PRESS
SECRETARY TO THE PRESIDENT
OF
THE UNITED

The State House,
Tel:
Fax. No. 255-22 2113425 DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kikwete - ……….Ufisadi
Na Maura Mwingira
10/10/2007
ARUSHA
Rais
Jakaya Kikwete ameonya tabia inayotaka kujengeka miongoni mwa wananchi na
hususani wanasiasa ya kugeuka kuwa wapelelezi, wakamataji, waendesha mashtaka
na watoa hukumu, na tena wakizitoa huku hizo bila ya watuhumiwa kuwapo.
Amesema
tabia hiyo ikiachwa kuendelea siyo tu itaipeleka nchi pabaya, lakini itawatisha
wananchi, itawatia hofu na kujenga chuki kati ya mtu na mtu hali ambayo amesema
haiendani na taratibu za kuendesha nchi kwa misingi ya kufuata kanuni,
taratibu, na sheria za nchi.
Amebainisha
kwamba tabia hiyo ya wanasiasa kujigeuza kuwa wao ndio wapelelezi, wakamataji,
waendesha mashtaka na watoa hukumu kuwa haimtendei haki mtuhumiwa ambaye
naye ana haki yake ya msingi ya kulindwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Rais
Kikwete ameeleza kuwa kila taarifa inayohusu rushwa au tuhumu za mtu
kutuhumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa, zitachunguzwa kwa kuzingatia misingi
ya sheria za nchi na vyombo vinavyohusika na si vinginevyo na kuongeza kwamba
yeyote atakayethibitishwa na mamlaka halali kwamba ama ametoa rushwa au kupokea
rushwa atachukuliwa hatua za kisheria bila ya kujali nafasi na madaraka
aliyonayo.
Rais
kikwete ameyasema hayo jana usiku (Jumanne) wakati alipokuwa
akimshukuru Askofu Thomas Laiser wa Dayosisi Mkoani Arusha ya
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania, kwa kumpongeza (Kikwete) kwa
ujasiri mkubwa wa kupambana na vitendo vya rushwa na hasa
rushwa katika uchaguzi.
Askofu
Laiser alitoa pongezi hizo kwa Rais wakati wa hafla ya uchangiaji wa
ujenzi wa hosteli ya Dayosisi ya KKKT Arusha, hafla iliyofanyika katika
hoteli ya
Rais
Kikwete amebainisha kwamba nia na dhamira ya serikali ya Chama cha Mapinduzi ya
kupambana na vitendo vya rushwa ni ya dhati, na utekelezaji wa vita hivyo
umeanzia ndani ya Chama chenyewe.
“
Akasema
Kikwete “Mhe. Baba Askofu, naomba nikushukuru kwa kunipongeza kwa
juhudi zangu za kupambana na rushwa, nimefarijika
Akizungumzia
zaidi juhudi hizo za serikali za kupambana na rushwa ndani ya Chama cha Mapinduzi
na taifa kwa ujumla, Rais ameeleza kwa kusema “ Nilitoa ilani na tahadhari
kabla ya uchaguzi kuanza katika ngazi za wilaya, maana huko ndiko pesa
zinakotembea tembea. Niliwaambia wenzangu jamani taarifa hizi za kwamba
viongozi wanapata uongozi kwa kununua hii si heshima nzuri, tuachane na tabia
hii”.
Akaendelea
“Tuliviagiza vyombo vyetu kuifanya kazi hiyo. Lakini tunafanya hivyo kwa
kuzingatia misingi ya kanuni, taratibu na sheria za nchi”. Anasema Kikwete na
kuongeza “ Hata wale TAKUKURU wakisema huyu tumemkamata akitoa rushwa au
katika mazingira ya kutoa rushwa wao hawana uamuzi wa mwisho wa kutoa hukumu,
zipo mamlaka halali zinazohusika na kutoa hukumu baada ya kuridhika na
upelelezi na uendeshaji wa kesi hiyo. Ni mahakamani ndiko kutakako
thibitisha
Anaonya
Rais kwa kusema. “ Lakini tusifike mahali tukageuka sisi ndio wapelelezi,
wakamataji, waendesha mashtaka na watoa hukumu. Wako wenzetu ambao wameamua
kuwa wapelelezi wao, wakamataji wao, waendesha mashitaka wao na watoa hukumu
wao, tena wanatoa hukumu wakati mtuhumiwa hayupo.Tusijipeleke huko na tukifanya
hivyo tunaipeleka nchi pabaya, nchi itayumba na hili si jambo nzuri na wala si
sawa”.
Anasisitiza
kwa kusema “ tabia hii ya watu kujifanya wao ndio wapelelezi, wakamataji na
watoa hukumu ni tabia ambayo ikiendekezwa itawatisha wananchi, itawatia
hofu, na itajenga chuki kati ya mtu na mtu, hii si haki na wala si sawa, hii
si nchi isiyokuwa na utawala wa sheria (law of the jungle). Ni nchi yenye
utawala halali na unaozingatia sheria za nchi na ina mamlaka ya kutekeleza
majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya haki, nje ya hapo ni
ukiukwaji wa misingi hiyo.”
Akasema
haiwezekani kauli ya mwanasiasa mmoja ya kumtuhumu fulani ndio mla rushwa
ikawa ndiyo hukumu, au serikali ikalazimishwa kumchukulia hatua mtu yule kwa
kutumia kauli ya mwanasiasa tu, lazima taratibu za kisheria zifuatwe, lakini
kubwa na la msingi hapa hata yule anayetuhumiwa naye anayo haki yake ya msingi
ya kutendewa haki.
“Baba
Askofu ninashukuru umeyasema haya na mimi nimeamua kuyaeleza haya niliyosema”
akafafanua Rais.
Awali
katika pongezi zake, Askofu Laiser alimweleza Rais kuwa, Dayosisi Mkoani Arusha
ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Akasema
Askofu Laiser “tunajua katika mapambano yoyote wataathirika waliomo na
wasiokuwako katika jambo lenyewe, lakini afadhali waathirike wachache
wasiokuwamo maana bila ya mapambano hayo wale wengi waliomo wataendelea
kuendeleza uovu na dhambi hiyo”
Akasisitiza
kwa kusema “Mhe. Rais tunajua mapambano hayo yana gharama zake kijamii na
kisiasa, lakini gharama hizo ni ndogo ukilinganisha na athari zitakazolikumba
taifa hili, rushwa za aina hii na aina nyingine zote zitakapoendelea kufumbiwa
macho. Neno la Mungu linasema ila wanawe
hawakuenda njia zake bali waliziacha ili wapate faida wakapokea rushwa na
kupotosha hukumu”.
Dayosisi
Mkoani Arusha ya Kanisa la Kiijili la Kilutheri
Hoteli
hiyo inayotarajiwa kukamilika mwezi Februari mwakani itagharimu Tshs.
Bilioni 3.6 sawa na dola za Kimarekani milioni 3.5.
Askofu
Laiser amemweleza mpango wa maendeleo wa Dayosisi hiyo ambayo inahusisha ujenzi
wa shule za sekondari, hospitali ya rufaa ni juhudi za Dayosisi hiyo la upunguzwaji
wa umaskini na kuisaidia serikali ya awamu ya nne iweze kufikia lengo lake la maisha
bora kwa kila Mtanzania.
Kabla
ya kuongoza harambee hiyo, Rais Jakaya Kikwete alitembelea na kukagua miradi
mikubwa ya shule ya sekondari ya watoto yatima
Mwisho.