| .
Uanachama
katika jumuiya za uchumi za mikoa na kimataifa.
§
SADC
§
EAC
§
UNDP
MIKATABA YA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA NCHI
NYINGINE.
USHIRIKIANO
NA WABIA WAKUBWA KATIKA MAENDELEO
Ubelijiji,
Canada, China, Denmark, Finland, Ujerumani, Ireland, Japani,
Uholanzi, Norway, Sweden, Uingereza, Umoja wa Nchi za Ulaya.
Balozi
za Tanzania Nje
Balozi
Ndogo za Tanzania Nje
Balozi
zilizopo Tanzania
Mashirika
ya Kimataifa
Tanzania
ni mwanchama wa jumuiya za kimataifa na kimaeneo, ndiyo kusema
Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi Kusini
mwa Afrika(SADC). Jumuiya
ya Afrika Mashariki ina nchi wabia tatu:
Uganda, Kenya, na Tanzania.
Jumuiya
ya Afrika Mashariki ilianzishwa chini ya mkataba uliotiwa saini na
nchi wabia Novemba 30, 1999.
kwa kuanzia, Jumuiya itaunda umoja wa forodha na soko la
pamoja ambazo mikataba yake inatarajiwa kukamilishwa kutiwa saini
katika kipindi cha miaka minne kuanzia Novemba 1999.
Hatua nyingine za ufungamanisho ni kuundwa kwa umoja wa
mambo ya fedha na hatimaye uundaji wa shirikisho.
Jumuiya ya Afrika Mashariki inanuia kuimarisha utengamano
wa uchumi wa nchi hizi kwa kutoa vipaumbele, na kwa misingi ya
vitendo, ikiwemo kufanikisha biashara kwa kulinganisha ushuru,
malipo, usafiri, matembezi ya watu mipakani, na kusawazisha nyanja
nyingtine zenye maslahi ya pamoja, kama vile siasa, jamii na
utamaduni. Uanachama wa Tanzania SADC ulianzia pale ilipoanzishwa
jumuiya hiyo mapema miaka ya 80.
Jumuiya ya SADC ni ya nchi 13 ambazo ni Angola, Botswana,
Lesotho, Malawi, Muaritius, Msumbiji, Namibia, Afrikaya Kusini,
Swaziland, Tanzania, Zambia, Zimbabwe na Jamhuri ya Demokrasia ya
Kongo.
Wanachama
wa SADC walitia saini hati za awali za mkataba wa biashara Januari
25, 2000, wenye lengo
la kuanzisha eneo huru kwa kuondoa
vikwazo vya biashara na huduma, kuweka sheria
zifaazo za biashara (kukataza kuuza kwa bei nafuu katika
nchi nyingine bidhaa zisizotakiwa soko la nyumbani, ruzuku,
kufidia ushuru na ulindaji wa biashara).
Eneo huru la biashara la SADC linatarajiwa kuwa
litaanzishwa katika kipindi cha miaka nane kuanzia Septemba, 2000.
Tanzania pia imejifunga katika mipango mingine ya
kimataifa, kama ile ya Shirika la Biashara Duniani(WTO), Afrika,
Caribean-Pasifiki (ACP) na Umoja wa Ulaya (EU)
UANACHAMA
NA NCHI JIRANI NA ZA KIMATAIFA KATIKA MAKUNDI YA KIUCHUMI
JUMUIYA YA MAENDELEO YA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA
(SADC)
Madhumuni:
Kukuza
maendeleo ya uchumi unaojitegemea na muungano katika nchi za SADC
pamoja na kuendeleza amani na usalama katika nchi hizo.
Mipango mikuu inayoendelea
Utekelezaji
wa SADC programme of Action unajumuisha yafuatayo:-
¨
Mpango wa SADC wa Takwimu.
¨
Mpango wa SADC wa kudhibiti
madawa.
¨
Mpango wa SADC wa jinsia
¨
Mpango wa SADC wa kufikia kilele
cha uchumi (SADC Economic Summit Programme).
¨
Itifaki kuhusu Ruksa na Upendeleo
(Immunities and privileges).
¨
Itifaki kuhusu mifumo ya mgao wa
mwenendo wa maji (shared water course systems).
¨
Itifaki kuhusu Nishati
¨
Itifaki kuhusu usafirishaji
mawasiliano na Hali
ya Hewa.
¨
Itifaki kuhusu Biashara
¨
Itifaki kuhusu kupambana na
Biashara ya Madawa ya kulevya (Combating Illicit and Drug
Trafficking).
¨
Itifaki kuhusu madini.
¨
Itifaki kuhusu Elimu na Mafunzo.
¨
Itifaki kuhusu utalii.
Anwani:
Katibu
wa SADC
Private
Bag 0095
Government
Enclave
Gabarone
BOTWASANA
Website:
www.sadc.com
JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC)
Madhumuni:
Kuimarisha
ushirikiano wa uchumi, jamii, utamaduni, siasa, teknolojia na
ushirikiano mwingine kwa kuleta maendeleo sawa na ya kudumu ya
nchi husika (Tanzania, Kenya, Uganda).
Mipango mikuu inayoendelea:
Kutathimini
Mpango wa Maendeleo ya EAC kwa kipindi cha 1999-2000 na kuridhia
mpango wa maendeleo wa EAC kwa 2001-2005.
Mipango inayoanzishwa na iliyopo inahusu yafuatayo:
¨
Kuanzisha pasi/pasipoti za
kusafiria zilizo sawa kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na
utoaji wa vitambulisho vya kitaifa.
