KIKWETE AFADHAISHWA NA MIGOGORO ISIYOKWISHA
AFRIKA
· ahimiza utashi wa kisiasa kuimaliza
· awashukuru viongozi wenzie kwa kumpongeza
· ahimiza kuutokomeza umaskini
Na
Maura Mwingira
Rais Jakaya Mrisho amesema inasikitisha
kuona baadhi ya maeneo ya bara la Afrika yakiwa bado yakabiliwa na migogoro
hata baada ya miaka mingi ya uhuru wa nchi hizo.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akitoa
hotuba ya shukrani wakati wa ufungaji wa mkutano wa sita wa kawaida wa viongozi
wakuu wa nchi na serikali uliomalizika leo hapa Khartoum Sudan.
Rais ambaye huu ulikuwa ni mkutano wake wa
kwanza kuhudhuria akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alieleza
kwamba licha ya migogoro hiyo kuwapo katika nchi hizo, utatuzi wake
umekuwa ukichukua muda mrefu kwa kile alichosema ni ushirikiano mdogo
kutoka kwa wadau.
Rais ambaye alizungumza kwa lugha ya Kiswahili,
alisema kuwapo kwa migogoro hiyo pia kunaziathiri siyo tu nchi
zinazohusika bali pia hata zile zinazopakana nazo.
Wimbi la wakimbizi, matatizo ya usalama,
kudidimia kwa uchumi na kudodora kwa huduma za kijamii ni baadhi tu ya athari
zinazozikabili nchi zinazopakana na zile zenye migogoro.
"Hata kwa zile nchi ambazo ziko mbali na
nchi zenye migogoro, nazo zinaathiriwa na taswira mbaya inayotokana na migogoro
hiyo. Hivi ni lini viongozi wenzangu
taarifa za migogoro ya Afrika zitaacha kupamba vichwa vya habari katika nchi
zetu na dunia? akahoji Rais.
Na kuongeza kuwa ni vigumu kwa bara la Afrika
kujinasua na kujiendeleza kiuchumi na kijamii
Rais akawaeleza viongozi wenzie kwamba
Akasema kuwa mwezi huu,
Akabainisha kuwa nchi nyingi za Afrika ambazo
zinahusika moja kwa moja na machakato wa amani na maendeleo katika kanda
hiyo zimealikwa kushiriki kwenye majadiliano hayo. Ambayo alisema yatawahusisha
Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje.
"Napenda kuhimiza nchi zilizoalikwa
kuhudhuria majadiliano haya ya wazi yatakayofanyika
Aidha Rais Kikwete alisema kuwa jambo jingine ambalo alipenda kulizungumza
katika mkutano huo ni namna ya kushughulikia tatizo la umaskini katika
Bara la Afrika.
Amesema kuwa tafiti mbalimbali zimefanywa juu ya
kiini cha umaskini barani Afrika, na mambo mengi yamependekezwa juu
ya namna ya kupata ufumbuzi wa tatizo
Akasema Rais, "Kimsingi, Afrika inaendelea
kugubikwa na umaskini, lakini suala la kujiuliza ni kwa nini Afrika,
ambayo inautajiri mwingi wa raslimali
Akabainisha kuwa ili kuondokana na umaskini huo,
Afrika inatakiwa kutekeleza mkakati wa pamoja uliopendekezwa na Jeffrey Sachs,
mshauri wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Mkakati unaozihusisha nchi tajiri
na maskini.
Akasema mkakati huo unalenga kusaidia nchi
maskini angalau kutekeleza kwa wakati Malengo ya Maendeleo ya Milenia,
yanayohusu programu za kutokomeza umaskini.
Akasisitiza kuwa mkakati huo unajumuia pia
ufutaji wa madeni, kuandaa sera za biashara za kimataifa zinazofaa nchi maskini
"Umoja wa Afrika na nchi zetu kwa ujumla ni
vema zikatambua wajibu wake katika jambo hili na kuutumiza ipasavyo,
pamoja na kuyahimiza mataifa makubwa kutumiza wajibu
wao",akasisitiza Rais.
Akizungumzia kuhusu Mkutano wa sita wa AU, Rais
alisema kuwa amefarijika sana na namna mkutano huo ulivyoendeshwa, lakini
amefarijika zaidi na mapokezi mazuri na pongezi alizopewa na viongozi wenzake
kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akasema, salamu hizo za pongezi zimedhihirisha
urafiki na upendo wao kwake na kuthibitisha mahusiano mazuri yaliyojengeka kati
ya
"Napenda kuwathibitishia nia yangu na ya
serikali yangu ya kuendeleza mahusiano hayo mazuri, pamoja na kuendeleza
mchango wetu katika kuimarisha Umoja wa Afrika.
Akawashukuru kwa kumchagua yeye kutoka hotuba ya
shukrani kwa niaba ya viongozi wenzie.
Rais pia alimpongeza Rais wa
Akasema Rais "kwa niaba yangu na wananchi
wa Tanzania tumefurahishwa na ushidi wako wa kihistoria kwa nchi yako na
bara letu la Afrika. Na kuhakikishia ushirikiano wangu na ule wa serikali na
nchi yangu".
Aidha Rais alimpongeza Rais wa Sudan Omar El
Bashir na viongozi wa SPLA chini ya marehemu John Garang na sasa Mhe. Salva
Kiir, Makamu wa Ris wa Sudan kwa ujasiri wao na moyo wao wa uzalendo kwa
nchi yao na huruma wa raia wao waliokuwa wakiteseka kwa madhara ya vita.
Rais na Ujumbe wake anarejea nyumbani kesho (Jumatano)
Mwisho.
Maura Mwingira