THE   UNITED   REPUBLIC   OF   TANZANIA

PRESS SECRETARY TO THE PRESIDENT

 

Fax. No. 255-22 2113425                                                  The State House,                        

Tel: 255-22-2116539/2116913                                           P.O. Box 9120,

 E-mail:  press@ikulu.go.tz                                            DAR ES SALAAM.

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

 

Ujumbe wa  Al Bashir  … 1

 

Rais Jakaya Kikwete leo asubuhi amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Omary Al- Bashir wa Sudan, ulioletwa  kwake na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Sudan Dr. Tijan Salehel Fidel.

 

Katika ujumbe huo, Rais Bashir amemwomba Rais Kikwete, kushiriki katika juhudi za kuleta amani na hasa katika utekelezaji wa makubaliano ya kuleta amani huko magharibi mwa Sudan, hususan katika jimbo la Darfur na pia kusaidia katika kushawishi vikundi vingine ambavyo havijasaini makubaliano hayo ya kusitisha mapigano ya Abuja , Darfur Peace Agreement (DPA) yaliyotiwa saini mwezi Mei mwaka huu.

 

Mgogoro wa Darfur huko magharibi mwa Sudan ulianza miaka mitatu iliopita kati ya serikali ya rais Bashir na kikundi kikuuu cha Sudan Liberation Movement (SLM) Ingawa makubaliano ya amani yameshatiwa saini na baadhi ya makundi  bado kuna vikundi vingine ambavyo havijasaini makubaliano hayo.

 

Kikundi kingine cha Uasi kijulikanacho kama Sudan Liberation Army (SLA), kimegawanyika katika makundi mawili moja likiongozwa na Minni Minnawi na lile la Abdul Walid Mohammed Al –Nur ambaye anashinikiza maelewano zaidi kutoka kwa serikali ya Omar Al Bashir.

 

Serikali ya Sudan inaiomba Tanzania kama mjumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuvishawishi vikundi ambavyo havijatia saini na kufikia makubaliano vifanye hivyo ili utekelezaji uweze kwenda haraka zaidi”. Waziri Fidel amemueleza Rais Kikwete wakati akimpa ujumbe toka kwa Rais Bashir.

 

Ujumbe wa  Al Bashir  …2

 

Waziri huyo wa ushirikiano wa kimataifa wa Sudan amemueleza Rais Kikwete kuwa migongano ilioko Sudan  ni ya kisiasa na kiuchumi hivo jitihada zaidi zinahitajika kuelezea umma kuwa si lazima kutumia silaha kufikia maelewano.

 

Mjumbe huyo wa Rias Bashir pia amemuomba Rais Kikwete arudishe uhusiano wa kibalozi kati ya nchi mbili hizi

 

 Tanzania ilifunga ubalozi wake huko Sudan kwa muda tangu Machi 1989  kutokana na matatizo ya kiuchumi, lakini majengo ya ubalozi yana kodishwa na Uganda.

 

Waziri huyo wa ushirikiano wa kimataifa wa  Sudan alifuatana na balozi wake hapa Tanzania, Balozi El -Mughira Ali Omar.

 

Mwisho

 

Ikulu,

Dar es Salaam

 

23 Juni, 2006