¨
Kuanzisha nyumba ya biashara
(Stock Exchange) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na soko la fedha
(Capital Market).
¨
Kupunguza urasimu katika
kutayarisha hati za wateja (simplification of customers
documentation).
¨
Kupunguza viwango vya kodi
kufuatana na mapendekezo ya “Cross Border Initiative - CBI)”.
¨
Itifaki juu ya kupambana na
Biashara ya Madawa ya kulevya katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
¨
Itifaki juu ya kuwa na viwango
vilivyosawa, bidhaa zilizo mathubuti, Hali ya Hewa na Uchunguzi
(Standardisation, Quality Assurance Meteorology and Testing).
¨
Uchunguzi wa Sheria za taratibu
kwa ajili ya mikutano ya Wakuu wa nchi (Observance of the rules of
procidure for the summit of heads of state).
¨
Uchunguzi wa sheria za taratibu
kuruhusu nchi za nje katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
¨
Uchunguzi wa sheria za taratibu
za kuruhusu
¨
waangalizi/wachunguzi katika
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
¨
Itifaki juu ya kuanzisha muungano
wa ushuru wa forodha kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki iko katika
hatua za mwisho.
Anuani:
Katibu
wa Tume ya EAC
S.L.P.
1096
Arusha
TANZANIA
Website:
http/hometwiga@.com/eac
SHIRIKA LA MAENDELEO LA UMOJA WA MATAIFA (UNDP)
Madhumuni:
Kuimarisha
na kuendeleza maendeleo ya uchumi na ukuaji.
Mipango mikuu inayoendelea:
Utekelezaji
wa mpango wa 6 wa UNDP wa Nchi (6th UNDP Country
Programme) kwa ajili ya Tanzania ambao unajumuisha yafuatayo: -
¨
Mpango wa kupunguza umaskini.
¨
Mpango wa kurekebisha utumishi
serikalini.
¨
Kujenga uwezo kwa ajili ya
kusaidia maendeleo katika ngazi za Serikali Kuu na serikali za
mitaa.
¨
Mpango wa kurekebisha sheria.
¨
Mpango wa Utawala bora.
¨
Mpango wa UKIMWI.
¨
Mpango wa kurekebisha Serikali za
Mitaa.
¨
Mpango wa TCDC.
MAKUBALIANO
YA NCHI MBILI YA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA NCHI NYINGINE:
Tanzania
imeshaweka saini mkataba wa uwekezaji na Uingereza na kuweka saini
mikataba inayofanana na huo ambayo iko katika hatua ya
kuthibitishwa na Serikali za nchi ya Sweden, Denmark, Uholanzi na
Jamhuri ya Korea.
Hatua
za mwisho zimefikiwa za Uwekezaji kati ya Serikali za Finland na
Italy.
Maeneo
yanayohusika na mikataba hiyo ni pamoja na: -
¨
Kukuza na kulinda uwekezaji
¨
Transfer of Principal, returns,
proceeds, payments, compensation and earnings.
¨
Expropriation and Compensation
¨
Kusuluhisha mogogoro.
USHIRIKIANO
WA WASHIRIKI WAKUU KATIKA MAENDELEO:
Tanzania kama nchi nyingine zinazoendelea
inamakubaliano ya ushirikiano na washiriki kadhaa, kwa madhumuni
ya kusaidia maendeleo ya Tanzania
ya kijamii na kiuchumi. Mpango huu unafanikishwa kwa msaada
wa fedha, ufundi na misaada ya vifaa (ruzuku na mikopo kwa
Tanzania). Washiriki wakuu wa kusaidia kuleta maendeleo ni
wafuatao: -
BELGIUM:
Ushirikiano wa Maendeleo ya Belgium
Tanzania unaendeshwa kupitia serikali na kupitia mfumo usiokuwa wa
serikali. Makubaliano rasmi wa ushirikiano wa Maendeleo baina ya
nchi hizo mbili uliwekwa saini mwaka 1984. Maeneo
yanayoshughulikiwa sasa ni yafuatayo: -
i.
Usafirishaji na Mawasiliano.
¨
Contral Railways Corridor Programme involving weigh
bridges, mobile container crane and 12 petrol tanks.
¨
Mafunzo kwa ajili
madereva wa magari moshi.
¨
Karakana ya matengenezo.
¨
Provision turnout’s/switches and truck fittings.
¨
Kutoa vifaa na mafunzo kwa ajili ya matengenezo na
vyombo vya kuzolea uchafu chini ya maji bandarini (provision of
equipment and training for maintenance and dredging in the
harbour).
¨
Kuazimisha wataalam wa Kibelgji wa kompyuta.
¨
To assist in the computerisation of the principal
and voyage account.
ii.
Maendeleo ya Sekta ya Vijijini.
-
Kuendeleza Mkoa wa Kagera
-
Kuendeleza zao la ndizi na uzalishaji wa mazao ya biashara.
-
Uchimbaji wa malambo.
-
Afya.
-
Vituo vya upimaji.
iii.
Kupunguza umaskini
Mpango huu
unatekelezwa na UNDP kupitia juhudi za “National Income
Generation Programme”.
iv.
Kuendeleza Sekta Binafsi.
-
Uchunguzi wa kutambua maeneo ya kuendeleza sekta binafsi
umekamilika na inaelekea kwamba shirika la “Tanzania Venture
Capital Funds’ huenda likapendekezwa kushughulikia.
v.
