| .
Upatikanaji
wa maji salama ni muhimu katika kupigana na umaskini na matatizo
ya afya. Watu maskini
ambao wengi wao huishi vijijini wana nafasi finyu ya kupata maji
safi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwa ajili ya mazao na
matumizi ya afya. Faida za uchumi zinaweza kupatikana siyo kwa
njia ya moja kwa moja tu bali kwa kuwa na afya bora na kuokoa muda
unaotumika kuhangaika na kazi za kuchosha za kubeba maji kwa
umbali mrefu. Takwimu
zinaonyesha kuwa magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya maji
hupatikana zaidi katika sehemu ambapo watu wanatumia maji
yaliyoambukizwa au hawana maji ya kutosha kwa matumizi yao ya kila
siku.
Idadi
ya magonjwa hayo ni zaidi ya nusu ya magonjwa yanayowaathiri watu
na kwamba asilimia themanini ya magonjwa yanayowashambulia
watanzania wanaoishi vijijini.
Serikali inalenga katika upatikanaji wa maji vijijini.
Usimamizi wa maji pia unawashirikisha washika dau wote kwa
ajili ya kufanikisha upatikanaji wa maji wa kutegemewa, unaofaa na
maji hayo yanatumika ipasavyo, yanalindwa na kuhifadhiwa.
Sehemu
moja ya tatu ya Tanzania inapokea chini ya milimeta 800 ya mvua na
hivyo kusababisha sehemu hiyo kuwa kavu au nusu jangwa.
Ni
sehemu moja tu ya nchi ambayo hupata zaidi ya milimeta 1000 za
mvua. Aidha, msimu wa
kiangazi, ambao hudumu kuanzia mwezi Juni hadi Oktoba hupunguza
mtiririko wa maji katika mito na maji hukauka kwenye mabwawa.
Lakini asilimia 7 ya Tanzania hufunikwa na maziwa ya maji
kwenye mipaka yake licha ya maziwa mengine ya maji ambayo
yako ndani ya nchi.
Maziwa
hayo ya maji ni
pamoja na Ziwa Victoria (Ziwa la maji baridi la pili kwa ukubwa
duniani), Ziwa Tanganyika (la pili kwa kina kirefu duniani), na
Ziwa Nyasa. Maziwa ya
maji ambayo yako ndani ya nchi ni pamoja na maziwa Rukwa, Eyasi na
Manyara. Ipo pia mito
mingi mikubwa ambayo humimina maji kwenye maziwa.
Maji yaliyo chini ya ardhi pia ni chanzo kingine cha maji
kwa ajili ya maeneo ya makazi ya mijini na vijijini.
Matumizi
makubwa kuliko yote ya maji ni ya nyumbani.
Kutokana na shughuli za kiuchumi na za kuhudumia jamii
ambazo, kwa njia moja au nyingine, zote zinatumia maji,
upatikananji na usambazaji wa maji umekuwa ni mzigo mkubwa kwa
serikali ambayo haiwezi kuubeba peke yake bila ya ushirikiano wa
sekta bianfsi. Nia
ya sera ya serikali kuwashirikisha wafadhili katika mirdi
yote ya maji mijini na vijijini.
Kwa muda mrefu mchango wa sekta ya maji kwa pato la taifa
(GDP) limebaki kuwa asilimia 0.2 ambacho ni kiwango kidogo sana
ikitilia maanani umuhimu wa sekta hii katika uchumi kwa
kulinganisha na sekta, kwa mfano ya kilimo ambayo kwa mwaka 1999
ilichangia asilmia 48.9 ya pato la taifa.
Lakini maji kwa vyovyote vile, ni muhimu zaidi katika
kukuza maendeleo ya uchumi wa Tanzania kwa sababu sekta khiyo
inaunganisha sekta nyingine zote kwa mfano, hata kilimo ambayo ni
sekta kubwa kuliko zote, haiweze kufua dafu bila maji kwa bahati
nzuri, maji nchini Tanzania ni sekta ambayo ina uwezo wa kukua
ikilinganishwa na sekta nyinginezo mwaka 1999 maji yalichangia
kwenye pato la taifa ongezeko la asilimia 3.0.
hivyo, Serikali inahamasisha uwekezaji binafsi katika sekta
hiyo ya maji.
Vyanzo vya maji vilivyopo:
Tanzania
ina vyanzo vya kutosha vya maji kukidhi mahitaji yake, na vyanzo
hivyo ni pamoja na maji yaliyo juu na chini ya ardhi.
Asilimia 7 ya ardhi imefunikwa na maziwa ya maji matamu
ambayo yako mpakani licha ya maziwa mengine ambayo yako ndani ya
nchi.
