THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

 

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY TO THE PRESIDENT

 

Fax. No. 255-22 2113425                                                  The State House,                

Tel: 255-22-2116539/2116913                                          P.O. Box 9120,

                                                                                           DAR ES SALAAM.

E-mail:  press@ikulu.go.tz                                             

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

 

 

AU YAMPONGEZA BAN-KI MOON KWA UTEUZI WA MIGIRO

 

  • Yeye asema  anasifa zote za uongozi

 

Na Maura Mwingira

29/01.2007

  • ADDS ABBA

 

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika,  Bw. Alpha Konare, amempongeza na kumshukuru Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki- Moon kwa uamuzi wake wa kumteua mwana wa Afrika, Dk. Asha-Rozi Migiro kuwa Naibu wake.

 

Bw. Konare amesema uamunzi wa Moon kumteua Dk. Migiro kuwa Naibu wake, ni kilelezo cha namna gani anavyolijali   Bara la Afrika na nia yake ya kutaka kuleta mabadiliko ya dhati katika Umoja wa Mataifa.

 

Ameyasema hayo  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nane wa siku mbili wa viongozi  Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika ambao umeanza leo hapa Addis Ababa , Ethiopia.

 

Rais Jakaya Kikwete  ni miongoni mwa viongozi wakuu wa nchi wanaohudhuria mkutano huu akiongoza ujumbe wa Tanzania, unaowajumuisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe, Bernard Membe, Waziri  wa Utawala Bora kutoka serikali ya mapinduzi Zanzibar, Ramadhani Shabani, Mbunge kutoka  CUF, Khalifa S. Khalifa na Mbunge wa CCM Dk, James Wanyancha.

 

Bw. Konare  alisema uamuzi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano huu wa AU ikiwa ni takribani mwezi mmoja tu tangu achukue uongozi wa Taasisi hiyo  ni udhihirisho wa namna anavyotoka umuhimu wa kipekee kwa bara la Afrika.

 

Aliueleza mkutano huo ambayo ajenda yake kuu  ni Sayansi, Teknolojia na Utafiti kwa Maendeleo ya Afrika, pamoja na Mabadiliko ya Hali ya Hewa kwa Afrika, kwamba, Umoja wa Afrika, unaamini kwamba Katibu Mkuu huyo ataendelea kutoa kipaumbele  cha pekee katika mazuala yote yanayolihusu bara la Afrika.

 

Akaongeza kwamba licha ya hali tete ya usalama katika maeneo mengi ya bara la Afrika, AU itaendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika changamoto za  kukamilisha malengo ya maendeleo ya millennia  na kupamba na umaskini.

 

Konare alibainisha kwamba, mabadiliko ambayo Ban Ki Moon ameanza kuyafanya katika UN kama vile kumchagua Naibu wake kutoka Afrika, yanapashwa kufanyika pia katika  Taasisi nyingine za UN kama kile  UNESCO  na WHO.

 

Alisema afrika inahitaji  mabadiliko ya kweli ili na nayo iweze kutambulika,  na kujulikana na kusisitiza kwamba mabadiliko yoyote yatakayofanyika katika UN ni lazima yafanyike kwa haki na  uwazi.

 

Aidha Mwenyekiti huyo wa Tume ya Umoja wa Afrika, alisisitiza kuwa muhimu kwamba mabadiliko katika Umoja wa Mataifa yakajadili kwa kina uhusiano na ushirikiano  uliopo kati ya  Nchi za Afrika na Taasisi za Fedha za Kimataifa ambazo zimekuwa zikitoa misaada yake kwa Afrika.

 

Hata hivyo alisema licha ya Taasisi hizo kutoka  misaada yake wa Afrika, masharti yanayoendana na misaada hiyo yanaendelea kuziumiza na kuzikandamiza nchi za Afrika. Hali aliyosema, Katibu Mkuu huyo anapaswa kuiangalia hali hiyo kwa kina.

 

Akizungumza  wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon alisema. “Anashukuru sana  hususani kwa kuweza kumchagua Naibu wake, Mwana Mama kutoka Afrika, ambaye ana sifa zote za uongozi naye ni Dk. Asha-Rose Migiro” kauli iliyoshangiliwa na  wajumbe wa mkutano huo.

 

Aliongeza,  kuwa bila shaka wajumbe wa mkutano huo wa nane wa Umoja wa Afrika watakuwa wanamfahamu vizuri, Naibu wake, Dk. Asha-Rose Migiro ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.

 

Bw. Ban Ki Moon alisema kuwa amesimama mbele  viongonzi wakuu wa nchi na serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, kutoa shukrani zake kwa imani kubwa walioonyesha kwake na  kufanikisha yeye kuchukua uongozi wa Umoja wa Mataifa.

 

Alisema kuwa imani kubwa ambayo ilionyeshwa na viongozi wa Afrika, pamoja na kumpigia kura wakati wa mchakato wa kumpata katibu mkuu wa umoja huo, ni  udhihirisho kwamba walimwamini kuwa anaweza kuliongoza jahazi hilo.

 

Alibainisha kwamba, katika kupindi chake kifupi cha uongozi katika UN, tayari amekwisha kujenga urafiki na uhusiano wa karibu na viongozi wa Afrika, na kwamba ni matumaini yake kwamba watampatia ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa majukumu  yake.

 

Alitumia nafasi hiyo kutoa shukrani zake kwa mtangulizi wake, Bw. Koff Annan aliyemwelezea kama mwana wa Afrika ambaye alileta mageuzi makubwa katika Umoja wa Afrika.

 

Aliongeza kuwa Bw. Annan aliweza kukuza na kuboresha mahusiano kati ya  bara la Afrika na Umoja wa Mataifa  hali ambayo umoja huo hivi sasa unalitambua bara la Afrika kuwa ndilo chimbuko la mwanadamu.

 

“Annan alifanya kazi kubwa sana ya kuleta mabadiliko katika umoja wa  wa mataifa ndiye aliyeiingia UN katika karne ya 21, hivi sisi tunapo kuja hapa afrika,  tunarudi kwenye chimbuko letu” alisema Bw. Moon.

 

Aliahidi kufanya kazi bega kwa bega na Umoja wa Afrika katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazolikabili Bara hilo na Umoja wa Mataifa kwa ujumla.

 

Mwisho.