PRESS SECRETARY TO THE PRESIDENT

OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 

 

 

 

                                                      

                          The State House,

Tel: 255-22-2116539/2116913                                                P.O. Box 9120,

Fax. No. 255-22 2113425                                                       DAR ES SALAAM.

E-mail:  press@ikulu.go.tz                                                      Tanzania.

              ikulupress@yahoo.com

 

                                                                                              18 Desemba, 2007

 

 

TAARIFA KWA WAHARIRI WA VYOMBO

 

 

Mhe. S. Sitta,

Spika wa Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

DAR ES SALAAM.

 

SALAMU ZA RAMBIRAMBI

 

Nimepokea kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Benedict Losurutia, Mbunge wa Kiteto, mkoani Manyara.

 

Katika uhai wake, nilimfahamu marehemu kama kiongozi shupavu ambaye katika nafasi mbali mbali za uongozi ambazo alizishikilia, alitekeleza majukumu yake kwa ukamilifu, uaminifu na uadilifu.

 

Marehemu  atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kama mwalimu na baadaye mbunge, na kwa jitihada zake kuchangia maendeleo na ustawi wa wananchi wa jimbo lake ambao aliwatumikia kwa moyo wake wote.

 

Hapana shaka kuwa kifo chake kitakuwa kimetugusa wengi wetu  hususani familia yake na wananchi wa jimbo lake na wale waliowahi kufanya kazi naye katika maeneo mbali mbali ya maendeleo ya nchi yetu. Lakini yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

 

Kwa moyo wa dhati kabisa, nachukua nafasi hii kutuma rambirambi zangu za pole kwa familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na wananchi wote wa Jimbo la Kiteto.

 

Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu. AMINA

 

 

Jakaya Mrisho Kikwete

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA