PRESS SECRETARY TO THE PRESIDENT
Fax. No. 255-22 2113425 The State House,
Tel:
DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SITAINGILIA
UHURU WA MAHAKAMA-KIKWETE
·
Aahidi kuongeza idadi
ya majaji wa mahakama ya rufaa
Na Mwandishi Maalum
14/2/2006
Ikulu
Rais Jakaya Kikwete amesisitiza kwamba, serikali ya awamu ya
nne itajitahidi kuheshimu utawala wa
sheria na kutoingilia uhuru wa mahakama.
Ametoa ahadi hiyo jana (Jumatatu)
wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa mahakama ya Tanzania, katika
mfululizo wake wa kuzitembelea wizara na idara mbalimbali za serikali.
“Narudia tena, kama nilivyozungumza wakati nalihutubia Bunge, serikali ya
awamu ya nne itajitahidi kuheshimu utawala wa sheria na kutoingilia uhuru wa
mahakama, mimi sitafanya hivyo na nitahakikisha kuwa na wenzagu hawafanyi
hiyo”. Akasema Rais.
Akakitaka chombo hicho
kinachosimamia utoaji wa haki, kuwa huru kabisa katika kutimiza majukumu yake.
Na kuongeza kuwa uhuru huo lazima uhakikishe kuwa raia wanapata haki zao kwa
wakati na kwa usawa.
Hata hivyo Rais alisema kuwa pamoja na kuwa mahakama iko huru katika
utekelezaji wa majukumu yake, lakini uwezeshaji uko ndani ya serikali.
“Ninachoweza kuwaahidi ni kwamba tutatimiza wajibu wetu ili muweze
kutekekeleza wajibu wenu. Na katika uwezeshaji huo ni pamoja na uteuzi wa majaji wa mahakama ya rufaa mapema
iwezekanavyo”, akasema Rais.
Akasema kuwa serikali pia itajitahidi kuongeza bajeti ya mahakama pale hali ya mapato ikatakaporidhisha. Ikiwa ni pamoja na kuongeza watumishi wa idara nyingine, majengo na vitendea kazi vya kisasa.
Rais akatumia
nafasi hiyo kuipongeza mahakam ya
Akimkaribisha
Rais kuzungumza na uongozi wa mahakama ya
Akasema kuwa hivi sasa wapo majaji tisa tu katika mahakama hiyo ya rufaa ambayo ndiyo chombo cha juu kabisa. Idadi ya majaji inayotakiwa ili waweze kukabiliana na wingi wa kesi za rufa zinazofunguliwa katika mahakama hiyo ni 15.
Jaji Mkuu alisema kuwa hivi sasa majaji hao tisa wa mahakama ya rufaa waliopo wanashughulikia kesi kati ya 400 na 500 na kwamba kalenda ya usikilizaji wa kesi hizo imejaa hadi mwezi Agosti hali inayopelekea kesi mpya kupangiwa mwezi Septemba na kuendelea.
Akielezea zaidi
kuhusu upungufu wa watendaji katika mahakama ya
Aidha Jaji Mkuu
alibainisha kuwa bajeti halisi inayotakiwa kukidhi mahitaji ya mahakama ya
Kuhusu vita
dhidi ya rushwa miongoni mwa watumishi, Jaji Mkuu alisema kuwa vita dhidi ya
rushwa ndani ya mahakama ya
Akaeleza kuwa
Tume ya Utumishi wa Mhakama zimeendelea kuwastaafisha kazi mahakimu wote
walioonekana kwamba walijihusisha na vitendo vya rushwa hata
Katika mwaka 2004/2005 mahakimu wa walaya watano na mahakimu wa mahakama za mwanzo nane walistaafishwa kazi kwa makosa ya kinidhamu na kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Katika mazungumzo hayo, uongozi huo wa mahakama uliomba serikali kuangalia uwezekano wa kudhamini vipindi vya elimu ya uraia vinavyohusu kazi za mahakama ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuzifahamu vema haki zao na namna ya kuzitafuta.
Uongozi huo ulisema kuwa wananchi walio wengi hawana ufahamu na shughuli za mahakama, hali inayowafanya washindwe kutafuta haki zao. Aidha walipendekeza kuwa vianzishwe vipindi katika shule za msingi na sekondari ili kupanua uelewa wa wanafunzi katika masuala yanayohusu mahakama.
Mwisho.