PRESS
SECRETARY TO THE PRESIDENT

The
State House,
Tel:
Fax. No. 255-22 2113425 DAR ES SALAAM.
E-mail:
press@ikulu.go.tz
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Na Mwandishi
Maalum
13/06/07
Ikulu
Rais Jakaya Kikwete amesema anayo
nia na dhamira ya dhati ya kuwaondoa Watanzania
katika maisha ya dhiki na umaskini.
Ameeleza kuwa hali ya umaskini inayowakabili zaidi ya asilimia 39 ya Watanzania hasa wale wa vijijini, ni
jambo linalomsumbua sana. na ndio maana
anabuni mikakati na mipango
mbalimbali ya kuwaibua wajasiriamali
wadogo na wakati ili hatimaye waongeze kipato chao na kuboresha maisha yao.
Kikwete ameyasema hayo jana jioni ( Jumanne) wakati alipokuwa
akibadilishana mawazo na mtaalam maarufu wa uchumi, mwanzilishi wa Benki ya
watu maskini Gramees Bank, na Mshindi wa
Tuzo ya Amani ya mwaka 2006 (Nobel Peace Prize Laurette) Professa Yunus Mohamed, kutoka Bangladesh.
Amesema kuanzishwa kwa mchakato wa utoaji
wa mikopo nafuu ambayo kwa sasa imepachikwa jina la mabilioni ya JK, ni sehemu tu ya mikakati yake ya kutafuta njia
muafaka za kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini na maskini.
Akifafanua zaidi, Rais amesema kunahitajika
ubunifu zaidi, utaalamu na utashi wa kisiasa kutoka kwa viongozi na wananchi
wenyewe katika mchakato mzima wa kuondokana na umaskini.
“Wakati wote wa kampeni za uchaguzi, nilijitahidi sana kuelezea nia na
dhamira yangu hiyo ya kuinua hali ya
maisha ya wananchi kwa kuwapatia fursa ya kupata mikopo nafuu ili hatimaye waweze kuendesha
shughuli za ujasiriamali zitakazowaongezea kipato. Ni dhamira niliyonayo
na ni jambo linalonigusa
Rais amemweleza ProfessaYunus
Mohamed kwamba, nia yake ya kumwalika
kuja hapa nchini ililenga hasa kutaka wabadilishane mawazo, uzoefu na mbinu
ambazo zitamuwezesha yeye binafsi
“Ninakushukuru sana professa kwa kuukubali mwaliko wangu, niliona ni bora tukutane na tuweze kubadilishana mawazo, lakini kubwa zaidi kuchota maarifa yako uliyotumia kuwaondolewa umaskini maelfu ya wananchi wa Bangladesh na kuboresha maisha yao kwa njia ya mikopo nafuu” amesema Rais.
Amebainisha kwamba siku zote amekuwa akiamini kwamba Mabenki ya biashara si rafiki wa watu maskini, hivyo inatakiwa kuundwa mifumo rasmi nje ya mifumo ya benki za biashara ambazo licha ya kutoza riba kubwa lakini zimejaa urasmu mkubwa inapofikia suala la kuwakopesha watu wa kipato cha chini.
Hata hivyo Rais amesema kidogo kidogo baadhi ya benki zimeanza kuwaamini na kuwakopesha watu wa kipato cha chini kwa kuwa wameonyesha uadilifu mkubwa wa kurudisha mikopo hiyo.
Akitoa mchango wake wa mawazo
ya nini
Amesema tofauti na ilivyo nchi kwake Bangladeshi ambao kuna mamilioni ya watu maskini, kwa Tanzania ambayo ina asilimia 39 sawa na familia milioni 2.5 tu ina kazi nyepesi zaidi ya kuwaondolea umaskini watu hao kwa kuwa nchi inazo raslimali nyingi, serikali mathubuti na kinachotakiwa ni ubunifu tu .
“
Ameongeza “kila mtu ni mjasiriamali, hata ombaomba yule wa mtaani anaweza kuwa mjasiriamali, tofauti iliyopo ni kwamba wengine walipata fursa ya kujipambanua na kuwa wajasiriamali, na kundi jingine halijawezeshwa kufanya hivyo” anasema Professa Yunus
Professa Yunus ambaye alikuwa hapa nchini kwa mwaliko maalum wa Rais Jakaya Kikwete, amemweleza Rais kwamba hakuna njia ya haraka na ya uhakika ya kuwaondoa wananchi katika umaskini kama ile ya kuwapatia fursa na uwezo wa kupata mikopo ama isiyo na riba kabisa au yenye riba ndogo sana.
“Wamiliki wengi wa Mabenki na hata wasomi, hawaliamini hili, lakini sisi tumedhihirisha kwamba inawezekana na tumelifanya kupitia benki yetu ya watu maskini, Gramees Bank” anasisitiza.
Amefafanua kwamba mkopo anaopewa mtu maskini unatakiwa kuwa wa bure au riba yake isizidi asilimia 10 kwani ikizidi hapo huo si mkopo wa kumwezesha mtu maskini kujiwezesha na kujinasua na umaskini…… “ ukizidisha riba juu ya asilimia kumi wewe si mkopeshaji bali unafanya biashara ya fedha” anasema.
Aidha Professa huyo amepinga ile dhana ya kwamba watu maskini hawalipi mikopo wanayopewa kwani amesema katika Benki ya Grameen ambayo yeye ni mwanzilishi wake, watu maskini na wengi wao wakiwa ni wanawake wameonyesha uadilifu wa hali ya juu katika urejeshaji wa mikopo kwa asilimia 98.
Ameelez kuwa Grameen Bank ni benki ambayo inajiendesha kwa amana ya watu hao maskini, na wala haitegemei au kupata fedha yoyote kutoka nje au kwa wafadhili.
“Grameen Bank, ni benki ya wananchi wenyewe, wanaimiliki wenyewe kwa amana zao, wala hatuna fedha yoyote kutoka kwa mfadhili, na hili hata nyinyi mnaliweza mkiamua, mkitegemea fedha ya mfadhili hamtafika kokote.
Katika mchango wake huo, Profesa Yunus, amemweleza Rais, kwamba katika utekelezaji wa mchakato wa kuwaondoa watu katika umaskini, lengo lisiwe ni watu wangapi wamefikiwa bali ni wangapi hawajafikiwa.
“Kila wakati malengo yenu yawe ni watu wangapi hatujawafikia, siyo wangapi tumeshafanikiwa kuwafikia, mkifanya hivyo mtabweteka, daima zingatieni hili, mwezi huu tunataka kuwafikia wangapi, miezi sita ijayo wangapi, mwakani wangapi hapo ndipo mtakapoweza kufanikiwa.
Aidha Professa huyo ambaye
anaheshimiwa
Amesema yuko tayari na wakati
wowote kushirikiana kwa hali na
Akiwa hapa nchini, pamoja na kuwa na mazungumzo na Rais, Profesa Yunus alikutana pia na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Gavana wa Benki Kuu, wamiliki wa Mabenki, asasi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na utoaji wa mikopo midogo midogo, watafiti na wataalamu wa uchumi.
Mwisho.