PRESS
SECRETARY TO THE PRESIDENT
OF
THE UNITED

The State House,
Tel:
Fax. No. 255-22 2113425 DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz Tanzania.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS KIKWETE AWAPA CHANGAMOTO VIONGOZI KUONGEZA TIJA
Rais Jakaya Kikwete amekamilisha ziara ya siku kumi mkoani Kagera kwa kutoa changamoto kwa viongozi mkoani Kagera kuongeza tija ili pato la mwananchi lipate kuongezeka.
“Tunayo kazi kubwa kuutoa mkoa hapa ulipo, baada ya kuzunguka sioni sababu ya nyie kuwa chini wakati mkoa una raslimali zinazoweza kuufanya mkoa huu kuwa mbele kimaendeleo” Rais amesema., wakati wa kufanya majumuisho katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Kishoju wilayani Muleba Jumatano jioni (23.1.08)
Taarifa zinaonyesha kuwa pato la mkoa wa Kagera lilo chini, ikiwa ni mkoa wa wa kumi na nane (18) kitaifa.
Rais amesema ili mkoa utoke hapo ulipo kimapato ni lazima viongozi wafanye jitihada za kwenda mbele kimaendeleo ili mapato ya watu yaongezeke na maisha kuwa bora kutegemea shughuli wanazofanya ambazo ni pamoja na kilimo, , uvuvi na ufugaji.
Zaidi ya asilimia 75 ya wananchi wa Mkoa wa Kagera wanategemea kilimo hususan zao la kahawa.
Rais amesema mkoa una mvua za kutosha ila tija ni ndogo hivyo changamoto kubwa kwa viongozi ni jinsi ya kuongeza tija kwenye ukulima wa kahawa, pamba, mahindi na mihogo.
Amewataka viongozi kuhimiza wananchi watumie miche bora iliyofanyiwa utafiti ambayo inaweza kustahimili maradhi na pia kuzaa zaidi.
“Fanyeni jitihada za kufufua zao la Kahawa mkoani humu maana likifa mkoa utakuwa maskini zaidi” amesema
Rais pia amevitaka vyama vya ushirika kujiimarisha zaidi ili wananchi waondokane na tatizo la soko na bei nafuu kwa mkulima kwani bei imekuwa kichocheo kikubwa cha magendo.
Rais pia amehimiza mazao mengine
Pia amewahimiza viongozi kuwa wabunifu na kuchangamkia zao la miwa kwa wananchi
walioko karibu na kiwanda cha sukari cha Kagera ili wananchi wapate kuuza mazao
“Muwahamasishe wananchi wajiletee maendeleo na pia kujitaftia na kujiongezea kipato kwa kutumia fursa mbalimbali, msiwarudishe nyuma kwa kuwaambia wasubiri serikali iwafanyie” amehimiza
Rais amewashauri viongozi mkoani Kagera kuboresha mifugo
Katika kuongeza ubunifu na kujituma zaidi katika kutafuta njia mbalimbali za kuongeza Tija Rais amnewataka viongozi kuweka mikakati ya kuvutia wawekezaji mkoani kagera kwa kutangaza vivutio na raslimali zinazopatikana mkoani Kagera.
Kuhusu Mfuko wa Rais wa kuwawezesha wananchi, Rais amesema ameyataka mabenki kote nchini kutoa taarifa za wananchi waliokopa ili serikali ifanye tathmini na kutafuta njia zaidi za kuuboresha mfuko huo ili uweze kuwafikia wananchi zaidi hasa vijijini.
“Tungependa kijua mikopo hii imekwendaje,
Rais amesema awamu ya pili ya mikopo hii inatarajiwa kuanza tena mwezi Julai mwaka huu, ambapo safari hii pesa zitapelekwa kwenye asasi ndogo ndogo zinazokopesha wananchi hasa walioko vijijini.
Akiwa Mkoani Kagera rais ametembelea wilaya zote saba mkoani humu na kukagua shughuli za maendeleo kwa kuzindua shule, vituo vya afya, kuweka mawe ya msingi na pia kutembelea shughuli mbalimbali za wananchi ambapo alitumia nafasi hiyo pia kuwapa wananchi maendeleo na hatua mbalimbali zilizofikiwa na serikali katika kutimiza ahadi zake za uchaguzi zikiwemo barabara, maji, umeme, afya, elimu na juhudi za kuinua maisha ya wananchi.
Rais Kikwete ameshafanya ziara za kikazi katika mikoa mingine nchini
Rais amerejea Dar-es-salaam leo jioni
Mwisho.
Imetolewa na
Premi Kibanga,
Mwandishi Habari Msaidizi wa Rais
Kagera.
23 Jan, 08