Maisha ya Watanzania wa leo na vizazi vijavyo, yanategemea maliasili ya nchi. Tanzania imebahatika kuwa na rasilimali nyingi ikiwemo misitu, wanyamapori, mito, maziwa na maeneo kinamasi. Rasilimali hii ni muhimu kwa utoaji wa huduma kiuchumi na kijamii. Kufifisha rasilimali hii ni kuharibu mazingira endelevu ya shughuli za kiuchumi.
Rasilimali ya Uvuvi na Ugavi
Tanzania ina pwani yenye rasilimali nyingi za uvuvi. Ina mwambao wa bahari wenye kilomita za mraba 64,000 pamoja na kilomita nyingine za mraba 223,000 za Eneo la Uchumi la Bahari ya Hindi.
Eneo la maji baridi ni pamoja na maziwa Makuu Victoria, Tanganyika na Nyasa. Kuna maziwa mengine madogo, mabwawa, mito na maeneo kinamasi yenye kuweza kukaa samaki. Maeneo haya yana kilomita za mraba 58,000. Tanzania ina mwambao wa pwani wenye urefu wa kilomita 800 uliotengwa kwa shughuli za kiuchumi, lakini hautumiwi. Mavuno ya samaki kwa mwaka ni tani za metriki 350,000.
Kuna wavuvi wapatao 80,000 na wengine wachache wapatao riziki kwa kuajiriwa katika shughuli zinazohusiana na uvuvi. Wavuvi wadogo wanavua asilimia 90 ya samaki wote wanaovuliwa nchini, na asilimia 10 huvuliwa kwa njia za kibiashara. Sehemu kubwa ya samaki wanaovuliwa hutumika ndani ya nchi; wakati sangara, sadini na kamba huuzwa nje ya nchi. Samaki huchangia theluthi moja ya lishe ya protini kwa Taifa. Rasilimali ya uvuvi hutoa ajira, ni chakula, burudani na ni kivutio kikubwa cha utalii kinachoingiza fedha za kigeni katika Pato la Taifa. Mchango wa sekta kwa Pato la Taifa kwa kipindi cha miaka mitano umekuwa kati ya asilimia 1.6 na 3.1.
Maliasili ya uvuvi humalizika, hivyo lazima ilindwe, isimamiwe na kuendelezwa kwa misingi endelevu. Sera ya uvuvi ya sasa imelenga kuondoa matatizo yanayoikabili sekta, na kuainisha hatua zitakazochukuliwa. Mkazo umetiliwa katika uvunaji endelelevu, utumiaji na masoko, ili kuleta manufaa ya kiuchumi ya kuwezesha kulinda na kuhifadhi mazingira ili kuwe na maendeleo ya kudumu. Sekta binafsi, tasasi za kijamii zisizokuwa za kiserikali na washika dau wengine, wana wajibu mkubwa katika kufanikisha maendeleo endelevu ya sekta. Hii inatokana na ujuzi mbalimbali walio nao, utaalam na uwezo katika sekta. Mchango wao ni muhimu ili kufanikisha malengo ya sekta. Uchangiaji utaongeza uwekezaji, utaboresha biashara na uendeshaji kwa jumla wa tasnia ya uvuvi.
Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (FAFIRI)
Utafiti unafanyika kwenye maji baridi na ya chumvi. Taasisi inaendesha utafiti wa rasilimali ya uvuvi na usambazaji wa matokeo ya utafiti huo kwa lengo la kuendeleza na uendeshaji endelevu wa rasilimali hiyo. Aidha Taasisi inatoa mafunzo na kutafiti teknolojia ya zana za uvuvi na tathmini ya wingi wa samaki.
Anwani:
Wizara ya Maliasili na Utalii
Idara ya Uvuvi
S.L.P. 2462
Dar es Salaam
TANZANIA
TEL: 255-22-2650043/44
Taasisi ya Mafunzo ya Uvuvi Kunduchi
Inatoa mafunzo ya stashahada ya uvuvi. Mafunzo haya ni pamoja na uhandisi wa majini, kuvua, biolojia ya viumbe wa majini, teknolojia ya chakula na sayansi ya mwendo katika maji.
Anwani:
Taasisi ya Mafunzo ya Uvuvi Kunduchi
S.L.P. 60091
Dar-es-Salaam
TANZANIA
TEL: 255-22-2650011
Kituo cha Maendeleo ya Uvuvi Mbegani
Kinatoa mafunzo ya stashahada ya uvuvi, ikiwemo ujenzi wa mashua, usindikaji wa samaki, masoko, kuthibiti ubora, ufundi na uhandisi wa vyombo vya majini, na kozi mbalimbali kulingana na matakwa ya
mteja.
