WARAKA WA HAZINA NA. 14 WA MWAKA 2003 MGAO WA FEDHA
ZA MATUMIZI MENGINEYO (O.C) KWA ROBO YA TATU YA MWAKA KWA MWEZI JANUARI,
2002/2003
Kuanzia mwezi wa Desemba, 2000; Serikali ilianza kutangaza
kupitia vyombo vya habari fedha zinazotolewa kwa ajili ya matumizi mengineyo
(other charges OC) kwenye ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri. Hii ni taarifa ya tatu kwa mwaka wa fedha wa
2002/2003. Taarifa hii inatakiwa iwekwe
kwenye mbao za matangazo ya kila Afisa Mhasibu. Kwa muhtasari fedha zilizotolewa Januari mwaka 2002/2003 ni kama
ifuatavyo:-
(i) Deni la Taifa sh 20,440.0mln
(ii) Utawala 26,170.3mln
(iii) Ulinzi na Usalama
10,702.2mln
(iv) Huduma za Jamii
39,357.2mln
(v) Huduma za Uchumi 9,253.8mln
(vi) Uzalishaji 4,907.7mln
JUMLA Sh 110,831.2mln
Mchanganuo
wa fedha zilizotolewa kwa Wizara, Mikoa na Halmashauri, umeonyeshwa kwenye
majedwali 1, 2, 3.
Fedha za sekta zinazopewa kipaumbele za elimu, afya, maji, barabara, kilimo,
sheria na mahakama zimetolewa kwa
kipindi cha miezi miwili.
KATIBU MKUU
WIZARA YA FEDHA
DAR ES SALAAM