PRESS
SECRETARY TO THE PRESIDENT
Fax. No. 255-22
2113425 The State House,
Tel:
DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
JK AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA
AKUKWETI
Rais Jakaya Kikwete leo amewaongoza waombolezaji katika utoaji wa heshima
za mwisho kwa mwili wa Marehemu Juma
Akukweti, uliofanyika nyumbani kwa marehemu
Masaki, Jijini
Shughuli za utoaji wa heshima kwa mwili wa marehemu Akukweti zilifanyika kuanzia saa moja asubuhi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo marais wastaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Makamuwa Rais, Dk Mohammed Shein, na Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya
Viongozi wengine waliotoa heshima za mwisho, ni Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, Jaji Mkuu Barnabas Samatta, Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo, wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mawaziri, Naibu Mawaziri, Wabunge, Makatibu Wakuu, viongozi wa vyama vya siasa, wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.
Baada ya shughuli za kutoa heshima za mwisho kukamilika, ilifuatia sala kwa marehemu na dua zilizoongozwa na Naibu Mufti Sheikh Mkuu Abubakari Zuberi.
Baada ya sala na dua mwili wa marehemu Akukweti ulingizwa katika gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) namba 1776 JW04 na kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere tayari kwa safari ya kwenda Tunduru, mkoani Ruvuma kwa mazishi hayo kesho.
Mazishi hayo yataongozwa na Rais Jakaya Kikwete ambaye anaondoka leo mchana kuelekea Masasi na kesho Tunduru.
Mwisho.
Ikulu
06 Januari, 2007