Misitu
Tanzania ina hekta zipatazo 33.5 milioni za misitu na mwitu. Theluthi mbili ya eneo hili ni la mwitu wa umma usiokuwa na usimamizi maalum. Karibu hekta 13 milioni zimeorodheshwa kuwa ni hifadhi ya misitu. Zaidi ya hekta 80,000 za eneo hili ni misitu iliyopandwa, na karibu hekta 1.6 milioni hulindwa kama vianzio vya maji. Misitu hutoa hifadhi kwa wanyama, ufugaji nyuki, ikolojia asilia na rasilimali ya jenetiki. Pia nishati itokanayo na mimea ni asilimia 92 ya nishati yote itumiwayo nchini. Hata hivyo inakadiriwa kuwa mchango wa sekta katika pato la ndani la Taifa ni kati ya asilimia 2.3 ya mauzo ya nje yaliyoandikishwa. Mchango huu ni kadirio pungufu kwa sababu haujumuishi matumizi ya kuni na mkaa, asali, vyanzo vya maji, na thamani kwa mazingira na mazao mengine ya misitu.
Thamani ya msitu wa Tanzania ni ya juu kwa sababu ya mrabaha unaoweza kukusanywa na hivyo kuongeza mapato ya nchi kutokana na mazao ya kuuza nje na mapato ya utalii. Thamani nyingine ni pamoja na kutengeneza dioksidi ya kaboni, na uhifadhi wa viumbehai adimu duniani. Sekta inatoa miaka-mtu ya kazi 730,000 ambao wameajiriwa katika shughuli zinazohusiana na misitu. Mchango halisi haufahamiki kwa sababu nguvukazi inayokusanya kuni na mkaa unaotumika majumbani haifahamiki. Tasnia ya mbao inachangia nusu ya mchango wa sekta kwa pato la Taifa.Nusu nyingine inachangiwa na mazao yasiyo ya mbao na huduma mbalimbali.
Pamoja na umuhimu na dhima ya rasilimali ya misitu kwa uchumi wa Taifa, yapo matatizo kadhaa yanayokabili maendeleo ya sekta hii na hivyo kusababisha mchango wake kuwa mdogo zaidi. Matatizo hayo ni pamoja na ukataji miti ovyo, huduma duni ya ugani, viwanda vya mazao ya mbao visivyo na ufanisi na miundo mbinu duni. Nyingine ni sheria zilizopitwa na wakati, uongozi dhaifu katika ngazi zote toka makao makuu hadi vijijini, kutokuwepo ushirikishwaji wa washika dau katika kusimamia rasilimali hiyo, ukosefu wa vituo vya takwimu na kutokuweko mipango ya kutumia rasilimali ya misitu kwa ufanisi.
Kulingana na utaratibu wa Ukaguzi wa Mahesabu Tanzania, ufanisi wa sekta hupimwa kifedha kutokana na bidhaa na huduma zitolewazo. Kwa hiyo uzalishaji na mauzo ya bidhaa za misitu ndani na nje ya nchi unahusika. Kwa mwaka 1999 jumla ya mita za ujazo 26,269.79 zilivunwa. Huduma nyingine zitokanazo na sekta hiyo ni malisho kwa mifugo, malighafi kwa viwanda, uhifadhi wa maji, vyanzo vya maji ya umwagiliaji, uzalishaji umeme, ulinzi wa mazingira, kudhibiti mmomonyoko na virutubisho vya ardhi. Vyote hivi hupatikana kutokana na rasilimali ya misitu.
Ufanisi wa sekta umegubikwa na matumizi madogo japo rasilimali iliyopo ni kubwa. Vile vile rasilimali hii ina uwezo mkubwa wa kutoa bidhaa zisizo za mbao, huduma mbalimbali kama utalii, wanyama, na mazao ya nyuki; na vyote hivi havijaendelezwa. Matumizi na usimamizi wa rasilimali hii unahitaji usimamizi wa misitu wenye kuzingatia wingi wa matumizi yote, usindikaji wa ndani na uboreshaji masoko.
Upandaji Miti
Kwa miaka michache iliyopita, ufanisi wa sekta ya misitu katika kupanda na kuvuna miti ulikuwa mzuri. Upandaji miti umekuwa unafanyika nchi nzima ili kulinda mazingira, na ulifanyika kwa kuhirikishwa sekta binafsi, jumuiya, mashirika yasiyo ya kiserikali na wananchi kwa jumla. Kwa mfano, mwaka 1999 ilifanyika kampeni ya kupanda miti na miti 100 milioni ilipandwa. Uvunaji mazao ya misitu hufanywa na makampuni makubwa na madogo, na wapasuaji mbao binafsi.
Mwelekeo wa mauzo ya mazao ya misitu nje kwa miaka mitano kutoka 1995 – 2000 upo kwenye jedwali la “Economic Survey” kwenye mtandao
“www.tzonline.org”.
