PRESS
SECRETARY TO THE PRESIDENT

Tel:
Fax. No. 255-22 2113425 DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali inafanya marekebisho
katika sekta ya madini ili kupata faida na mapato
zaidi kwa ajili ya wananchi
wake.
Katika marekebisho hayo,
Serikali imeshafanya majadiliano na
kukubaliana na kampuni za Barrick Tanzania Limited (inayomiliki migodi ya Bulyanhulu
ulioko wilayani Kahama, Tulawaka ulioko wilayani Biharamulo; na North Mara ulioko wilayani Tarime) na Resolute Tanzania Limited (inayomiliki mgodi wa Golden Pride ulioko wilayani Nzega) ili kuyawezesha
kampuni hizi kulipa kodi na
ushuru stahili kwa Serikali.
Katika majadiliano hayo
kampuni hizi zimekubali kuondolewa
kwenye mikataba baadhi ya vivutio
vya ziada ikiwa ni
pamoja na nyongeza ya asilimia 15 kwenye mtaji
wa uwekezaji ambao haujarejeshwa/kukombolewa (15% additional capital allowance
on unredeemed qualifying capital
expenditure). Hatua hii itawezesha kampuni hizi kukomboa gharama zao za
uwekezaji mapema na hivyo kulipa kodi ya mapato (corporate tax). Endapo kipengele hicho kisingeondolewa, kungekuwa
na uwezekano mkubwa wa kampuni hizo kutolipa corporate tax.
Serikali bado inaendelea na majadiliano na kampuni ya Geita Gold Mine
Limited inayomiliki mgodi wa Geita ili nayo ikubali kufuta kipengele hiki
kwenye mkataba wake. Hata hivyo, Serikali tayari ilisharekebisha kipengele hiki
cha 15% additional capital allowance on
unredeemed qualifying capital expedicture, kilichokuwa kwenye Sheria ya
Kodi ya mwaka 1973 ambayo ilifanyiwa marekebisho. Sheria ya Kodi ya mwaka 2004
haina kipengele hicho tena, hivyo
mikataba mipya ya madini haitakuwa na kipengele hiki.
Pamoja na suala la ulipwaji kodi ya mapato (corporate tax), kampuni hutakiwa kulipa
kodi na ushuru mbalimbali ikiwemo mrabaha. Mrabaha wa asilimia 3 kwa madini ya
dhahabu na madini mengineyo; na asilimia 5 kwa madini ya almasi na vito hulipwa
Serikalini bila kujali kama kampuni inapata hasara au faida tofauti na kodi ya
mapato (corporate tax) ambayo hulipwa
baada ya kampuni kupata faida kwa kuondoa gharama za uendeshaji na uzalishaji.
Kodi nyingine zinazolipwa na kampuni za madini ni pamoja na kodi ya zuio (withholding taxes) kodi za ajira (PAYE);
ushuru wa forodha, stamp duty; ambapo ushuru ni pamoja na ada ya pango (annual rent), ada ya maombi na
utayarishaji wa leseni za utafutaji (application
and preparation fee); na ada za leseni mbalimbali za biashara ya madini.
Katika jitihada za Serikali za kuhakikisha sekta ya
madini inachangia ipasavyo kijamii na kiuchumi inafanyia marekebisho Sera ya
Madini ya mwaka 1997. Aidha, Sheria ya
Madini ya mwaka 1998 nayo inafanyiwa marekebisho ili kuhakikisha usimamizi wa
sekta ya madini unaihakikishia Serikali na wananchi wake mapato zaidi kutokana
na rasilimali ya madini.
NB: Taarifa
hii tunaitoa kwa nia ya kufafanua taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa
zikinukuliwa kwenye magazeti wiki hii ambazo zinachanganya aina za kodi ambazo
wawekezaji katika migodi wanapaswa kulipa.
Imetolewa na:
Premi
Kibanga
Mwanza
08/05/2007