Hata
hivyo kuna tofauti kubwa ya kuwepo kwa maji katika sehemu
mbalimbali za nchi. Tofauti
hiyo inatokana na tabia ya mahali, mvua na hali ya hewa.
Maji yaliyo juu ya ardhi
Vyanzo
vya maji yaliyo juu ya ardhi yanatokana na maziwa ya maji, mito,
chemichemi, mabwawa na maziwa ya maji yaliyotengenezwa na
binadamu. Asilimia 50
ya maji yaliyo juu ya ardhi yanapatikana kwenye mito ambayo
humwaga maji yake moja kwa moja katika Bahari ya Hindi.
Mito hiyo ni ya Pangani, Wami, Mkondoa, Ruvu, Rufiji,
Ruaha, Mbwemkulu, Lukuledi na Ruvuma. Asilimia 50 ya maji ya juu iliyobaki imegawanywa katika maji
ambayo hutiririka na kuishia katika mabonde bila kufika baharini.
Maji hayo yanaishia Ziwa Rukwa, Bonde la Bubu, Ziwa Eyasi
na Ziwa Manyara. Maji
ya mito mengine hutiririka katika Ziwa Victoria (mito Meri, Maru
na Kagera), mto Malagarasi humwaga maji yake katika Ziwa
Tanganyika na mto Songwe na Ruhuhu inatiririka kuelekea kusini na
kumwaga maji katika mfumo wa Ziwa Nyasa – Zambezi.
Mabwawa
Tanzania
ina hekta 5,439,000 za maziwa na mabwawa ambayo ni asilimia 5.8 ya
ardhi yote ya nchi, lakini asilimia hiyo haijumuishi mabwawa
ambayo hutokana na mafuriko ya msimu wa mvua.
Mfumo
wa kuchukua maji
Tanzania
imegawanywa katika mifumo mitano ya kuchukua maji yanayotiririka
kutoka mito yake. Mifumo
hiyo ni:
1.
Mfumo wa kuchukua maji yanayoingia katika Bahari ya Hindi.
2.
Mfumo wa maji yaingiayo katika Ziwa Eyasi, Natron na Bonde
la Bubu.
3.
Mfumo wa Ziwa Rukwa.
4.
Mfumo wa
Bahari ya Atlantic na
5.
Mfumo wa Bahari ya Mediterranean.
Vyanzo vya maji yaliyo chini ya Ardhi
Maji
yaliyoko chini ya ardhi ni chanzo kikubwa cha maji katika maeneo
mengi ya Tanzania na ni njia nyingine ya nyongeza ya kuaminika ya
kupata maji katika maeneo ya kati na kaskazini ya nchi ambayo
yanakabiliwa na ukame katika mikoa ya Dodoma, Singida,
Shinyanga, Tabora, Mwanza, Mara, Arusha, Pwani na kusini mwa
Kilimanjaro.
Sera ya Sekta ya Maji
Maendeleo
ya sekta ya maji nchini Tanzania inaongozwa na sera ya sekta ya
maji. Sera
inayotumika ni ile iliyotolewa mwaka 1991.
Hivi karibuni serikali imeanzisha marekebisho ya mpango
ambao utahusisha sekta zote za jamii, uchumi na siasa ikiwemo na
ya maji. Hivyo sekta
ya maji imeongezewa nguvu kwa mpango unaoendelea kwa kurekebisha
sekta hiyo ambayo itastawisha
sera ya maji katika kuimarisha masuala ya usimamizi na utendaji
kwa kuzingatia yafuatayo:
¨
Maji
hustahili kufikiriwa kuwa ni hitaji la msingi.
¨
Sera
ya Serikali ina nia ya
kufanikisha mpango wa upatikanaji wa maji safi na salama na
ya uhakika katika maeneo ya vijijini na mijini.
¨
Lengo la sera ni kuhakikisha kuwa
maji safi na salama yanapatikana katika umbali usiozidi mita 400
kutoka sehemu wanazoishi watu.
¨
Shughuli za kuendeleza na
usambazaji wa maji ziongozwe na soko huru ambapo wote wanaohusika,
kama vile jamii, sekta binafsi vyama visivyo vya kiserikali viwe
vya hapa nchini au nje ya nchi viweze kuwekeza katika sekta hii
ili kusaidia juhudi za serikali katika kuendeleza na upatikanaji
wa huduma za maji.
¨
Serikali itaamsha jitihada za
kuishirikisha sekta binafsi na wahisani katika huduma ya
upatikanaji wa maji kwa madhumuni ya kuongeza ufanisi na uwezo na
hivyo kujenga huduma za maji zinazotegemewa.
Jukumu na kazi za Serikali
Wakati
sekta ya maji ni eneo huria kwa vyombo vya aina yote vyenye moyo
wa kuipenda sekta hiyo, Serikali kwa kupitia wizara yenye dhamana
ya maji ina wajibu na kazi kuu zifuatazo:
¨
Kuendelza, kukagua na kukuza sera
ya maji safi na maji taka.