Sera ya Misitu na Sheria Zake
Sera ya Misitu ya 1998 ina lengo la kuongeza uchangiaji wa sekta ya misitu kwa maendeleo endelevu ya Tanzania na uhifadhi na usimamizi wa rasimali asilia kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Malengo Makuu ya Sera
- Uhakika wa ugavi endelevu wa mazao ya misitu na huduma kwa kuwa na eneo la kutosha la misitu chini ya usmamizi madhubuti
- Ongezeko la ajira na fedha za kigeni kutokana na maendeleo endelevu ya viwanda vya mazao ya
misitu.
- Uhakika wa mazingira tulivu kutokana na uhifadhi wa viumbe na mimea, vyanzo vya maji na urutubishaji wa
ardhi.
- Ongezeko la uwezo wa taifa wa kusimamia na kuendeleza sekta ya misitu kwa kushirikiana na washika dau
wote.
Sera ya Misitu inalenga maeneo yatuatayo:
- Usimamizi wa ardhi ya misitu
- Viwanda vya mazao ya misitu
- Mazingira endelevu ya viumbe hai na mimea
- Taasisi na rasilimali ya binadamu
Zana muhimu kwa utekelezaji wa sera ya misitu ni uundaji wa mazingira ya kisheria, ndio kusema sheria ya misitu, na uandaaji wa mpango kamilifu wa Taifa. Mpango huu utahusisha masuala yote ya misitu katika muktadha wa maendeleo endelevu.
NB: Maelezo kamili ya Sera angalia “www.tzonline.org”.
Wajibu wa Sekta ya Umma na Binafsi
Sera mpya ya misitu imeweka mazingira mazuri zaidi kwa ushiriki mpana wa washika dau wote katika masuala ya misitu. Washika dau wakubwa ni Idara ya Misitu, Serikali za Mitaa, sekta binafsi, vyama visivyokuwa vya kiserikali na jamii ya wahisani.
Mazingira mazuri, pamoja na taratibu zenye kuwezesha sekta binafsi zitaanzishwa kwa kuwa na ugavi wa uhakika wa malighafi, mafunzo, utafiti na upatikanaji teknolojia. Vituo na mikopo kwa ajili ya uwekezaji vitadumishwa, na uwekezaji wa ubia utashawishiwa. Dhima ya sekta ya umma italenga kwenye kuendeleza sera, kuweka taratibu, tathmini na huduma. Ugawaji madaraka katika usimamizi wa rasilimali ya misitu utaendelezwa. Huduma za kitaalam pamoja na usambazaji wa habari utaimarishwa. Jumuia zitahamasishwa kushiriki kwenye shughuli za misitu. Umilikaji wa ardhi ya misitu utaainishwa.
Maeneo yenye fursa ya kuwekeza ni pamoja na:-
- Sekta binafsi kushirikishwa uvunaji, usindikaji na utafutaji wa masoko kwa bidhaa za misitu, na utoaji wa mikopo.
- Utoaji mafunzo na teknolojia.
- Huduma za ugavi na kuwezesha watu binafsi na jamii kuendeleza na kusimamia misitu.
- Urekebishaji wa sekta ya misitu.
Wajibu na majukumu ya washika dau wakuu katika kutekeleza sera ya misitu yameainishwa kulingana na mbadiliko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ya Tanzania; umuhimu wa misitu katika kulinda mazingira, bidhaa za misitu, kupanua kilimo, mifugo na watumiaji wengine. Pamoja na hayo kuna uridhiaji wa mikataba ya kimataifa kama ya kukabili ukame ili jangwa lisitokee, na mabadiliko mengine yanayohitajika katika sekta. Ili kufanikisha hili mikakati ya kushirikisha jamii katika mipango ya misitu na kuongeza uwezo wa washika dau wote walio na jukumu la kuhifadhi, kusimamia na utoaji wa bidhaa za misitu na huduma, itaendelezwa.
Vyama vya Kitaalamu
Chama cha Wanamisitu Tanzania (The Tanzania Association of Foresters)
Chama kilizinduliwa 1979. Wanachama ni wataalamu wote wa fani zinazohusiana na misitu.
Malengo makuu ni:-
- ¨ Kuendeleza maslahi ya umma katika misitu
- ¨ Kuwa mahali pa kusemea kwa walio kwenye tasnia ya misitu
- ¨ Kuendeleza na kukuza taaluma ya misitu na fani zake
- ¨ Kutoa habari za misitu kwa taifa na taasisi zinazohusika
- ¨ Kushirikiana na asasi nyininge kwa maslahi ya pamoja.