Mfuko wa kuishi – Ngara (survival fund)
-
Kusaidia upatikanaji wa kuni na ustawishaji wa misitu chini
cha usimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia
wakimbizi na kutekelezwa na CARE.
CANADA:
Utangulizi:
Ushirikiano wa
Tanzania Canada Maendeleo ulianza 1965.
Msaada wa Canada kwa Tanzania unatolewa kupitia wakala ya
Msaada wa Maendeleo (Development Aid Agency) inayojulikana kama
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Canada (Canadian
International Development Agency – CIDA).
Msaada unalenga katika mahitaji ya binadamu maendeleo ya
wanawake, sekta binafsi, utawala na haki za binadamu.
Miradi
inayoendelea
Sekta
Mradi
Miundo mbinu na usafirishaji -
Vifaa vya kutengenezea magari
Moshi ya Shirika
la Reli la Tanzania
(TRC)
Msaada na mafunzo kwa ajili ya
TRC
Kituo cha mawasiliano cha Kagera
Kupiga picha za anga Hanang
Elimu -
Mfuko wa mafunzo kwa ajili ya
wanawake.
Community based for girls?
Basic Education Specialist/
Maendeleo
vijijini
-
Mfuko wa Hanang wa maendeleo ya
ushirikishwaji
Mradi wa vifaa na Afya ya mtoto
Mfuko kwa ajili ya maendeleo ya
viwanda vya mazingira.
Utawala
-
Mradi wa Maendeleo ya Demokrasia
Tanzania.
Maendeleo
ya biashara
ndogondogo
-
Mennonite Economic Development
Associates (MEDIA).
Mfuko wa Canada kwa ajili ya
kusaidia juhudi za binafsi kwenye
makazi.
Mfuko wa Tanzania wa kurekebisha
majengo.
Miradi
mingineyo
-
Kamusi za kiingereza – Kiswahili
Mifuko
ya Ushirikiano wa Tanzania Canada.
Tanzania program support unit
Uchunguzi wa gesi ya songosongo.
Food monitization
Kuendeleza
mipango na usimamizi wa sekta ya afya
Miradi
ya Mikoa
-
Decentralized Democratic
Development
Mpango wa mafunzo ya UKIMWI
kusini mwa Afrika (Southern African
AIDS Training program (SALTZ).
CHINA
Utangulizi:
Ushirikiano
baina ya Tanzania na China ulianza tangu 1964 kwa mapatano ya
kutoa mikopo yenye masharti laini ya biashara.
Ushirikiano uliopo sasa unalenga kwenye kilimo, viwanda,
usafirishaji na mawasiliano, ujenzi, madini, biashara, afya na
elimu.
Miradi
inayoendelea
- Mradi wa makaa ya mawe wa Kiwira:
Mradi
unaendeshwa kwa pamoja ambapo China inamiliki hisa asilimia 62 na
Tanzania asilimia 38.
Mradi
wa nguo unaoendeshwa kwa pamoja
Miradi
inayobuniwa
- Shamba la mpunga la Mbarali:
Kampuni ya Kichina ya Jiangsu Agricultural and Forest
Department imeonyesha nia ya kuingia ubia na serikali ya
Tanzania.
- Shamba la mpunga la Ruvu:
Jitihada zinafanyika kuipata kampuni ya kuingia naye
ubia
- Kiwanda cha zana za kilimo cha
Ubungo (UFI): Kampuni
ya Kichina iitwayo Tianjin Machinery Import Export Cooperation
imeonyesha nia ya kuingia ubia.
- Kiwanda cha kutengeneza mashine
cha Mang’ula: Mipango inafanywa ya kumpata mmbia wa
kuwekeza.
DENMARK
Ushirikiano
wa maendeleo wa Tanzania – Denmark ulianza katika miaka ya
mwanzo ya 1960 kupitia shirika la Nordic Aid Project. Kuanzia
wakati huo Tanzania imekuwa moja wa washiriki wakuu wa ushirikiano
wa maendeleo na Denmark.
Kutokana na mkataba wa makubaliano uliowekwa saini tarehe 7
Agosti, 1995 mpango wa baadaye wa ushirikiano utaelekezwa katika
kusaidia mipango ya sekta na “sector concentration”.
Licha ya “sector concentration” Denmark inaendelea
kujihusisha na masuala ya kuendeleza haki za binadamu – zikiwemo
haki za wanawake,. Utawala
bora na maendeleo ya demokrasia.
Mpango wa kusaidia sekta ya afya – awamu ya kwanza
- Mipango ya afya ya kushughulikia
masuala ya UKIMWI na magonjwa ya zinaa kwa gharama nafuu
kwenye hospitali za Wilaya, vituo vya afya, dispensari na
katika jumuiya.
- Mfumo wa afya wa usafirishaji wa
kitaifa/kiwilaya.
- Kuimarisha sehemu muhimu katika
Wizara ya Afya.
- Kuendeleza watumishi,mipango na
uwezo wa usimamizi katika Wizara ya Afya.
Mpango
wa kusaidia sekta ya kilimo
- Mpango huu unalenga katika
kuimarisha uwezo wa kuanzisha uzalishaji wa mbegu shambani,
miradi ya wakulima wadogo wadogo ya
umwagiliaji maji, utafiti wa mawe ya phosphate na
hifadhi ya mazingira.
