PRESS SECRETARY TO THE PRESIDENT
Fax. No. 255-22
2113425 The State
House,
Tel:
DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete kuhutubia mkutano wa Ajira.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
ni mmoja wa viongozi wa
Afrika wanaotarajiwa kuhutubia mkutano wa 11 wa kanda ya Afrika wa
Shirika la Kazi Duniani (ILO) kuzungumzia maendeleo na kutoa muelekeo
wa ajira barani Afrika, utakaoanza Addis Ababa, Ethiopia tarehe
23 April, 2007.
Mkutano
huu wa Shirika
la Kazi Duniani hufanyika kila baada ya miaka
minne na kukusanya baadhi ya viongozi kutoka
nchi 53 barani. Rais ataondoka Kesho Jumapili tarehe 22 April, 2007 kuelekea
Katika kikao kilichofanyika Ouagadougou,
Burkina Faso, Septemba 2004, kuhusu
Ajira na Kuondoa Umaskini viongozi wa Afrika waliohudhuria kikao hicho waliahidi
na kuweka dhahiri kutoa kipaumbele kwenye kutengeneza ajira ili iwe
kitovu na lengo kuu katika
sera za kiuchumi na kijamii katika
ngazi ya nchi, kanda na barani
kwa ujumla kwa nia ya
kuondoa umaskini na kuboresha hali
za maisha ya watu.
Tangu kutolewa kwa
mapendekezo hayo, kukuza ajira zenye
tija katika mazingira yenye hadhi kumepewa kipaumbele siyo kwa nchi na
barani tu bali imekuwa lengo
la kimataifa.
Mkutano
huu wa 11 wa Viongozi utalenga
na kuainisha hatua zinazohitajika kufuatwa na kuchukuliwa
na nchi wanachama,
ILO na wenza wao katika maendeleo
kwa miaka ijayo, ili kuhakikisha
kuwa shabaha hii ya kuwa
na mazingira ya kazi yenye
hadhi na tija inafanikiwa na kutendeka barani,
ili kuweza kupata njia muafaka
ya kupunguza umaskini kwa njia
zinazokubalika.
Katika mkutano huo viongozi
watajadili ripoti mbalimbali zitakazotolewa na Mkurugenzi Mkuu
wa ILO ambazo zitaelezea jinsi ILO ilivyofanya kazi na nchi wanachama,
hasa nchi za Afrika na
ripoti yenye kuelezea malengo halisi ya dunia
na Afrika, kuainisha sera na mifano halisi ambayo
ni muhimu kutekelezwa katika ajira zenye hadhi.
Mkutano pia utashuhudia
ripoti za ILO zikitolewa mkutanoni zinazoelezea mifano kadhaa kuonyesha juhudi katika ajira
zenye hadhi barani na
pia kuonyesha muelekeo, muhtasari na mchanganuo wa
hali ya ajira
barani. Rais atarejea nchini
tarehe 25 April, 07.
Imetolewa na
ikulu,
April 21, 07