Wajibu wa vyama hivyo ni kuunga mkono juhudi za kuhifadhi mazingira kupitia usimamizi wa rasilimali asilia wa jumuiya, na kushiriki shughuli za uhifadhi kwa kushirikiana na watu binafsi, Serikali, jumuiya, taasisi na vyama visivyo vya kiserikali.
Anwani:
Afisa Mtendaji TAF
Chama cha Wanamisitu
S.L.P. 1975
MOSHI
Rais:
1.Y. Lunangwone,
S.L.P. 426,
DSM
Simu: 281657/2172122
E-Mail-misitu@twiga.com; au sapu@afsat.com
Washika Dau Wengine
Taasisi ya Utafiti Misitu Tanzania (TAFORI) inatafiti kugundua na kusambaza elimu ya kisayansi kwa washika dau ambayo itachangia usimamizi endelevu na kuendeleza rasilimali ya misitu nchini.
Anwani:
S.L.P. 1854
Morogoro
TANZANIA
Simu: 255-023-2263725
UNIDP-LEF East Afrikan Gross Border Biodiversity Project
47 Old Moshi Road
Anwani:
S.L.P. 1041
Arusha
TANZANIA
Simu: 255-27-508398
255-27-508791
E-Mail-biodiversity@cybsnet.com
Mpango wa Taifa wa Mbegu za Miti (NTSP)
Mpango huu uko chini ya Idara ya Misitu na unahusika na kukusanya mbegu za miti za hali ya juu kwa matumizi ndani ya nchi na kwa kuuza nje.
Anwani:
S.L.P. 373
Morogoro
TANZANIA
Simu: 255-023-2563192
Fax: 255-023-2563275
Taasisi ya Misitu Olmotony
Taasisi inatoa mafunzo ya diploma na cheti katika misitu na ufugaji nyuki Pamoja na taasisi hii, kuna vituo vya kufundishia wafanyakazi wa misitu huko Iringa na Rongai, Moshi.
Anwani:
S.L.P. 943
Arusha
TANZANIA
Simu: 255-027-50441
Chuo Kikuu cha Kilimo, Sokoine
Chuo kinatoa mafunzo ya shahada ya misitu.
Anwani:
Kitivo cha Misitu
Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine
Morogoro
TANZANIA
Simu: 255-023-263511
E-mail: Forestry@hhettan.gn.apc.ogr
Forestry@costach.gn.apc.org
Chama cha kuhifadhi wanyamapori Tanzania (W(ST))
Anwani:
S.L.P. 70919
Dar es salaam
TANZANIA
Simu: 255-22-2124572
Mamlaka: Shirika lisilo la kiserikali linaloshugulikia usimamizi wa misitu ya pwani.
Ufugaji Nyuki
Ufugaji nyuki una dhima kubwa katika kuleta maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi, pamoja na kuhifadhi mazingira. Ufugaji nyuki ni chanzo cha chakula, malighafi katika viwanda mbalimbali, dawa, na ni pato la wafugaji nyuki. Mchango wa sekta kwa zao la taifa (GDP) ni asilimia moja. Sekta hii inatoa ajira na kipato kwa baadhi ya wananchi, utalii, na kuleta fedha za kigeni.
Masoko ya asali na nta yana ushindani mkubwa kimataifa. Mwaka 1991 asali ya Tanzania ilishinda kwa asilimia 100 katika ubora wa asali asilia huko Uingereza. Mahitaji ya mazao ya nyuki yamekuwa yakiongezeka kila mwaka.
Makadirio ya uwezo wa sekta ni tani 138,000 za asali na 9,200 za nta kwa mwaka kutoka kwenye makisio ya mizinga 9.2 millioni. Ripoti zinaonyesha kuwa ni tani 4,860 za asali na 324 za nta zinazozalishwa kila mwaka.,kiasi ambacho ni sawa na asilimia 3.5 tu ya mazao ambayo yangeweza kuzalishwa na sekta hii. Wafugaji asilia ndio wazalishaji wakuu wa mazao hayo.
Mazao na Uwezo Wake
- Uzalishaji asali na nta
- Kukuza sekta hususan kilimo, misitu na ufugaji nyuki ili kupata bidhaa na huduma kutoka sekta hizo tatu.
- Uanzishaji, usimamizi na umilikaji wa hifadhi ya nyuki na washika dau wote.
- Uanzishaji na usimamizi wa sehemu binafsi za kufugia nyuki.
- Uzalishaji na ugavi wa zana za ufugaji nyuki na masoko
- Uanzishaji na uendelezaji wa viwanda vya mazao ya nyuki.
Sera ya Ufugaji Nyuki na Taratibu za Kisheria
Madhumuni ya Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ni kuongeza mchango wa sekta hii katika maendelo endelevu ya Tanzania, na kuhifadhi na kusimamia rasilimali asilia kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Malengo ya Sera
- Ulindaji endelevu wa nyuki na hifadhi yake chini ya usimamizi madhubuti
- Mazao bora na mengi ya nyuki kwa misingi endelevu.
