PRESS
SECRETARY TO THE PRESIDENT

Tel:
Fax. No. 255-22 2113425 DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Jakaya Kikwete leo amekuwa
na mazungumzo na Naibu Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika
la Fedha la Kimataifa
(IMF), Bw. Murilo
Katika mazungumzo
“Nimesoma
katika magazeti ya leo juu
ya kauli yako kuhusu matumizi
mabaya ya fedha za serikali
na hatua unazokusudia kuchukua, huu ni mwanzo
mzuri, na ninaamini kwamba kutakuwa
na matokeo bora” amesema Bw.
Ameongeza kuwa hatua hiyo pia imepokelewa vema na wabunge wa Kamati ya Fedha wakiongozwa na Mbunge wa UDP. John Cheyo ambao alikutana nao leo, na wamemwelezea kwamba sasa wana imani kwamba na wana Rais ambaye anaunga mkono uwajibikaji.
Naibu Mkurugenzi Mkuuhuyo wa IMF amesema tatizo la matumizi mabaya ya fedha za
serikali haliko
Amebainisha
kwamba wakati Serikali Kuu zinajitahidi
kurekebisha makosa
Amemweleza Rais kwamba fedha za serikali katika nchi yoyote ni lazima zitumike vizuri ile kuleta matokeo yaliyotarajiwa na kwamba udhibiti wa fedha hizo na uhakiki wa matumizi yake ni jambo la msingi sana.
Katika mazungumzo hayo, Naibu Mkurugenzi Mkuu alitaka, pamoja na mambo mengine kupata maelezo kutoka kwa Rais kuhusu mipango mbalimbali ya maendeleo na kiuchumi inayofanywa na serikali.
Aidha amesema kuwa IMF inaridhika na hali ya mambo ilivyo nchini pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali, na kuahidi kwamba itendeleza ushirikiano wake na Tanzania pamoja na kutoa misaada ya kiufundi, na kimawazo wakati wowote Tanzania itakapohitaji msaada wa aina hiyo.
Kwa upande
wake, Rais Jakaya Kikwete ,
amesema bado
Rais amesema kuwa tatizo la udhibiti mbaya ya mapato ya matumizi ya fedha za serikali ni tatizo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likimkosesha amani, na ambalo alikuwa akilitafutia mahali pa kuanzia.
“Ripoti hii ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imenipa mahali pa kuanzia, kwani ni tatizo ambalo limekuwa likininyima raha, na maneno niliyoyasema jana kwenye mkutano wangu na watendaji wa serikali za mitaa, si maneno ya vitisho tu bali ninamaanisha yale niliyoyasema. Sitasita kuzivunja halmashauri zitakazoendelea kufanya vibaya na kuitisha uchaguzi mwingine,.
Rais amesisitiza kuwa serikali yake itaendelea kuweka mkazo katika uendelezaji wa kilimo ili kiwe cha kisasa na hivyo kuongeza tija kwa mkulima na kuboresha maisha yake.
Aidha amesema mchakato za kupanua na kuboresha huduma za elimu, afya, nishati na miundombinu, ni mchakato endelevu, na kwamba ukusanyaji wa mapato na uwezeshaji wa chombo kinachohusika na ukusanyaji wa mapato hayo ni jambo linalopewa kipaumbele na serikali.
Mazungumzo kati ya Rais na Naibu Mkurugenzi wa IFM, Bw. Murilo Portugal yalihuduhiriwa pia na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, Gavana wa Benki Kuu, Daudi Balali na Katibu Mkuu Fedha, Bw. Gray Mgonja.
Mwisho.
Ikulu
DAR ES SALAAM
30/04/2007