HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI
MHE. OMAR RAMADHAN MAPURI (MB) WAKATI WA UZINDUZI WA BODI YA TAIFA YA PAROLE UNAOFANYIKA
HOLIDAY INN,
DAR ES SALAAM TAREHE
Mwenyekiti wa Bodi
ya Taifa ya Parole Mama Julie Manning
Wajumbe wa Bodi ya
Taifa ya Parole
Wageni Waalikwa
Mabibi na Mabwana
Ndugu Mwenyekiti
Awali ya yote
napenda kuwashukuru
Kufanya kazi vizuri
kwa sheria hii ni faraja kwenu na kwangu na Wizara kwa
ujumla wake.
Napenda kuchukua
fursa hii pia, kuwapongeza wajumbe wote wa kuteuliwa wa bodi hii kwa kuteuliwa tena baada ya kumaliza
kipindi chao cha kwanza cha miaka mitano.
Nimeambiwa kwamba hata miongoni mwa wajumbe wanaoingia kwenye bodi hii kwa nyadhifa zao ni mmoja tu aliyebadilika. Nawapongeza
pia wajumbe hao kwa kuendelea kuwepo na pia naomba
nichukue nafasi ya kipekee kumkaribisha mjumbe mpya aliyejiunga nanyi. Matokeo ya msimamo wenu wa
kutetea mlichoamini kuwa ni sahihi – sheria.
Naamini uzoefu wa miaka mingi mlio nao katika
bodi utasaidia kuleta ufanisi zaidi, kwani uzoefu ni suala muhimu katika
kuongeza ufanisi wa jambo lolote. Ninawatakieni
wote utendaji wenye ufanisi na wenye heshima na usio
na majuto ya kuwepo kwa sheria mnayosimamia.
Ndugu Mwenyekiti
Narudi
kwenye historia. Wakati Mheshimiwa
Waziri Mkuu alipokuwa akizundua Bodi za Parole za Taifa na Mikoa kwa mara ya
kwanza hapa nchini mwaka 1998 alielezea kwa kina kuhusu dhana nzima ya Parole
na umuhimu wake katika mfumo wa utekelezaji wa sheria za kupambana na uhalifu
nchini na hivyo kudumisha usalama wa jamii kwa ujumla. Pamoja na kutoa wito
kwa jamii kuielewa na kuikubali dhana ya Parole, Mheshimiwa Waziri Mkuu
alisisitiza kwamba kwa kukubali kuanzishwa kwa mfumo wa Parole nchini, haina
maana kwamba Serikali imeweka rehani
dhamana kuu ya kudumisha usalama wa jamii.
Aliwahakikishia wananchi kwamba parole ni mfumo
uliokwishatumika duniani kwa miaka zaidi ya 300 na kuthibitika kwamba ni sahihi
katika kuimarisha urekebishaji wa wahalifu na hivyo kuimarisha usalama wa
jamii. Sio vinginevyo.
Ndugu Mwenyekiti
Nimelazimika
kukumbusha yale aliyoyasema Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa
sababu kuu mbili.
Katika hali hii,
wito wa Serikali uliotolewa mwaka 1998 kuitaka jamii
ya Watanzania kuielewa na kuikubali dhana ya parole ulikuwa na umuhimu wa
pekee. Napenda nichukue fursa hii
kuwapongeza na kuwashukuru
Ndugu Mwenyekiti
Sababu kuu ya pili
ya kukumbushia wito wa Serikali ni suala zima la
ushiriki wa jamii katika kufanikisha urekebishaji wa wale watakaopata msamaha
wa parole. Nataka nichukue fursa hii
kusisitiza kwamba, sheria ya parole haitaweza kutekelezeka bila ya ushirikiano wa jamii
katika kuwapokea wahusika, kuwakubali, kuwasaidia na pia kufuatilia
mienendo
Ndugu Mwenyekiti
Ninazo taarifa
kwamba kutokana na sheria hii mpya, tofauti na tulikotoka, walipatikana
wafungwa 2,098 wenye sifa za kufikiriwa katika mpango wa parole lakini wengi
wao majina yao hayataweza kufikishwa kwenye kikao hiki cha kwanza kwa sababu mbalimbali. Sababu zilizotajwa ni:-
(i)
Majalada
(ii)
Matokeo ya uchunguzi wa alama za
vidole kuchukua muda mrefu kupatikana kutoka kitengo cha utambulisho (IB).
(iii)
Nakala za hukumu kuchelewa kupatikana kutoka mahakama
husika.
(iv)
Kuchelewa kwa taarifa kutoka kwenye
vijiji wanakotarajia kwenda kuishi kutokana na umbali wa Magereza walipo
wafungwa husika.
Nachukua fursa hii
kuwataka watendaji Wakuu wa Idara zinazohusika na
vipengele hivi muhimu vinavyowawezesha
wafungwa kujadiliwa kwenye Bodi za Parole, kuongeza ushirikiano wa karibu ili
mpango huu uweze kutekelezeka kwa ufanisi zaidi. Ni mategemeo yangu kwamba idadi hiyo kubwa ya
wafungwa wenye sifa itajadiliwa na Bodi hii mapema
iwezekanavyo. Napenda kusisitiza kuwa, ni ushirikiano wa karibu wa vyombo vyote husika tu ndiyo utakaowezesha utekelezaji wa
sheria hii kuwa na ufanisi uliokusudiwa.
Vinginevyo tutakuwa na utaratibu mzuri lakini
ambao utendaji unafanya matunda yake
yachelewe au yasipatikane kabisa. Uamuzi
wa Parole wakati mfungwa ameshamaliza kifungo ni
jitihada zisizo na matunda.
Ndugu Mwenyekiti
Kabla sijatekeleza
kazi mliyonituma kuifanya hapa asubuhi
ya leo, naomba nichukue fursa hii kuzungumza japo
kwa muhtasari kuhusu suala zima la adhabu mbadala wa kifungo hapa nchini. Nataka kukumbusha kwamba wakati tunaanzisha
Parole hapa nchini tulijadili matatizo yaliyoukumba mfumo wa
Magereza duniani ikiwa ni pamoja na hapa
Ndugu Mwenyekiti
Tangu Maazimio hayo
yapitishwe na Umoja wa Mataifa mwaka 1990
Huu ni utaratibu
mzuri zaidi wa kuwaadhibu wakosaji has wenye makosa madogo madogo, kwani
kufungwa gerezani kumekuwa na athari nyingi siyo kwa anayeadhibitiwa tu, bali
hata kwa familia yake na wale wote wanaomtegemea; watu ambao kwa namna fulani
wanaadhibiwa bila kuwa na hatia yoyote.
Kufungwa gerezani kuna athari nyingi,
Napenda kutoa wito kwa wananchi, waupokee kwa dhati mfumo huo wa “Community Service” kwa umuhimu unaostahili
na washirikiane ipasavyo na wale watakaokuwa wanasimamia utekelezaji wake. Mratibu wa mfumo huo
amekwisha kuteuliwa na Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Ndugu Mwenyekiti na Ndugu
Wajumbe
Baada ya kusema
hayo, ninayo furaha kutamka kwamba, Bodi ya Taifa ya Parole kwa mwaka 2003 hadi
2008 imezinduliwa rasmi na pia kikao chake cha kwanza cha Bodi hiyo kimefunguliwa
rasmi.
Asanteni