- Ongezeko la ajira na mapato ya fedha za kigeni.
- Uwiano mzuri wa mazingira na viumbe na mimea.
- Ongezeko la uwezo wa taifa wa kusimamia na kuendeleza sekta ya ufugaji nyuki.
Wajibu wa Sekta ya Umma/ Binafsi
Sekta za umma na binafsi zinashirikiana kusimamia na kuendeleza sekta ya ufugaji nyuki. Kila sekta imepewa dhima na wajibu wake kama ilivyoainishwa katika Sera ya Ufugaji Nyuki ya 1998. Jumuiya, sekta binafsi na vyama vingine visivyo vya kiserikali vinahusika katika kuhifadhi na kusimamia ufugaji nyuki, wakati Serikali itatoa miongozo na taratibu za kutekeleza shughuli za ufugaji nyuki endelevu. Taratibu za haki ya mtumiaji na manufaa mengine kutoka rasimali hiyo zitatayarishwa na Serikali.
Mabadiliko katika Sekta
Shughuli zote za kibiashara za sekta ya ufugaji nyuki zitaandaliwa na sekta binafsi, vyama visivyo vya kiserikali na jumuiya. Wajibu wa Serikali utakuwa kudhibiti, kubuni sera, kuweka taratibu na kutoa ushauri wa kitaalam na kiufundi. Uratibu wa sera za sekta zinasohusiana utaimarishwa.
Wanyamapori
Wanyamapori Tanzania wanauzwa, na hivyo kuwa chanzo kizuri cha mapato ya fedha za kigeni.Aidha ni kivutio kikubwa cha watalii. Matumizi mengine ni uwindaji kwa watalii na wanchi na kilimo. Nyara na ndege-hai huuzwa nje ya nchi kupata fedha za kigeni.
Aidha, sekta inaajiri kwa masharti ya kudumu na wengine kwa masharti ya muda kama waongozaji na wabebaji mizigo katika misafara ya watalii. Jumuiya zinazoishi kando kando ya maeneo yaliyohifadhiwa zinafaidika kwa uwindaji wa kitoweo, na kupata huduma nyingine kutoka makampuni yaliyopo karibu, na taasisi za Serikali zinazohusiana na sekta ya wanyamapori.
Kwa upande mwingine, sekta inakabiliwa na uwindaji haramu hasa wa wanyama walio kwenye hatari ya kutoweka kama tembo; ushindani na watumiaji wengine wa ardhi, umma kutoelewa umuhimu wa wanyamapori, ukosefu wa taarifa na data, ukosefu wa haki kwa watumiaji wa jumuiya za vijijini, na uwezo mdogo wa kifedha na utaalamu.
Rasilimali ya wanyamapori
Tanzania ni tajiri wa aina nyingi za mimea na wanyama, zikiwemo aina zilizotapakaa na nyingine adimu. Anuwai ya viumbehai na usambaaji wake, ina mamalia wa hali ya juu (aina 20 na 4 zilizoenea), palakala (aina 34 na 2 zilizotapakaa), samaki (aina nyingi zikiwa zimetapakaa Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa, na maziwa mengine madogo na mito); mtambaazi/reptila (spichi 290 na 75 zilizotapakaa ) anfibia (aina 40 iliyotapakaa), wanyama wasio na uti wa mgongo aina ipatayo 11,000, ikiwemo nyingi iliyotapakaa nchi nzima. Licha ya hii Tanzania ina aina ya viumbe muhimu ambayo vinatishiwa na kutoweka duniani na ambavyo vimetapakaa Afrika.
Kwa upande wa makazi, mbuga mbalimbali kama vile Serengeti na miinuko ya Umasaini kaskazini mashariki mwa Tanzania, huishi baadhi ya makundi ya wanyamapori wakubwa duniani. Wanyamapori wa Tanzania ni hazina kubwa asilia na ya manufaa kitaifa na kimataifa.
Asilimia 19 ya eneo la Tanzania limetengwa kwa ajili ya wanyamapori katika hifadhi ambako makazi ya binadamu hayaruhusiwi; na asilimia 9 ambako wanyamapori huishi na binadamu.
Sera ya Wanyamapori
Sheria ya Hifadhi ya Wanyamapori ni ya kulinda, kuhifadhi, kuendeleza, na kudhibiti viumbe hai na mimea. Ufugaji kwenye maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wanyamapori hauruhusiwi kwa mujibu wa sheria.
Madhumuni ya Sera na taratibu zilizowekwa ni kuhusisha sehemu kubwa ya jamii katika kuhifadhi wanyamapori na hasa jamii za vijijini na sekta binafsi.
