PRESS
SECRETARY TO THE PRESIDENT
OF
THE UNITED

The State House,
Tel:
Fax. No. 255-22 2113425 DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
LIMENI MAZAO YA BIASHARA MUONDOKANE NA
UMASKINI - KIKWETE
Na Maura Mwingira
3/9/2007
KONGWA
Rais Jakaya Kikwete
amewataka wananchi wa wilaya ya Kongwa, kulifufua na kutilia mkazo zao la
karanga na ili liwe zao lao la biashara.
Amesema
umaskini utaondokana na maisha bora yatapatikana ikiwa wataelekeza nguvu
zao katika kulima mazao ya biashara kama karanga na ufuta, badala ya kuelekeza
nguvu zao kwa mazao ya chakula pekee.
Rais Kikwete ametoa
wito huo leo kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa akisalimiana na wananchi wa
vijiji vya wilaya ya Kongwa katika siku yake ya tatu ya ziara ya kikazi
mkoani dodoma .
“Mlilima sana
karanga kwa kusimamiwa na wakoloni, mlifanya kazi kwa wakoloni, leo wakoloni
wameondoka tumeacha kulima karanga kwa nini” akahoji Rais na kuongeza
“lifufueni zao hili kwani ndio litakalo waondoa kwenye umaskini na kuwapatia maisha
bora” akatitiza.
Amefafanua kwamba
wilaya au mkoa ambao hauna zao la biashara, ni wazi umaskini katika eneo hilo
hautatoweka na wananchi hawatakuwa na maisha bora. Na hivyo akawasisitizia
kujielekeza katika utafutaji wa mazao ya biashara.
Amewaeleza wananchi
hao kwamba serikali inaposema maisha bora kwa kila Mtanzania haimanishi kuwajaza
fedha mikononi bali ni kwa wananchi wenyewe kujishughuliza katika
kazi zitakazowapatia kipato na kuboresha maisha yao .
“Nimekwisha
kuzungumza na mkoa, kwamba wakati umefika sasa wa kutillia mkazo mazao ya
biashara, na kwa mkoa wenu mazao hayo ni karanga, mtama, na zabibu, la
sivyo Yesu atakapokuja kutuhukumu atatukuta bado tu maskini na tukiishi
katika nyumba za tembe.
Amewataka wananchi
hao kuzingatia maelekezo ya wataalamu na kanuni bora za kilimo na ufugaji kwa
kuwa ndiyo hasa mambo yatakayobadilisha maisha yao kwa haraka.
Aidha Rais
amewaeleza wananchi ambao waliojitokeza kwa wingi kumwona na kumsikiliza kwamba
serikali imejipanga vema kuwatumikia na kuwaondolea kero zao, na kwa wilaya
hiyo kero kubwa ni maji na barabara.
Kuhusu tatizo la
maji katika wilaya hiyo, Rais amewahakikisha wananchi kwamba tatizo hilo
litakwisha kabla ya mwisho wa mwaka huu, baada kukamilika kwa mradi
unafadhailiwa na Benki ya dunia.
Tayari asilimia 60
ya utekelezaji wa mradi huo ambao ni ujenzi wa matanki ya kuhifadhi maji na
utandikaji wa mabomba umekwisha kukamilika.
Kuhusu barabara, Rais
amesema Serikali imetenga shilingi milioni 800 kwa ajili ya barabara za wilaya
hiyo.
Akiwa katika wilaya ya
Kongwa, Rais alifungua jengo la wagonjwa wa nje katika hospitali ya
Wilaya hiyo ambalo limeghalimu shilingi milioni 86. Kukamilika kwa jengo
hilo kutasaidia sana kupunguza msongamano na wagonjwa na kuboresha huduma kwa
wananchi.
Aidha Rais aliweka
jiwe la msingi katika shule ya sekondari ya Sagara, shule hiyo ambayo ni
ya kata imejengwa kwa michango ya wananchi Serikali Kuu, Halmashauri na
wafadhili imegharimu shilingi milioni 91, kati ya hizo milioni 42 zimetumika
kwa jengo la utawala na milioni 49 kwa ujenzi wa madarasa saba.
Kwa kufurahishwa na
majengo mazuri ya shule hiyo ambao ina walimu 11 na wanafunzi 197, Rais
alichangia shillingi milioni mbili, wanafunzi wa shule hiyo wanapatiwa huduma
ya kifungua kinywa na chakula cha mchana ili kuwaepusha na utoro.
Kuhusu ukimwi, Rais
amewahimiza kujitokeza kwa wingi Septemba 22 kupima kwa hiari ili wajue hali ya
afya zao huku akiwasisitizia kutumia kinga ili kujiepusha na maambukizo mapya.
Wilaya ya Kongwa ina maambukizo ya asilimia 9.
Mwisho.