¨
Kuhimiza, kushirikisha, kusimamia
na kuratibu huduma za maji safi na maji taka kwa ajili ya watu
wote kwa kutilia maanani masuala
ya jinsia.
¨
Kuwaendeleza wataalam wenye uwezo
mkubwa kushughulikia sekta hiyo.
Sheria
Usimamizi
na taratibu za kuongoza masuala ya maji uko katika Control and
Regulation Act Na 42 ya mwaka 1974 na Sheria ya
marekebisho Na. 10 ya 1981 pamoja na Miscellaneous Act No.
17 ya 1989. Sheria
kama ilivyorekebishwa, imetamka kuwa maji yote ya nchi yako chini
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeweka taratibu za matumizi
ya maji na kumpa madaraka Afisa Mkuu wa Maji kutayarisha sera na
kugawa haki ya kutumia maji kwa ngazi ya kitaifa.
Maji ambayo yako kwenye mabonde yatakuwa chini ya ofisi za
maji ya Bondeni anayewajibika na maji hayo ni Afisa maji wa Bonde.
Utendaji kazi wa sekta
Hadi
sasa maji mengi yanayotumika ni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Ingawa asilimia 80 ya watu wanaishi vijijini na asilimia 20
tu wanaishi mijini, maji mengi zaidi hutumika vijijini.
Hata hivyo, licha ya umuhimu mkubwa wa maji ambao
haujionyeshi, vyanzo vingi kvya maji bado viko duni na kwamba
idadi kubwa ya watu wanatumia maji kutoka vyanzo duni
havikutengenezwa. Vyanzo
hivyo duni ni maziwa ya maji,
mito, mabwawa, visima vifupi na vya wazi.
Hadi kufikia mwaka 1999, asilimia 45 wa watu waishio
vijijini na asilimia 68 ya watu wanaoishi mijini wana uwezo wa
kupata maji safi na salama. Wakati
tarakimu hizo zinaonyesha wastani tu wa kitaifa lakini hali halisi
inatofautiana sana kati ya sehemu na sehemu kadiri ilipo
kijeografia.
Kuhusu
huduma ya maji machafu, maeneo mengi ya mijini huendelea
kuathirika na huduma duni inayotolewa.
Ni asilimia 7 tu ya wakazi wa mijini ambao huduma zao za
maji machafu zimeunganishwa kwenye huduma iliyoko ya mifereji ya
maji taka ambayo hupatikana kwenye miji michache tu na kwamba
mifereji hiyo ilijengwa miaka mingi iliyopita.
Washika Dau wakubwa wa Sekta ya Maji.
Ni
kutokana na sera ya maendeleo ya nchi ambayo kwa muda mrefu
imeweka mkazo mkubwa wa kuendeleza sekta za jamii, ikiwemo ya
maji, aidha, na ni kutokana na sera ya maji ambayo imewahamasisha
washika dau wengine (mbali ya serikali) kushughulika na maendeleo
ya sekta ya maji, ndiyo maana hii leo Tanzania inayo orodha ndefu
ya mashirika ya serikali na ya watu binafsi wanao shughulika
katika kuendeleza na kusambaza huduma za maji safi na maji taka..
Nafasi za kuwekeza
Ziko
dalili zinazoashiria kuwa zipo nafasi na faida za kuwekeza katika
sekta ya maji kwa wakati huu na miaka mingi ijayo kama ifuatavyo:-
¨
Kiko chanzo kikubwa sana cha maji
ambacho bado hakijatumiwa kwa kupata faida.
¨
Yako mahitaji makubwa ya
huduma kwa ajili ya sekta ya maji ambayo bado
hayajashughulikiwa na kwamba mahitaji bado yanaongezeka kadiri
idadi ya watu
inavyokuwa na wa maendeleo ya uchumi yanavyongezeka.
¨
Sera ya sasa ya Serikali ni
kuziendeleza kuzishirikisha sekta nyingine katika kufanikisha
sekta za jamii ikiwemo sekta ya maji.
¨
Iko tayari idadi kubwa ya
mashirika yaliyowekeza katika sekta khii ambayo tayari yana uzoefu
wa kujivunia na ambayo yako tayari kutoa nafasi ya kuingia ubia na
mwekezaji mwingine yeyote.
¨
Sekta ya maji inayo maeneo mengi
ya kuweza kuwekeza kama vile katika kuhifadhi maji au katika
ujenzi wa miundo mbinu (kwenye vyanzo vya maji, chemchem), au
kuwekeza katika utengenezaji au upatikanaji wa mashine, vifaa
pamoja na kuendesha mafunzo ya watalaamu.
|