HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI
MHE. OMAR
RAMADHAN MAPURI (MB) KWENYE SHEREHE YA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA
13 FEBRUARI, 2004
Kamishna Mkuu wa Magereza,
Makamishna wa Magereza
Maafisa Waandamizi
wa Magereza
Mkuu wa Chuo,
Wahitimu wa Mafunzo
Wageni Waalikwa
Mabibi na Mabwana
Awali ya yote napenda kuchukua
fursa hii kutoa shukrani zangu nyingi za
dhati kwa
Uongozi wa Jeshi la Magereza nchini kwa kunipa
fursa hii ya kuwa Mgeni
Rasmi katika kufunga mafunzo haya ya Uongozi
Daraja la
Kabla ya kutekeleza jukumu lililonileta hapa la kuyafunga rasmi mafunzo haya nataka
nizungumze machache kwa wahitimu.
Hali ya magereza yetu
nchini hivi sasa bado siyo
ya kuridhisha.
Tunayo matatizo mengi ikiwa ni pamoja na uchakavcu wa
majengo ya magereza na nyumba
za askari, uhaba au ukosefu wa vyombo vya
usafiri, upungufu katika huduma ya
wafungwa na askari, upungufu wa vitendea kazi
mbalimbali na kadhalika. Hali hiyo isiyoridhisha
chimbuko
Wakati huo huo, mwelekeo wa
sasa wa kijamii
na kisiasa nchini na duniani
kote umeegemea katika suala zima
la utawala bora, ambapo mambo yanayozingatiwa ni utawala wa
sheria, haki za binadamu na
uendeshaji wa shughuli za kiserikali
kwa uwazi na ukweli. Mwelekeo huu umepelekea watu kutambua zaidi
haki na
wajibu wao na hivyo kuleta
hali ya uwajibikaji
zaidi katika kazi za umma.
Mambo haya mawili niliyoyaeleza ndiyo yanayotukabili hivi sasa na nadhani mtakubalina nami kwamba yameifanya kazi ya uaskari
magereza kuwa ngumu
Nimewakumbusha mambo haya
ambayo tayari mnayafahamu kwa
sababu yana umuhimu mkubwa katika utendaji wenu baada ya
mafunzo haya. Uongozi Daraja la
Ninafahamu kwamba uongozi wa
jeshi hili tayari umekwishaanza kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha
uimarishaji wa utawala bora kwa
kuandaa nyenzo mbalimbali za kuwawezesha
viongozi kutekeleza wajibu wao ipasavyo. Jeshi limechukua hatua ya kuboresha Prisons Standing
Orders ambazo ndiyo mwongozo wa
utendaji wa shughuli za kila
siku jeshini. Hali kadhalika, kila
askari amepatiwa Code of
Conduct for Prisons Officers. Wakati huo huo
wateja wa
aina zote wa jeshi hili
wameandaliwa utaratibu maalum wa kuwaelimisha
kuhusu huduma wanazopaswa kupatiwa na jeshi hili
na namna ya kulalamika pale wanapoona mapungufu. Baadhi ya taratibu hizo
ni vipindi
vya Radio na waaraka maalum unaoitwa Mkataba wa Huduma kwa
Mteja.
Wito wangu kwenu wahitimu wa mafunzo
haya ni kwamba
mzingatie nyenzo zote hizo mlizoandaliwa
ili muweze kutimiza wajibu wenu ipasavyo. Katika hali iliyopo hivi
sasa nchini na duaniani
kote
Baada ya nasaha hizi maalum
kwa wahitimu,
nataka sasa niwapongezeni wote wale walifanikiwa kumaliza vyema mafunzo haya
na kufaulu kustahili kupandishwa cheo kuwa Koplo
wa Magereza. Kwa kuwa cheo kina maana ya kuongezewa
majukumu zaidi, ni matumaini
yangu kwamba kufuzu kwenu ni
ishara ya kwamba sasa mnao
uwezo wa kumudu madaraka zaidi. Nawatakieni utendaji mwema vituoni ili siku zijazo wote muweze
kuteuliwa kuhudhuria mafunzo ya uongozi
Daraja la Pili.
Kwa hayo machache, sasa natamka kwamba
Mafunzo ya Uongozi Daraja la Kwanza Kozi Namba 5 yamefungwa
rasmi.
Asanteni.