HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
MHE. OMAR
RAMADHAN MAPURI (MB) KUMKARIBISHA
RAIS WA
WA JESHI LA POLISI NCHINI KWENYE UKUMBI WA MIKUTANO WA
KIMATAIFA ARUSHA, TAREHE
15 DESEMBA, 2003
·
Mheshimiwa Amani Abeid
Karume, Rais wa
·
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Mohammed Babu
·
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Omari Mahita
·
Makamishna wa Polisi
·
Naibu Makamishna wa Polisi
·
Makamanda wa Polisi
wa Mikoa na Vikosi
·
Viongozi mbali wa
Serikali Mkoani Arusha
·
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Arusha
·
Wakuu wa Madhehebu mbalimbali ya dini
Mkoani Arusha
·
Wageni Waalikwa
·
Mabibi na Mabwana
Mheshimiwa Rais
Kazi yangu asubuhi hii ni kukukaribisha rasmi kutufungulia mkutano wa mwaka
wa Maafisa Wakuu wa Jeshi
la Polisi nchini, unaofanyika hapa mjini Arusha. Lakini kabla sijafanya
hivyo, napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi
kutoa shukrani zetu nyingi za
dhati kwako kwa kukubali kuja
Mkoani Arusha kutufungulia mkutano huu.
Mheshimiwa Rais
Jana tarehe
Mheshimiwa Rais
Hatuna lugha ya kueleza shukrani
zetu nyingi za dhati kwako,
kwani katika hali ya kawaida,
siyo rahisi kuwa na kiongozi mkubwa wa hadhi yako,
kwa siku mbili mfululizo, katika mikoa miwili
tofauti kwa shughuli mbili tofauti, lakini za idara hiyo
hiyo moja. Kwa kweli tunakushukuru
Mheshimiwa Rais
Mambo mengi
kuhusu Jeshi la Polisi, yakiwemo mafanikio na
matatizo umeshaelezwa kwa kirefu na
ufasaha na Inspekta Jenerali wa Polisi. Sitapenda kukuchosha kwa
kurudia kuzungumzia hayo. Hata hivyo, napenda
kuchukua fursa hii kuishukuru Serikali ya Awamu
ya tatu ya
CCM kwa kutekeleza
kikamilifu ilani yake iliyouza kwa
wananchi mwaka 2000 kuhusu vyombo vya
ulinzi na usalama likiwemo Jeshi la Polisi. Serikali ya CCM iliahidi kuimarisha majeshi yetu ya ulinzi
na usalama
kwa kuyapatia mahitaji yake ya
vitendea kazi kwa kadri hali
ya uchumi inavyoruhusu, ili majeshi yetu yaweze
kutekeleza majukumu yake kwa urahisi.
Mheshimiwa Rais
Mheshimiwa Rais
Juhudi hizo za Serikali zinaonekana,
kwani hali ya Jeshi la Polisi
ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita ni tofauti
na ilivyo sasa. Bajeti ya Jeshi
la Polisi imeongezwa kwa asilimia
30 kwa mwaka wa fedha wa
2002/03 na 2003/04.
Pia vitendea kazi mbalimbali vimeboreshwa kwa
kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu,
naamini mazingira ya kazi yataendelea
kuboreshwa mwaka hadi mwaka. Tunaishukuru
Mheshimiwa Rais
Karibu sana Mheshimiwa Rais