Mpango
wa kusaidia Sekta ya Barabara
(i)
Matengenezo ya barabara ya Dar es Salaam –Mlandizi,
Daraja la Mto Wami na Barabara ya Chalinze – Segera.
(ii)
Usimamizi wa matengenezo ya barabara kuu awamu ya pili.
- Sehemu ya Barabara za Mikoani
Ukarabati
wa kilomita 150-200 wa barabara za mkoa wa Pwani.
- Sehemu ya Barabara za Wilaya
Ukarabati
wa barabara za Wilaya ya Rufiji katika Mkoa wa Pwani.
- Kusaidia Asasi/Taasisi
(institutional support)
-
Elimu ya ufundi na mafunzo
-
Kuimarisha Benki ya ushirika na Maendeleo ya Vijini (CRDB).
-
Kuendeleza hazina Ndogo
-
FEDHA Funds (risk capital for long term investment).
-
Msaada kwa vyama vya wafanyakazi na vyama vya biashara.
Mpango wa kusaidia sekta ya Maliasili na Utalii,
misitu na Nyuki.
- Mradi wa kusaidia uongozi wa
msitu wa Udzungwa katika Mkoa wa Iringa.
- Msaada kwa jumuiya ya Natural
woodland Management Project (Iringa).
- Msaada kwa eneo la Hifadhi la
Ngorongoro.
Mpango
wa kusaidia mazingira
(i)
Kuendeleza Arusha
(ii)
Kusaidia vijiji kusimamia misitu na nyika katika Mkoa wa
Lindi.
(iii)
Kuendeleza Mwanza.
FINLAND
Utangulizi
Ushirikiano
wa Maendeleo wa Tanzania – Finland ulianza katika miaka ya
mwanzo ya 1960 wakati shirika la Nordic Aid Project
lilipoanzishwa. Aina
ya msaada mkuu ulikuwa kusaidia miradi kwa njia ya fedha
mikopo au ufundi.
Miradi inayoendelea
Mazingira na misitu ambayo inajumuisha yafuatayo:-
-
The Tanzania Forest Action Plan (TFAP)
-
The East Usambara Catchment Forest Programme
-
Establishment of Amani Nature Reserve, Catchment Forest,
Farm Forest,kuimarisha na kutafiti pamoja na kusimamia
utekelezaji.
-
Utafiti wa Misitu nchini Tanzania Awamu ya Kwanza:
madhumuni ya keni kuimarisha utafiti na kuendeleza uwezo katika
Taasisi ya utafiti wa Misitu Tanzania (Tanzania Forestry Research
Institute – TAFORI).
-
Mradi wa kuendeleza misitu Zanzibar: madhumuni ni
kushughulikia masuala ya umaskini vijijini na upungufu katika
kusimamia maliasili.
-
Mradi wa Zanzibar Intergrated Lands and Environmental
management (ZILEM). Mradi
unalenga kuendeleza uwezo
katika maeneo yanayoshughulika na mpango wa matumizi ya ardhi,
usimamizi wa ardhi na usimamizi wa mazingira.
- Mradi wa Maji na Maji Taka
-
Mpango wa maendeleo ya maji katika mikoa ya Lindi na
Mtwara.
-
Mradi wa maji mjini Zanzibar.
- Mradi wa Maendeleo Vijijini
-
Rural Integrated Programmes Support (RIPS)katika mikoa ya
Mtwara na Lindi awamu ya III.
-
Mfuko wa Elimu.
-
Mfuko wa kusaidia Elimu ya ufundi.
-
Elimu ya shule ya msingi Wilayani.
-
Mfuko wa shughuli za utamaduni.
-
Urekebishwaji wa Serikali za Mitaa na “redeployment”
-
Msaada kwa kuendeleza demokrasia.
-
Mfuko wa Demokrasia.
-
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) – Integrated Tax
Administration Programme.
-
Msaada kwa kutayarisha mchanganuo wa Sera ya Hazina.
-
Demokrasia, haki za binadamu na usawa.
UJERUMANI
Utangulizi
Mkataba
wa kwanza wa ushirikiano wa maendeleo baina ya Tanzania na
Ujerumani ulitiwa saini 1962, ambao uliisaidia Tanzania kupata
msaada wa kusaidia maendeleo ya uchumi kwa njia ya mikopo na
ruzuku.
Licha
ya ushirikiano wa kiserikali ushirikiano mwingine wa Tanzania na
Ujerumani unajumuisha yafuatayo:
- Huduma za kujitolea kupitia
German Development Services (DED).
- DEG Investment activities (German
Private Investment cooperation).
- Shughuli za Biashara na Viwanda
- Non project tied scholarships.
- Integrated experts through center
of international migration (CIM).
Miradi
inayoendelea
(i)
Ushirikiano na makanisa katika kuhudumia miradi ya jamii.
(ii)
Miradi ya ushirikiano na shirika la Reli la Tanzania
(iii)
Mradi wa umeme wa Kihansi chini wa kusambaza umeme
unaotokana na maji.
(iv)
Kukarabati transfoma na mitambo ya kuwashia na kuzimia
umeme wenye nguvu kubwa.
(v)
Mpango wa kuongeza uwezo wa nishati
(vi)
Marekebisho katika kugharamia barabara.
(vii)
Marekebisho katika kusimamia
mtandao wa barabara.
(viii)
Mradi wa maji vijijini.
(ix)
Mradi wa maji Hai vijijini awamu I na II.
(x)
Mradi wa maji Ngara – Karagwe.
(xi)
Usimamizi wa maliasili.
