo kutokea kwa jamii na mazingira
kutokana na shughuli za uchimbaji madini.
§
Kukuza na kuwezesha bidhaa
zinazohusiana na madini kuwa na soko.
§
Kupunguza umaskini, hasa wa
wachimbaji wadogo
§
Kukuza na kuendeleza Tanzania
kama kituo cha vito Afrika
Sheria
na Udhibiti wa Sekta ya Madini
Yanayojitokeza
katika Sheria ya Madini 1998 ni yafuatayo:
I.
Haki ya kufanya biashara ya hati za madini.
II.
Kurahisisha na kuweka pamoja sheria za zamani za uchimbaji
na biashara ya madini.
III.
Kuboresha haki ya umilikaji kwa kuondoa uwezo wa Wizara na
kuweka kamati ya ushauri itakayaomshauri Waziri juu ya maamuzi ya
kufanywa.
§
Kukuza uwazi
§
Taratibu za utoaji leseni zilizo
za haki, zisizo na mizengwe na zisizobagua
§
Kusimamia mazingira
Sheria ya Madini Tanzania inakataza
kuhodhi habari za uvumbuzi mpya, kushikilia maeneo ya kiuchunguzi
kwa lengo la kuyalangua, kuhamisha uwekaji bei na ukwepaji kodi. Motisha ya kifedha kwa anayetafiti ugunduzi na uchimbaji wa
madini, ni pamoja na :
§
Msamaha wa kodi ya uingizaji
nchini na VAT kwa vifaa na bidhaa muhimu hadi atakapoanza
kuzalisha; baada ya
hapo atalipia asilimia 5.
§
Kipunguzi cha uchakavu asilimia
10.
§
Kuhamisha mtaji na faida
itokanayo na madini,
na
§
Ushiriki wa Serikali kwa
ridhaa.
Urekebishaji
wa Sekta za Madini
Kama
zilivyo Sekta nyingine za uchumi nchini, sekta ya madini
iliingizwa kwenye marekebisho yaliyofanywa na Serikali miaka ya 80
na 90, yanayopendelea zaidi maendeleo ya sekta binafsi na
kutawaliwa na nguvu za soko.
Kwa msingi huu. Serikali inakaribisha ubia wa kuendeleza
wenye shauku sekta binafsi na kuchochea kukua kwa uchumi.
Kutokana na mabadiliko haya, jukumu la Serikali
limebadilika, kutoka kuwa mmiliki na mwendeshaji na kuwa anayetoa
sera zilizo wazi, kuhamasisha uwekezaji binafsi na kusaidia
wawekezaji.
Marekebisho
haya ni kwa mujibu wa Sera ya Madini Tanzania 1997, Sheria ya
Madini 1998, na Vivutio vya Kumotisha 1998.
Vyama
vya Kitaalam
Chama
cha Wasafirishaji Madini
Nje Tanzania
Chama
cha Kijiolojia Tanzania.
|