Malengo ya Sera
- ¨ Kuwa na anuwai hai iliyothabiti na ambayo ni mhimili muhimu wa uchumi wa Taifa.
- ¨ Kupanua uwezo wa washika dau katika kutafsiri na kutekeleza sera hiyo.
- ¨ Kuongeza mchango wa sekta katika pato la taifa kutoka asilimia 2 hadi 5.
- ¨ Kuongeza hifadhi ya wanyamapori, matumizi, usimamiaji na maendeleo ya maeneo yaliyotengwa, na mashirikiano ya kimataifa.
- ¨ Kuhamasisha na kuongoza jamii na sekta binafsi kwa kudhibiti na kusimamia rasilimali ya wanyamapori.
Mkakati mkuu katika kutekeleza sera ni kuzuia matumizi haramu ya wanyamapori nchini kote; na kuunda mazingira yatakayowezesha kuweko kwa mipango endelevu itakayonufaisha wananchi katika maeneo husika kwa kubakiza mapato ya kutosha kutoka manunuzi ya wanyamapori kwenye maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya uendeshaji na shughuli za maendeleo, na kushirikiana na nchi jirani katika kuhifadhi ikolojia inayovuka mipaka.
Maendeleo ya Sekta na Ufanisi
Jukumu la msingi la sekta ya wanyamapori ni kuwezesha matumizi endelevu ya rasilimali ya wanyamapori. Vita dhidi ya uwindaji haramu imezidishwa na matokeo yake ni kupungua kwa vitendo hivyo. Sera imewezesha ufanisi kuongezeka katika lengo zima la kuwa na uhifadhi madhubuti na matumizi endelevu ya rasilimali ya wanyamapori. Jamii zinazoishi kando kando mwa hifadhi wananufaika kutokana na miundombinu ya kijamii na kiuchumi.
NB: kwa mwelekeo wa ufanisi wa sekta rejea Mapitio ya Uchumi (Economic Survey) kwenye mtandao: “Www.tzonline.org”.
Wajibu wa Sekta za Umma na Binafsi
Wanyamapori ni rasilimali asilia ya kibiolojia na kiikolojia, inayojihusisha na mazingira na yenye thamani ya lishe ambayo lazima ihifadhiwe. Sekta binafsi inahamasishwa kuwekeza katika uwindaji na upigaji picha,ufugaji kiranchi wa wanyamapori, kuvuna wanyama, pamoja na kuendeleza miundombinu ya utalii na skimu za vijiji za kutumia na kunadi maliasili ya wanyamapori. Dhima na wajibu wa kutekeleza sera umeainishwa kwa washika dau wote.
Washika Dau Katika Wanyamapori (Taasisi/ Wakala)
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
Ni Shirika linalodhibiti, kuendeleza na kusimamia hifadhi za Serengeti, Tarangire Arusha, Kilimanjao, Ruaha, Manyara, Katavi na Mikumi.
Anwani:
Hifadhi za Taifa
S.L.P. 3134
Arusha
TANZANIA
Simu: +255-27-2508040
Fax: +255-27-2508216
Baruapepe: tanapa@habari.com.tz
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Mamlaka ina eneo la kilomita 8,300 za mraba. Hifadhi hii ina mchanganyiko wa mandhari, wanyama, watu na sehemu za arkeolojia nzuri sana katika Afrika. Imekuwa ya kwanza katika majaribio ya matumizi mengi ya ardhi. Ni mamlaka yenye wajibu wakuendeleza maisha ya pamoja kati ya binadamu na wanyama katika hali ya asili. Inalinda anuwai hai na ikolojia ya Serengeti na miinuko ya Ngorongoro. Inalinda maeneo ya kimatifa ya uvumbuzi wa akiolojia ya binadamu wa kale. Inalinda na kuendeleza yale yanayodhaminiwa na yanayofanya pawe Hifahi ya Dunia na Hifadhi ya Kimataifa ya Bayosifia.
Anwani:
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
S.L.P. 1
Ngorongoro
TANZANIA
Simu: 255-27-2504619
Fax: 255-27-2503339
Baruapepe: neaa-hq@yako.habari.co.tz
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori .
Hii ni taasisi ya utafiti wa wanyamapori na magonjwa yao.
Taasisi inakusanya, kuweka na kusawazisha matokeo ya tafsiri na ushauri wa maendeleo endelevu ya rasilimali ya wanyamapori na kushauri washika dau ipasavyo.
Anwani:
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori
S.L.P. 661
Arusha
TANZANIA
Mfuko wa Kulinda Wanyamapori Tanzania
S.L.P. 1994
DAR ES SALAAM
Simu: 255-22-2866377
255-741-325581
Fax: 255-22-2963496
Baruapepe-kakakuona@intafrica.co.tz.