IRELAND
Utangulizi:
Ushirikiano
wa kwanza wa Tanzania – Ireland ulianza miaka ya 1970 kati ya
Irish Ropes na kiwanda cha Kilosa cha Mazulia (Kilosa Sisal Carpet
Factory). Kuanzia 1981, ushirikiano wa Ireland ulilenga Wilaya ya
Kilosa na Kuanzia 1980 Wilaya ya Ulanga na Kanda ya Pwani ya Tanga
ziliongezwa. Ushirikiano
unaelekezwa kwenye kupunguza umaskini, upatikanaji wa huduma za
msingi, usawa wa jinsia, maliasili na utawala bora.
Miradi
inayoendelea
- Kuendeleza mipango ya maendeleo
katika wilaya za Kilosa, Ulanga,Kilombero na Muheza.
- Kuimarisha mpango wa sekta ya
elimu wa maendeleo.
- Kuendeleza Idara ya Elimu ya
ramani ya bahari na mito (hydrology) ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam .
- Ukarabati wa shule za msingi
katika mkoa wa Kigoma (Katika maeneo yaliyoathiriwa na
wakimbizi).
- Mpango wa kurekebisha sekta ya
afya (kuimarisha rasilimali ya watumishi).
- Mfuko wa sekta ya afya wa
“Basket”
- Kuimarisha usalama wa chakula.
- Mradi wa kupanua Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo Morogoro.
- Mpango wa mafunzo ya utalii.
- Hifadhi ya asilia (Tanga Coastal
Zone Conservation program).
- Mradi wa utafiti na upanuzi wa
kanda ya mashariki.
- Msaada kwa mpango wa urekebishaji
wa serikali za mitaa.
- Mchango wa kusaidia bajeti ya
kupunguza umaskini.
JAPAN
Utangulizi
Ushirikiano
na Japan umeanzia miaka ya 1970.
ushirikiano wa sasa unaendeshwa chini ya utaratibu wa JICA
katika maeneo muhimu yafuatayo:-
§
Miundombinu
-
Mitambo kwa ajili ya matengenezo ya barabara kuu
-
Usambazaji wa umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro
-
Usambazji wa mtandao wa simu
-
Ujenzi wa barabara za jiji la Dar es Salaam
-
Kuimarisha madaraja katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.
§
Afya
-
Kuangamiza ugonjwa wa kupooza (poliomyetis) kwa watoto
walio chini ya miaka mitano.
§
Elimu
-
Msaada kwa elimu ya msingi pamoja na elimu ya sekondari.
§
Maji
-
Kuimarisha huduma za maji na afya katika maeneo
yaliyoathiriwa na wakimbizi.
§
Mahitaji ya msingi
-
Miradi ya kupunguza umaskini katika Wizara zinazohusika na
Kilimo, Maji na Afya.
§
Msaada wa ruzuku kupunguza madeni
-
ulipaji wa madeni ya Tanzania unagharamiwa na Serikali ya
Japan kwa utaratibu wa Tanzania Debt Relief Cover kwa ajili ya
kuingiza bidhaa kupitia njia za kawaida za biashara.
Mpango wa msaada wa chakula (KR I and KR II)
Kuhamisha
mali ili kuweka sawa hali ya ulaji kwa misingi ya upatikanaji wa
chakula katika soko
(KR I) na kutoa pembejeo na zana za kilimo ili kuongeza uzalishaji
wa chakula (KR II). Msaada wa chakula kama vile mchele, unauzwa ili kupata fedha
ambazo zinatumika kusaidia nguvu za serikali katika kugharamia
maendeleo ya miradi katika sekta zinazohudumia kilimo na jamii.
UHOLANZI
Utangulizi
Ushirikiano baina ya Tanzania na Uholanzi ulianza
miaka ya 1970
Miradi
inayoendela
Elimu
Mradi
unajumuisha mfuko wa elimu kusaidia utayarishaji wa mpango wa
kuendeleza Sekta ya Elimu, msaada kwa mradi wa vitabu vya
watoto,mpango wa muda wa vitabu vya kufundishia, kusaidia elimu ya
juu,kitengo cha utafiti wa kiuchumi cha chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Idara ya Uhandisi, Idara ya Utafiti kuhusu kupunguza
umaskini (REPOA), msaada kwa elimu ya msingi kupitia wilayani,
msaada kwa elimu
kupitia mpango wa wilaya wa kuendeleza vijiji hasa kwa kupitia
SNV, na mpango wa masomo (wanafunzi wapatao 80 – 100 huenda
kusomea kozi nchini Uholanzi kila mwaka
Afya
Shughuli
zinazoendelea chini ya mpango wa afya ni pamoja na mpango wa Taifa
wa kifua kikuu na ukoma, mpango wa afya ya uzazi kwa nia ya kuzuia
UKIMWI na utafiti juu ya UKIMWI na mahusiano ya jamii na uuzaji wa
kondomu.
Maji
Miradi
ya maji katika mikoa miwili ya Singida na Morogoro ya uchimbaji wa
visima vifupi, jinsi ya kuvitumia na kuvihudumia.
Serikali
za Mitaa
Kurekebisha,
kuendesha, kushauri na kuanzisha mfumo wa usimamizi wa fedha
(platinum) katika mikoa kumi na moja
Maendeleo
vijijini
Mikoa
kumi na moja inashiriki katika mpango huu, nayo ni Biharamulo,
Bukoba, Kahama, Karagwe, Kondoa, Maswa,Mbulu, Meatu, Monduli,
Songea na Ngara. Mpango huu uko katika awamu ya tatu na una nia ya kuongeza
umilikaji katika mahali na uwajibikaji katika kutumia mifuko ya
maendeleo ya Wilaya na kuongezeka kwa jukumu la kuisaidia serikali
kuu kutoa msaada kwa wilaya.
