PRESS
SECRETARY TO THE PRESIDENT
Fax. No. 255-22
2113425 The State
House,
Tel:
DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Premi Kibanga,
15.1.
07
Serikali ya Uingereza itachangia
paundi za uingereza 105 milioni kwenye bajeti ya
mwaka wa fedha wa 2007/8 kutoka paundi 90 milioni za mwaka
huu wa fedha
unaomalizika mwezi wa June. Mchango huu katika bajeti
ni kwa
ajili ya kusaidia juhudi za serikali katika
kupunguza umaskini kwa wananchi wa
Waziri wa Maendeleo
ya Kimataifa Hilary Benn amesema leo baada
ya mkutano wake na Rais Kikwete
na pia kutangaza
azma hiyo wakati wa mhadhara
kuhusu Maendeleo ya Afrika juu
ya Marekebisho ya Sekta ya
Utumishi wa Umma.
“Afrika inamudu kujifanyia marekebisho ikidhamiria, demokrasia inatendeka, uchumi unakuwa,
Bwana
Benn ameyataja mafanikio ya Tanzania kuwa ni kuongezeka kwa
idadi ya watoto waliojiandikisha katika shule za
msingi kuongezeka maradufu kutoka milioni 4 mwaka 2000 hadi milioni 8 hivi sasa, ikiwa ni
ongezeko la asilimia 96.(tisini na
sita), kukua kwa pato la Taifa
na uchumi kwa ujumla kutoka
asilimia 5 (tano) tangu mwaka 2000 hadi asilimia 7 (saba) kwa sasa
na kupungua kwa vifo vya
watoto wachanga katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Mapema katika Mhadhara kususu marekebisho ya Utumishi serikalini,
Rais Kikwete amesema
Rais Kikwete amesema tayari tume ya
kuangalia upya maslahi ya watumishi
wa umma imeshakamilisha
kazi yake na serikali itaanza
kuyatafakari mapendekezo yake, na kuwa
ana uhakika kwamba mapendekezo hayo yatatumika katika maamuzi..
“Marekebisho haya ya utumishi wa umma yanahusishwa
Mhadhara huo ulihudhuriwa na wanasiasa,
wafanyabiashara, wasomi, watafiti na mabalozi
kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika na Ulaya
ambao walipata nafasi ya kuuliza
maswali na kujibiwa na Rais.
Rais aliwasihi Waafrika walioko ulaya kushiriki
ipasavyo katika kuleta maendeleo na kuondosha
umaskini barani Afrika kwa kuunganisha
nguvu na mitaji yenye lengo
la kuweka vitega uchumi barani.
“Wito wangu kwa Waafrika wote nje ya
bara letu, mkusanye raslimali kwa nia ya
kuendeleza Afrika kwani hata wao
pia tunawahitaji na ni wenza
katika maendeleo na kuondosha umaskini.
Mapema kabla ya kutoa
mhadhara katika jumba la Chatam, Rais Kikwete alizungumza
na wafanyabiashara
wa Uingereza, hususan kwenye sekta ya Fedha
na kuwahimiza kuleta vitega uchumi
na kuwekeza
Katika kikao hicho Rais
ameelezea umuhimi na faida watakazopata
kwa kuwekeza Tanzania kuwa ni pamoja
na kuwa na
uhakika wa kufanya biashara katika mazingira ya amani na
utulivu, kuweza kupata wigo mkubwa
katika kufanya biashara na masoko
kwani Tanzania ni moja ya nchi
za Afrika Mashariki na pia
ndiyo lango kuu la kuingilia na kutokea nchi
za Maziwa Makuu.
Rais Kikwete leo asubuhi
( 16 Jan. 07) anakutana na Waziri Mkuu Tony Blair, Waziri wa Fedha Gordon Brown na Katibu Mkuu
wa Jumuiya ya Madola, Don McKinnon, Wabunge, viongozi wa vyama vya
siasa na dini kabla ya
kufanya mkutano na waandishi wa
habari kuzunngumzia ziara yake.
Mwisho