HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. OMAR RAMADHAN
MAPURI (MB) WAKATI WA KUFUNGA MKUTANO WA MWAKA WA MAAFISA WAKUU WA JESHI LA
POLISI NCHINI KATIKA UKUMBI WA AICC, ARUSHA TAREHE 17/12/2003
· Inspekta Jenerali wa Polisi
· Makamishna wa Polisi
· Naibu Makamishna
wa Polisi
· Makamanda wa Polisi wa Mikoa
na Vikosi
· Wageni Waalikwa
· Mabibi na Mabwana
Ndugu Mwenyekiti
Ninayo furaha kubwa kujumuika nanyi tena leo katika siku hii ya
kufunga rasmi mkutano mkuu wa
mwaka wa MaafisaWakuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Naamini kwa siku tatu mlizokaa
hapa, mmepata fursa nzuri ya
kupima utendaji kazi wenu kwa
kipindi cha mwaka mmoja uliopita, mmebadilishana uzoefu na mbinu za
utendaji kazi na mmepanga mikakati
mbalimbali ya kukabiliana kikamilifu na changamoto zilizoko
mbele yenu kwa lengo la kuboresha
zaidi utendaji kazi wenu, katika
kuhakikisha ulinzi na usalama wa
watu na mali
zao unadumishwa.
Ndugu Mwenyekiti
Nimepitia ratiba yenu na kuona mada mbalimbali
mlizojifunza na kujadili. Hakika ni
mada nzuri zilizochaguliwa vizuri na zinafaa kwa
wakati tulionao sasa. Kinachotarajiwa kwenu ni kuyazingatia
na kuyafanyia kazi yale yote
mliyojifunza, kwani
Ndugu Mwenyekiti
Nafahamu katika siku tatu mfululizo
mlizokaa hapa, mmepata fursa ya
kujadiliana kikamilifu, kwa kina na
ufasaha mambo yote muhimu yanayolihusu Jeshi la Polisi na utendaji kazi
wake kwa ujumla. Hata hivyo, napenda kugusia machache kwa lengo
la kuzidi kukumbushana na kusisitiza umuhimu
wa mambo hayo.
Ndugu Mwenyekiti
Suala la ushirikiano
na raia
wema ni suala
ambalo linapaswa kupewa umuhimu wa pekee kabisa. Nafurahi kuwa suala hili
lilisisitizwa pia na Mgeni
rasmi Mhe. Amani Abeid Karume, Rais
wa
Ndugu Mwenyekiti
Popote pale duniani,
iwe ni
kwa nchi tajiri au maskini, Jeshi la Polisi haliwezi kufanikiwa bila kuwa na
ushirikiano wa kweli na madhubuti
na raia wema.
Ndugu Mwenyekiti
Siku chache zilizopita, nilikuwa katika ziara ya
kikazi mkoani Mwanza na
katika baadhi ya wilaya za
mkoa huo. Katika mojawapo ya wilaya,
nilimuona mahabusu aliyekamatwa wakati akiuza silaha aina
ya bastola iliyokuwa na
risasi 6 kutokana na taarifa za
raia mwema. Pia nilielezwa tukio la raia mmoja mwema
kugundua silaha aina ya SMG iliyofichwa
na majambazi
shambani kwake na kutoa taarifa
Polisi. Sote tunafahamu matokeo, endapo raia hao wema
wasingetoa taarifa Polisi na
silaha hizo kuangukia mikononi mwa majambazi. Huo ni mfano mmoja
tu katika wilaya moja, naamini
ninyi mnayo mifano mingi zaidi
ya namna raia wema walivyosaidia
kuepusha maafa makubwa kwa nchi
yetu na mtakubaliana
nami kuwa taarifa kutoka kwa raia wema
ni uti wa
mgongo wa ufanisi wa kazi
za Polisi . Hivyo, mtakaporudi katika vituo vyenu vya
kazi, mkalipe umuhimu wa
pekee suala hili na mkalisisitize
pia katika mabaraza yenu.
Ndugu Mwenyekiti
Kwa upande mwingine wa
shilingi, raia wema wamekuwa mstari
wa mbele kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa mbalimbali
za uhalifu. Hata hivyo, wamekuwa wakikatishwa tamaa na baadhi
ya askari wachache wasiokuwa waaminifu ambao huvujisha siri za watoa taarifa. Kitendo hicho siyo tu
ni cha hatari
kwa raia wema, bali ni
cha hatari pia kwa Jeshi la Polisi,
kwani bila taarifa za uhalifu
Jeshi haliwezi kufanya chochote. Aidha, kwa upande
wa raia wema,
mbali ya askari hao wasio
waaminifu kujenga uhasama miongoni mwao, lakini pia
wanasabisha baadhi ya raia wema
kuumizwa, kujeruhiwa vibaya na hata
wengine kuuawa kutokana na waliowataja
kulipiza kisasi. Ni wazi kuwa hatutakubali baadhi ya askari
watuharibie sifa yetu njema. Hivyo, askari yeyote wa cheo chochote
atakayebainika kuvujisha siri za watoa
taarifa, hatua kali za kisheria zichukuliwe
dhidi yake, ikiwa ni pamoja
na kufukuzwa kazi kwa fedheha.
Ndugu Mwenyekiti
Ndugu Mwenyekiti
Kutokana na ongezeko hilo la abiria na pilika
pilika za mwisho wa mwaka,
baadhi ya madereva wa magari
ya abiria huenda kwa mwendo
wa kasi ili
waende safari nyingi zaidi na hivyo
kupata faida kubwa. Hali hii huonekana
zaidi kwa mabasi yanayokwenda mikoa jirani, mfano
Dar es Salaam – Morogoro,
Kilimanjaro – Arusha, na mabasi
madogo yanayotoka mikoani kwenda wilaya za jirani. Ni vyema makamanda wote wa mikoa
mhakikishe kuwa askari wa usalama
barabarani wanasimamiwa kikamilifu ili kuhakikisha ajali zinazosababishwa na uzembe na mwendo
kasi zinapungua. Mtakapowasimamia kikamilifu askari wa usalama
barabarani, mtasaidia kuokoa maisha ya
abiria wasio na hatia ambao
wamekuwa wakipoteza maisha
Ndugu Mwenyekiti
Ndugu Mwenyekiti,
ndugu Makamanda, Mabibi na
Mabwana, baada ya kusema hayo,
ninayo furaha kutamka kwamba, mkutano wenu wa
mwaka wa Maafisa Wakuu wa
Jeshi la Polisi nchini umefungwa rasmi.
Asanteni