Chama cha Kuhifadhi Wanyamapori
S.L.P. 70119
DAR ES SALAAM
Simu: 255-22-2112518
255-22-2124572
baruapepe: west@africanonline.co.tz.
Chama cha Wawindaji Tanzania
S.L.P. 33407
DAR ES SALAAM
Simu: 255-22-2116136
Fax: 255-22-2117695
Chama cha Kuuza Nje Wanyamapori
S.L.P. 5784
Dar es salaam
TANZANIA
Chama cha Muungano wa Wasafirishaji
Jengo la AICC, Ngorongoro
S.L.P. 99
Arusha
TANZANIA
Simu: 255-27-504381
Baruapepe: atto.blackmamba@africaonline.co.ke
UTALII
Sekta ya utalii Tanzania ni miongoni mwa sekta zenye uwezo wa kukua sana kiuchumi. Inaleta fedha nyingi za kigeni na kuajiri watu 30,000, na inahamasisha sekta nyingine kama kilimo na hivyo kukuza uchumi. Mchango wake katika Pato la Taifa ni asilimia 14, ambayo ni sehemu ndogo ikilinganishwa na uwezo wa sekta hii.
Tanzania imebahatika vivutio vingi vya utalii. Tanzania inashinda nchi nyingi kwa kuwa na wanyamapori wengi na wa aina nyingi na mandhari za kuvutia, mazingira yasiyoharibiwa, watu wakarimu na sekta za kiuchumi zenye kuweza kuhimili sekta ya utalii, kama sekta ya madini na nyinginezo.
Vivutio vingi asilia na ukubwa wa nchi unatoa nafasi ya kuendeleza shughuli za utalii kama kutazama wanyama, safari na shughuli za ufukweni, upandaji milima, kuona manthari, uwindaji, na upigaji picha.
Lengo letu ni kuendeleza utalii endelevu na bora ambao unaendana na uhifadhi, utunzaji wa mazingira na utamaduni wetu. Kwa kufanya hivyo Tanzania itakuwa inapata faida halisi kutoka kwenye shughuli mbalimbali za utalii.
Tanzania ni mahali pa pekee katika Afrika, ambapo bado hapajagundulika na wengi. Ni nchi yenye maajabu ya mimea na viumbe visivyopatikana kwingine. Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika wenye theluji; visiwa vya maajabu vya Zanzibar; hifadhi za wanyama za Seregeti; ziwa Tanganyika; ziwa Manyara; kileta ya Ngorongoro; magofu ya karne ya 14 na 16 ya Kilwa Kisiwani; goji la Olduvai; nyayo za Laitoti; hifadhi za Baharini Kisiwa cha Mafia ni machache tu ya sehemu za kuvutia utalii. Mandhari na topografia ya nchi na watu wake wakarimu, wana uwezo mkubwa wa kukuza utalii na utamaduni, likizo za ufukweni, uwindaji, shughuli za akiolojia, na upigaji picha mzuri kulilo wote barani. Kwa habari zaidi ya vivutio vya utalii, tazama www.tanzania-web-com/home2.Htm
Sera ya Utalii
Sera ya Utalii ya Septemba 1999 ina malengo yafuatayo:
- Kuongeza uchumi na kuleta hali nzuri kwa wananchi kwa kupunguza umaskini, kwa kuendeleza utalii ulio endelevu na wa hali ya juu kiutamaduni, unaokubalika na watu, unaokubalika kiikolojia, wenye kuzingatia mazingira mazuri na unaolipa kiuchumi.
- Kutangaza Tanzania kama kituo muhimu cha utalii na nchi yenye utajiri wa utamaduni na fukwe nyingi.
- Kuongeza mchango wa sekta kutoka asilimia 16 hadi 25 na 30 ifikapo mwaka 2010.
- Kuweka msingi wa rasilimali ya utalii kwa kiwango cha kutosha kama sehemu ya rasilimali ya umma.
- Kuboresha miundombinu ya utalii na kuiendeleza zaidi ili kupata pato kubwa kutoka kwenye sekta.
Mkakati wa kutekeleza Sera ni pamoja:
- ¨ Kuboresha miundombinu kama vile barabara, usafiri wa anga nk.
- ¨ Kuongeza huduma zaidi kama hoteli na migahawa.
- ¨ Kuongeza ubora na ufanisi katika kutoa huduma
- ¨ Kuchukua hatua za kuitangaza bayana tasnia na kuweka mipango ya masoko ya ndani na kimataifa.
- ¨ Kuboresha maeneo ya utalii kwa kutunza uasilia wa mahali.
