PRESS SECRETARY TO THE PRESIDENT

 

Fax. No. 255-22 2113425                                   The State House,                        

Tel: 255-22-2116539/2116913                        P.O. Box 9120,

                                                                              DAR ES SALAAM.

E-mail:  press@ikulu.go.tz

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

 

TANZANIA KUENDELEA KUPETA IKIWA......                             ….1

 

Na Maura Mwingira

CapeTown

Afrika ya Kusini

1.6.2006

 

 

Imeelezwa kuwa Tanzania inaweza kuwa nchi yenye umaarufu mkubwa duniani na itakayokuwa katika nafasi kubwa zaidi kuvutia wawekezaji wengi zaidi na misaada ya moja kwa moja kutoka nje, ikiwa itahakikisha kuwa inalivalia njuga suala la ujenzi na uboreshaji wa miundombinu yake, pamoja na masuala ya fedha.

 

Mkurugenzi Mtendaji na Mjumbe wa Bodi ya  Taasisi isiyo ya kiserikali ya World Economic Forum, Bw Peter Torreale, aliyasema hayo wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa kwa ushirikiano wa taasisi hiyo na serikali ya Tanzania, kwa lengo la kuinadi Tanzania kama nchi yenye vivutivo vizuri vya uwekezaji katika bara la Afrika na duniani.

 

Bw. Torreale aliwaeleza wageni waliohudhuria chakula hicho, wageni ambao ni waalikwa wanaohudhuria mkutano wa maendeleo ya uchumi katika Afrika  kuwa Tanzania ni moja ya nchi inayofanya vizuri sana katika vigezo karibu vyote vinavyotakiwa katika kuvutia wawekezaji na mitaji.

 

Alibainisha kuwa katika utafiti uliofanyika mwaka jana na  wataalam wa masuala ya uchumi, ulionyesha kuwa Tanzania imepanda hadi nafasi ya 11 kwa kufanya vizuri katika vigezo mbalimbali vya kiuchumi (economic indicators)  vilivyowekwa na wataalamu hao wakishirikiana na Benki ya Dunia.

 

"Mkiendelea na utaratibu huu, sina shaka kwamba ifikapo mwaka 2011  Tanzania mtakuwa mnaongoza duniani kwa kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na kuvutia mitaji "alisisitiza Bw. Torreale.

TANZANIA KUENDELEA KUPETA IKIWA......                             ….1

 

 

 

Katika chakula hicho na ambacho Rais Jakaya Kikwete ndiyo aliyekuwa akiinadi nchi yake, na kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wageni hao, Bw. Torreale alisema  kuwa  hivi sasa Tanzania inashika nafasi ya tatu duniani baada ya Brazil na Turkey kwa kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na kuvutia mitaji. Na kuongeza kuwa ina kila nafasi ya kuzipita nchi hizo.

 

Akiinadi Tanzania katika chakula hicho, Rais Kikwete aliwataka wageni hao kutoka mataifa na makampuni mbalimbali kuiangalia Tanzania kama kituo kikuu cha uwekezaji.

 

Alisema kuwa serikali yake itaendelea na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji, ikiwa ni pamoja na kupitia sheria mbalimbali, kupunguza gharama za kufanya biashara.

 

Aidha Alisema kuwa Tanzania  ni kituo kikubwa cha biashara katika nchi za Afrika Mashariki na Kati na kusisitiza kuwa mazingira ya  kufanyia  biashara ni mazuri na masoko yapo na hivyo kuwahimiza waje kuwekeza Tanzania.

 

Aliongeza kuwa  Tanzania ni nchi ya amani na inayotawaliwa kwa misingi ya sheria, utawala bora na kuheshimu haki za binadamu.  hivyo kuwatoa hofu  kuhusu kupotea kwa mitaji hao. Na kusisitiza kuwa kuna nafasi nyingi za uwekezaji katika maeneo mbalimbali kuanzia utalii hadi kilimo, uvuvi, biashara ya usafirishaji, madini,  ufugaji na utoaji wa huduma mbalimbali za  kijamii kama vile afya na elimu.

 

"Njooni muwekeze Tanzania, njoo tushirikiane", akasema Rais.

 

Pamoja na Rais Kikwete kutoa maelezo yaliyowagusa na kuwavutia wageni waliohudhuria chakula hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji, Bw Ole Naiko, alitoa maelezo kwa njia ya powerpoint na namna gani Tanzania ilivyo na mazingira mazuri ya uwekezaji.

 

Katika maelezo yake, Bw.Ole Naiko alisema kuwa wawekezaji hawana sababu ya kutokuja na kuwekeza nchini kwa kuwa  taratibu zote za kuwawezesha kufanya hivyo zimekwisha kuainishwa na serikali.

 

Alibainisha kuwa katika utafiti uliofanywa na Gazeti la Financial Times toleo la 2005/2006, kuhusu nchi za Afrika zenye mwelekeo mzuri, alisema kuwa gazeti hilo liliitangaza Tanzania kama nchi inayoongoza katika Afrika Mashariki na Kati, katika kuvutia mitaji (FDI), na ikawa ya pili katika vigezo ya culture and heritage na  ikawa ya pili  nyuma ya Afrika ya Kusini katika vigezo vya eneo muhimu la kiuchumi ( economic pontential category).

 

 

TANZANIA KUENDELEA KUPETA IKIWA......                             ….3

 

Baadhi ya Maeneo ambayo wageni hao walioonyesha kuvutiwa nayo ni katika  uendelezaji wa sekta ya kilimo na elimu ambapo walitaka kujua serikali imeweka mikakati gani ya kuboresha maeneo hayo lakini vilevivile inatoa vivutio gani kwa watu wanaotaka kuwekeza katika maeneo hayo.

 

Rais Kikwete leo anaendelea na mkutano ambapo atashiriki katika mijadala mbalimbali.

 

 

Mwisho.