PRESS
SECRETARY TO THE PRESIDENT
OF
THE UNITED

The State House,
Tel:
Fax. No. 255-22 2113425 DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Premi Kibanga
Shinyanga.
29 Agosti,
2007
Serikali imeahidi kufanya kila iwezalo kuhakikisha
zao la Pamba halianguki. Rais amewaambia viongozi wa
Mkoa wa Shinyanga
leo wakati wa kikao cha majumuisho
ya ziara yake ya kikazi
ya siku nane
moani humo.
Lakini katika kuhakikisha
zao hili halianguki, nawategemea nyie viongozi na
mipango yenu Rais
amesema.
Akiwapa changamoto wenye viwanda mbalimbali vya kusafirisha pamba
nje ya nchi na
kutengeneza mafuta alisema Muende mbali zaidi, mzalishe
nyuzi na hatimaye nguo ili
kuongeza thamani ya pamba yetu.
Mkoa wa
Shinyanga unazalisha asilimia 60 ya pamba yote nchini.
Akizungumzia
kuhusu sekta nyingine muhimu kwa uchumi wa
mkoa wa Shinyanga,
Rais ameahidi kwamba sekta ya
mifugo itafanyiwa mageuzi ili kuzalisha
nyama kwa wingi, maziwa na
ngozi bora ili kukuza mapato
kwa wafugaji na taifa.
Amewahimiza
viongozi wa
mkoa huo kushirikana na wafugaji kuboresha huduma kwa mifugo
Kuhusu sekta ya kilimo,
Rais amesema Tuna nia ya kuongeza
matumizi ya maji, kuanzisha programu ya umwagiliaji,
kutumia mbegu bora na mbolea
ambapo serikali inatoa ruzuku na
inafanya jitihada ili ruzuku hiyo
iende kwenye mbolea moja kwa
moja. Akawataka wakulima kuzingatia kanuni bora za
kilimo.
Aidha Rais amebainisha kuwa Serikali itaajiri
maafisa ugani 2500 waliohitimu elimu ya Chuo Kikuu ambao
watapelekwa katika kila
kata na tarafa
kwa lengo la kutilia mkazo kilimo
na kukiongezea thamani.
Sambamba na kuajiri maafisa
ugani hao, Serikali pia itaimarisha
miundo mbinu, hasa barabara za
vijijini, na na
kutilia mkazo uimarishaji wa ushirika ambao ndiyo soko kubwa
kwa mkulima.
Kuhusu sekta ya madini
ambayo pia ni eneo muhimu
la uchumi mkoani Shinyanga, Serikali pia imeahidi kuendelea kuhamasisha wachimbaji wakubwa kuja kuwekeza
wakati huohuo ikiwahimiza kutimiza wajibu wao kwa jamii
inayowazunguka.
Aidha Rais amesema kuwa
kazi kubwa inafanyika ya kuwaendeleza
wachimbaji wadogo na kuyahimiza
makampuni wakubwa kuwaendeleza wachimbaji hao.
Akizungumzia tatizo kubwa
la maji Mkoani Shinyanga, Rais amesema kuwa Serikali imetenga Tshs. Bil. 250 katika bajeti ya maendeleo
kwa ajili
ya kutatua tatizo la maji Mkoani Shinyanga.
Rais amehitimisha ziara yake mkoani Shinyanga na kurejea
Mwisho.