- ¨ Kuimarisha taasisi mbalimbali zinazohusika na utalii na kuongeza uratibu wa huduma mbalimbali za kitalii
- ¨ Kuchochea uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi wa miundombinu na huduma za utalii
- ¨ Kuendeleza uwezo wa wafanyakazi kulingana na mahitaji ya utalii.
- ¨ Serikali itahusika katika kuweka miundombinu ya msingi na mazingira yanayofaa kwa washika dau wakati sekta binafsi itaachiwa kuendeleza sekta ya utalii.
Tanzania iko kwenye mazingira ya ushindani katika utoaji wa bidhaa bora na huduma za utalii, dhidi ya idadi ya vituo vingine vya utalii na uchaguzi mkubwa walio nao watalii. Katika hali hii, sera imeweka wazi haja ya kuwa na sheria na taratibu zinazowezesha mazingira ya ushindani.
Washikadau wa Sekta ya Utalii:
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
Bodi ya Utalii Tanzania inakuza maendeleo ya utalii.
Kazi zake
- ¨ Kutangaza utalii ndani na nje ya nchi
- ¨ Kufanya kampeni (matangazo, uhusiano wa umma.maonyesho) kwa lengo la kuvutia utalii.
- ¨ Kutayarisha na kuchapisha vipeperushi na makala za kujitangaza
- ¨ Kutoa habari za kitalii
- ¨ Kutafiti na kuweka kumbukumbu za kisasa za utalii.
Anuani:
S.L.P. 2485
Dar es Salaam
TANZANIA
Simu: 255-22-2110908, 2111244/5, 2136105
Fax: 255-22-2116420
Baruapepe: md@ttb.ud.or.tz. or safari@ud.co.tz.
Website: www.tanzania-web.com/map/home.htn
Taasisi ya Mafunzo ya Hoteli na Utalii
Kazi yake:
Kutoa mafunzo ya uendeshaji hoteli na utalii kiwango cha cheti. Kozi zitolewazo ni vyakula na vinywaji, mapokezi, utoaji chakula na utunzaji wa nyumba.
Anwani:
Taasisi ya Hotel na Utalii
S.L.P. 9181
Dar es salaam
TANZANIA
Simu: 255-22-2112223
Idara ya Mambo ya Kale na Makumbusho
Lengo la idara hii ni kuhifadhi, kulinda, kutafiti na kuendeleza urithi asilia wa utamaduni wa Mtanzania kwa vizazi vya sasa na vijavyo na kukuza burudani na maendeleo ya utalii.
Maeneo ya kihistoria na urithi wa Taifa yabidi yanahifadhiwa kwa vile ni vivutio vya utalii na vituo vya elimu. Maeneo 118 kati ya 400 yameorodheshwa na yanalindwa kisheria.
Kazi zake
- ¨ Kusimamia maeneo ya utamaduni.
- ¨ Kuongeza ushirikiano wa utamaduni na nchi za nje.
- ¨ Kuanzisha vituo vya habari juu ya makumbusho
- ¨ Kufanya utafiti wa usanifu
- ¨ Kutumia maeneo hayo kama rasilimali ya elimu na utalii
- ¨ Kuhusisha jamii katika elimu ya umma na usimamizi wa maeneo.
- ¨ Kutoa manufaa kwa jamii inayozunguka maeneo
- ¨ Kuhakikisha matumizi endelevu ya asili ya urithi huo na jamii
Mawasiliano: baruapepe: mipango.mnrt@twiga.com
Idara ya Mazingira
Idara ya mazingira ina kazi zifuatazo:
- ¨ Kubuni Sera ya mazingira
- ¨ Kuratibu na kufuatilia masuala ya mazingira
- ¨ Kubuni mipango ya mazingira
- ¨ Kufanya utafiti wa kisera wa mazingira
Sera ya Mazingira
Sera ya Taifa ya Mazingira, 1997 ina malengo yafuatayo:
- ¨ Kuhakikisha uendelevu, usalama na matumizi ya rasilimali katika kutimiza mahitaji ya vizazi vya sasa na vijavyo bila kuharibu mazingira au kuhatarisha afya na usalama.
- ¨ Kuzuia na kuthibiti uharibifu wa ardhi, maji, mimea na hewa ambayo inalinda uhai wetu.
- ¨ Kuhifahi urithi asilia ikiwemo anuwai hai ya mfumo wa ikolojia wa Tanzania.
- ¨ Kuboresha tija ya maeneo yaliyoharibiwa, ikiwa ni pamoja na makazi ya mijini na vijijini, ili Watanzania wote waishi maisha salama ya afya na yenye kufurahisha.
- ¨ Kuongeza mwamko na uelewa wa uhusiano uliopo kati ya mazingira na maendeleo, pamoja na kuendeleza ushiriki wa mtu binafsi na jamii katika shughuli za mazingira.
|