Mipango mingine inahusu Multilateral Debt Fund, mazingira,
miundombinu na wanawake katika maendeleo.
Miradi/mipango
inayogharamiwa na Uholanzi chini ya ORET
(i)
Barabara ya Kongowe – Mjimwema Kivukoni.
(ii)
Kuimarisha hudumna za viwanja vya ndege (zima moto na
dharura).
(iii)
Kukarabati huduma za
uchunguzi na yakini ya mgonjwa – Wizara ya Afya.
NORWAY
Utangulizi
Ushirikiano
wa maendeleo kati ya Norway na Tanzania ulianza miaka ya mapema ya
1960 katika nyanja ya ushirikiano
wa kiufundi yanayohusu maeneo ya utawala, afya na elimu.
Kutoka 1995, ushirikiano umekuwa unaongozwa na mkataba wa
makubaliano wa maendeleo wenye madhumuni ya kuendeleza uchumi
imara wenye kulenga katika sekta
zifuatazo:
§
Kuimarisha uchumi.
§
Miundombinu.
§
Utafiti na elimu.
§
Marekebisho ya siasa.
§
Mazingira na usimamizi wa
rasilimali
§
Uhusiano wa biashara na
utamaduni.
§
Mipango ya ushirikiano na nchi za
jirani kwa mfano Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC)
§
Co-financing with multilateral
organizations.
§
Msaada kwa vyama visivyo vya
kiserikali (NGO’s) na huduma za kujitolea.
Miradi
inayoendelea
- Kukuza jitihada za vijiji na
maendeleo ya biashara (promotion of Rural Initiatives and
Development Enterprises (PRIDE) katika mikoa ya Arusha, Tanga
na Dar es Salaam.
- Ujenzi wa kituo cha umeme chini
ya ardhi na bwawa la kuzalisha umeme katika kituo cha Kihansi.
- Ujenzi wa kituo kidogo cha umeme
katika maeneo ya Kunduchi na Magomeni jijini Dar es Salaam.
- Kuvuta nyaya za kusambaza umeme
kutoka Mbala (nchini Zambia) hadi Sumbawanga (Mkoani Rukwa).
- Kusaidia Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Maendeleo
ya Uongozi (Mzumbe) na Taasisi ya Dar es Salam ya mafunzo ya
Bahari.
- Mradi wa mbao wa Sao Hill.
- Mradi wa kuhifadhi ardhi na
misitu katika mkoa wa Shinyanga.
- Msaada kwa sekta ya Maliasili.
- Mpango wa UKIMWI Mkoani Arusha na
Kilimanjaro.
- Ukarabati wa barabara kuu
(barabara ya Himo – Holili).
- Matengenezo ya barabara za vijiji
katika mikoa ya Mbeya na Tanga.
- Ujenzi wa daraja la Mgoda (mradi
wa ubia)
- Upanuzi wa Bandari ya Dar es
Salaam (Kurasini Oil Jetty).
- Msaada kwa bajeti ya kusaidia
kupunguza umaskini.
- Mipango ya maendeleo ya vijiji.
SWEDEN
Utangulizi
Ushirikiano
wa Tanzania Sweden ulianza 1963, ukilenga kwenye miradi maalum
iliyopo Mikoani, kusaidia ulipaji wa mikopo, misaada ya dharura,
miradi ya mazingira, vyama visivyokuwa vya kiserikali pamoja na
shughuli za demokrasia na haki za binadamu.
Miradi inayoendelea
Elimu
¨
Kusaidia vifaa vya shule, mafunzo
ya walimu, mradi wa mpango wa vitabu vya shule na mfuko wa
utamaduni wa Tanzania.
Fedha na Utawala
¨
Mpango wa Serikali wa Maendeleo
ya Taarifa za Hesabu (Government Accounting Development Programme
– GADP), mpango wa Idara ya Utumishi wa Jinsia, Mamlaka ya Kodi
Tanzania na Capital Markets Development.
Usafirishaji na Mawasiliano
Kuimarisha
na kuendeleza kampuni ya simu Tanzania (TTCL)
Nishati
Kusaidia
mradi wa kuzalisha umeme wa Kihansi na Kampuni ya Umeme Tanzania
(kuweka magurudumu ya kuzalisha umeme wakati wa dharura
yanayoendeshwa kwa njia ya gesi).
¨
Mazingira
Baraza
la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
¨
Maliasili
EBD
– SAPU
¨
Serikali
za Mitaa
Mpango
wa kusaidia Wilaya, mpango wa kusimamia ardhi – Babati, Kiteto
na Simanjiro, kusaidia mipango ya Wilaya ya Singida na utawanyaji
wa vifaa vya elimu.
¨
Maendeleo
ya Jamii, Wanawake na Watoto
Mradi
wa afya na maji (HESAWA)
Mipango
mingine
Inajumuisha
kushirikiana katika utafiti, masuala ya urari wa malipo, na
kusaidia mipango inayoendeshwa kwa kushirikiana na FAO, WFP,
UNICEF, NGOs za Sweden na SCAPA.
