HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. OMAR RAMADHAN
MAPURI (MB) WAKATI WA KUFUNGA SEMINA YA WADAU WA MPANGO WA HUDUMA KWA JAMII
ILIYOFANYIKA KUNDUCHI BEACH HOTEL, DAR ES SALAAM TAREHE
12 DESEMBA 2003
· Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Taifa ya
Mpango wa Huduma
kwa Jamii na Mwenyekiti wa
Semina hii Mhe. Jumanne Mangara
· Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Huduma kwa Jamii Mhe. Omar Kwaangw’
· Katibu Mkuu – Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi Bw. Bakari Mahiza
· Wawakilishi kutoka nchi za
· Wajumbe wa Kamati ya Taifa
ya Mpango wa Huduma kwa
Jamii
· Wageni Waalikwa
· Mabibi na Mabwana
Ndugu Mwenyekiti
Ninayo furaha kujumuika nanyi tena leo
katika siku hii ya kufunga
Semina ya Wadau wa Mpango
wa Huduma kwa Jamii.
Ndugu Mwenyekiti
Ni imani yangu kuwa, kutokana
na mada
mbalimbali zilizowasilishwa,
wadau wote mmepata elimu kubwa
na ya kutosha
kuhusu mpango mzima wa huduma
kwa jamii na umuhimu wake kwa nchi yetu. Aidha, mmepata uzoefu, ikiwa ni
pamoja na kufahamu mafanikio na matatizo ya
mpango huu kutoka kwa wenzetu
wa nchi za
jirani zilizoanzisha mpango huu kitambo
sasa ambao mlikuwa nao katika
semina hii. Hivyo, nchi yetu ina bahati kuwa, inatarajiwa kuanza mfumo huu
kwa ufanisi kutokana na kurekebisha
makosa mbalimbali ambayo wenzetu walianza nayo.
Ndugu Mwenyekiti
Kama mjuavyo, lengo la semina hii ni
kuwakutanisha wadau wote muhimu
katika utekelezaji wa Sheria ya
Mpango wa Huduma kwa Jamii
ili kuwaelimisha juu ya wajibu
na majukumu ya kila mmoja
katika mfumo mzima wa huduma
hii. Naamini lengo
Ndugu Mwenyekiti
Kwa ruhusa yako naomba ninukuu
kwa lengo
la kusisitiza maneno aliyosema Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokuwa
akifungua semina hii jana. Mheshimiwa Waziri Mkuu alisisitiza
umuhimu wa
elimu kwa jamii ili jamii
iuelewe vizuri mpango huu na
kutoa ushirikianao unaotakiwa. Katika hotuba yake
alisema, nanukuu; “Ni wajibu wetu sote kuwaelimisha
wananchi ili waone umuhimu wa
wahalifu wa makosa madogo madogo
kama vile ugomvi mdogo mdogo, wazururaji,
wanaotoa matusi, n.k kutumikia vifungo
vyao nje ya Magereza kwa
kufanya kazi kwenye jamii, ili
Magereza machache tuliyonayo yabaki kwa ajili ya
wahalifu sugu wenye makosa makubwa
kama vile mauaji, ujambazi, ubakaji, usambazaji na utumiaji
wa dawa za
kulevya na makosa mengine yanayohatarisha usalama na maisha ya
jamii”. Mwisho wa
kunukuu. Hivyo, ni
imani yangu kuwa kazi hii
ya kuelimisha jamii kutokana na ujuzi mlioupata
hapa mtaifanya kwa uaminifu na
ukamilifu.
Ndugu Mwenyekiti
Matarajio ya Serikali kwenu kuhusu utekelezaji wa mpango
huu kwa ufanisi
ni makubwa. Nafurahi kuwa wadau wote
muhimu katika utekelezaji wa
mpango huu wameshirikishwa kikamilifu. Michango mliyotoa wakati wa kujadili
mada mbalimbali zilizotolewa itasaidia kupata mikakati na mbinu madhubuti
za kukabiliana na changamoto zote
zitakazojitokeza.
Serikali haitarajii mpango huu kuwa
wa majaribio kwa kipindi kirefu katika mikoa sita tu
iliyochaguliwa (yaani,
Ndugu Mwenyekiti
Nina ujasiri
wa kusema hayo kwa sababu
faida za mpango huu wa
Huduma kwa Jamii kwa wananchi na kwa
Serikali ziko wazi. Wananchi watafaidika kwa wahalifu
kufanya kazi za kutengeneza barabara, kujenga shule na zahanati,
kusafisha na kutunza mazingira, n.k. Kwa upande wa vijijini, wananchi watapata msaada wa wahalifu
katika kufanya kazi za maendeleo
ya kijiji, hali ambayo siyo
tu itatoa nafuu kwa wanakijiji
bali pia itaharakisha kazi hizo. Kwa upande wake Halmashauri za Miji na Wilaya, fedha ambazo
zingetumika kulipa vibarua wa kutengeneza
barabara, kujenga shule na zahanati,
kusafisha na kutunza mazingira, sasa zitatumika katika shughuli nyingine za maendeleo. Na kwa
upande wa Serikali Kuu, itapata
unafuu wa gharama za kumhudumia
na kumlisha mfungwa na unafuu
wa gharama za kuendesha Magereza. Aidha, kwa upande
wa mhalifu mwenyewe, atapata faida ya kuendelea
kuishi na familia yake uraiani
na hivyo kuepukana na adha
mbalimbali za jela, ikiwemo uwezekano
wa kuambukizwa magonjwa mbalimbali
Ndugu Mwenyekiti
Naamini mlikuwa na muda mzuri
wa kujadiliana kwa kina na ufasaha
mada mbalimbali zilizowasilishwa mbele yenu na mmetumia
vizuri na kwa ukamilifu muda
huo mliokaa hapa kujadiliana
mambo hayo, na mna hamu kubwa
ya kwenda kuyafanyia kazi yote mliyojifunza. Hivyo, sipendi kuwachosha kwa hotuba
ndefu.
Ndugu Mwenyekiti,
ndugu wana semina, mabibi na mabwana,
baada ya kusema hayo, ninayo
furaha kutamka kwamba semina yenu
ya wadau wa mpango wa
huduma kwa jamii imefungwa rasmi.
Asanteni