UINGEREZA
Utangulizi
Ushirikiano
wa maendeleo wa Tanzania – Uingereza ulioanza mwaka 1961,
unahusu msaada ya fedha na ushirikiano wa kiufundi.
Ushirikiano wa Uingereza pia unatolewa kupitia Umoja wa
Ulaya (EU), mfuko wa Maendeleo wa Ulaya, msaada wa Dharura, NGOs
na msaada wa chakula.
Miradi
inayoendelea
¨
Maliasili
Kusimamia
mradi wa wanyamapori wa Ruaha kwa madhumuni ya kuendeleza utalii
nchini, kuhifadhi, kuhudumia wanyama pori na kulinda wanyama ambao
idadi yao inapungua (tembo).
¨
Kilimo
Mpango
wa utafiti wa korosho
unaolenga katika utafiti wa kilimo juu ya uzalishaji wa zao la
korosho mkoani Mtwara kwa nia ya kufufua viwanda vya kahawa.
Mradi
wa kilimo cha mazao ya kibiashara, Zanzibar, wenye madhumuni ya
kuongeza pato la fedha za kigeni na kuongeza kipato cha jumuiya ya
wakulima kwa kuendeleza sekta ya mazao ya biashara.
¨
Afya
Mradi
wa Afya ya familia wenye lengo la kuimarisha afya ya uzazi na
kuzua kuenezwa kwa magonjwa ya zinaa.
Mradi huu uko katika wilaya nne za Mkoa wa Mbeya.
Mradi
wa kusaidia Afya na Lishe (Mbeya na Tukuyu).
Madhumuni ya mradi ni kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya,
kuimarisha mfumo wa maji na maji taka, huduma za uzazi wa mpango
wa majira, kuongeza uwezo wa kliniki na vituo vya afya pamoja na
kutoa huduma muhimu za afya na huduma za jamii.
Kuchangia
huduma za afya. Nia
ya mradi ni kuelezea na kuanzisha utaratibu wa kuchangia huduma za
afya kwa kuchunguza masharti yaliyopo kwa watumishi wa Serikali
kuingia mkataba wa lazima wa bima ya afya na kuanzisha mpango wa
kuchangia matibabu katika hospitali zote.
¨
Usafirishaji
na Miundombinu
Kuimarisha
mpango wa matengenezo ya barabara katika mikoa ya Iringa na
Ruvuma, ukarabati wa mifumo ya kupashana habari ya Shirika la Reli
la Tanzania na ukarabati wa magari moshi na mataruma.
¨
Mradi
wa kukarabati Bandari ya Tanga
Kuimarisha
shughuli za bandari ya Tanga na kusaidia mradi wa Benki ya Dunia
ya kuimarisha bandari ya Dar es Salaam.
¨
Urari
wa malipo
Kusaidia
urekebishaji wa uchumi wa nchi
¨
The
Multilateral Debt Relief Fund (MDF)
Mfuko
wa MDF ulianzishwa mwezi Julai, 1998 kwa
nia ya kushughulikia malipo ya madeni na kuchangia fedha
kusaidia sekta ya jamii yenye kujiwekea akiba.
Nchi sita
zikiwemo Uingereza, Sweden, Ireland, Norway, Finland na Denmark
ziliweka saini kuuchangia mfuko huu.
¨
Kuendeleza
Sekta Binafsi
Mradi
unalenga kuzisaidia biashara ndogondogo za ngazi za kati, pamoja
na kuzitafutia masoko ya nje.
Mipango mingine inayobuniwa ni pamoja na kusaidia mpango wa
biashara na kuongeza mapato kwa ajili ya wanawake.
Maeneo
mengine yanahusu kusaidia Venture Capital
Fund na Tanganyika Development Finance Company Ltd (TDFL).
¨
Mipango
ya kibanadamu
Kusaidia
shida ya maji katika jiji la Dar es Salaam, wakimbizi wa Rwanda na
dharura.
¨
Mabadiliko
ya Kituo cha Tanzania cha Uwekezaji
Kutayarisha
marekebisho ya mpango wa biashara wa kituo cha uwekezaji.
¨
Idara
ya Taifa ya Takwimu
Kusaidia
matayarisho ya zoezi la kuhesabu watu litakalofanyika mwaka 2002.
MAREKANI (USA)
Utangulizi
Ushirikiano
wa maendeleo baina ya Tanzania na Marekani unalenga katika maeneo
makuu matano ya afya, mazingira na maliasili, utawala, maendeleo
ya sekta binafsi na miundombinu.
¨
Miradi
inayoendelea
Kuongeza
juhudi za kutumia mpango wa uzazi wa majira na kuzuia ugonjwa wa
ukimwi.
Kupanga
na kutathmini usimamizi wa wanyama pori.
Mradi
wa ushirikishwaji wa kusimamia mazingira na rasilimali.
Kusaidia
juhudi za kujenga demokrasia nchini Tanzania.
Kusaidia
kuanzisha na kuimarisha kituo cha biashara.
Kutayarisha
ramani za barabara za kumsaidia mwekezaji.
Kuanzisha
“Venture Capital Fund” na
Social Action Trust Fund”
Kusaidia
mabaraza ya biashara
Kusaidia
mipango ya maendeleo ya mambo ya fedha na biashara.
BENKI YA AFRIKA YA MAENDELEO (ADB)
Benki
ilianza shughuli za kukopesha nchini Tanzania mwaka 1971. Hadi kufikia tarehe 31/12/2000 Benki iliidhinisha shughuli 69
ikiwemo miradi 33, mikopo 3 yenye mwelekeo wa viwanda, shughuli 20
za utafiti na 4 zinazohusu sera, na kusaidia mikopo 2 inayohusu
ushauri wa fedha.
¨
Shughuli
za Sekta Binafsi.
Tangu
kuanza kushughulika na sekta binafsi hapo 1991, Benki imeidhinisha
mikopo miwili nchini Tanzania, ambayo ni Graphan Limited (kuhusu
madini) na Aquva Limited (kuhusu masuala ya kilimo).
Katika
kipindi cha muda mfupi serikali itaingia mkataba na watoaji huduma
watakaotoa mafunzo na kujenga uwezo wa wakulima na wanachama wa
vyama vya ushirika (MAMCOS) ili kuwawezesha kupata huduma
zinazohitajika kutoka wakala wa Taifa wa Umwagiliaji (National
Irrigation Agency – NIA) na mashirika mengineyo.
Watoaji hao wa huduma pia watawasaidia wakulima kupata
masoko ya bidhaa zao.
¨
Mpango
wa Benki wa kukopesha wa muda mfupi na wa kipindi cha 1999 –
2001
Msukumo
wa kukopesha kwa Tanzania katika kipindi hiki unalenga kusaidia
maeneo ya kilimo, huduma ya jamii na huduma zinazotumika na watu
wote kama ifuatavyo:-
-
Mradi wa kukarabati mfumo wa maji safi na maji taka jijini
Dar es Salaam.
-
Ukarabati wa barabaa vijijini.
-
Structural Adjustment Loan II kwa ajili ya
¨
Utawala
¨
Maendeleo ya binadamu
¨
Maendeleo ya kilimo na ya
vijijini
¨
Kusimamia na kutathmini mpango wa
umaskini (PRSP).
-
Kusaidia uwezo kwa Wizara ya Afya.
-
Kusaidia utafiti wa matengenezo ya barabara ya Dodoma –
Singida.
-
Mradi wa kusaidia masuala ya
rutuba ya udongo na ukuzaji wa shughuli za kilimo.
¨
Miradi
inayobuniwa.
-
Mradi wa Elimu ya kazi na ufundi II.
-
Mradi wa kukarabati viwanja vya ndege.
-
Mradi wa maendeleo ya uvuvi Zanzibar.
-
Mradi wa utafiti na upanuzi wa kilimo II
UMOJA WA ULAYA (EU)
Utangulizi:
Tanzania
ni mwanachama wa mkataba wa LOME I (1975) na kwa sasa ni
mwanachama wa ACP kwenye mkataba wa LOME IV (kipindi cha 1991 –
2000 na kusainiwa 1989).
¨
Mipango
na kazi zinazoendelea
¨
Mfuko
wa 8 wa Maendeleo ya Ulaya (European Development Fund – EDF)
Makubaliano
ya ushirikiano kwa ajili ya “National Indicative Programme (NIP)
ya 8 ya mfuko huo uliwekwa saini Machi, 1997 na unashughulika na
sekta/miradi ifuatayo:
¨
Usafiri
-
Matengenezo ya barabara za Mwanza.
-
Matengenezo ya barabara ya Mwanza – Nzega/Isaka.
-
Kuimarisha sekta ya barabara
-
Matengenezo ya msimu
¨
Upatikanaji
wa maji na kushughulikia maji taka
-
Utoaji maji mjini Iringa.
-
Kushughulikia mfumo wa maji machafu Mwanza.
-
Utoaji maji mjini Mwanza
¨
Elimu
-
Mpango wa Maendeleo wa sekta
ya elimu.
¨
Kilimo
Msaada
kwa sekta ya kilimo unatolewa kupitia mpango wa STABEX na bajeti
iliyotayarishwa na siyo kupitia miradi ya “National Indicative
Progrmme” (NIP).
Tanzania
chini ya makubaliano ya LOME IV, imefaidika na msaada kwa ajili ya
mazao ya kahawa, pamba, chai, katani na karafuu.
Kutokana na umaarufu wa kahawa kuwa moja ya zao kuu
linaloiingizia Tanzania fedha za kigeni, mfuko wa 8 wa maendeleo
ya Ulaya litasaidia katika kuleta mabadiliko na mipango katika
kuiimarisha uzalishaji wa kahawa.
¨
Utalii
na Maliasili
-
Kusaidia mradi wa hifadhai ya Serengeti.
-
Kuimarisha sekta ya utalii (TANAPA)
¨
Maeneo
mengine ya ushirikiano.
-
Kupunguza shida inayosababishwa na wakimbizi kwa kuimarisha
miundombinu, huduma mbalimbali na
hifadhi ya mazingira katika eneo la kaskazini-mashariki ya
Tanzania.
-
Mkopo wa Benki ya uwekezaji ya Ulaya (European Investment
Bank – EIB) kwa viwanja vya ndege vya Dar es Salaam na
Kilimanjaro kwa ajili ya mitambo ya kuongoza/mawasiliano ya ndege,
umeme na vifaa vya taa katika viwanja vya ndege.
Mradi huu unaghramiwa kwa pamoja na Benki Kuu/IDA na ORET.
-
Mpango wa kutoa mikopo ya rasilimali kwa Benki ya Maendeleo
ya Afrika Mashariki, Stanbic Tanzania na CRDB Bank ili kuzikopesha
sekta binafsi zikiwemo kilimo, ulimaji wa maua, madini, utalii na
kazi zingine zinazofanana.
|