PRESS
SECRETARY TO THE PRESIDENT
OF
THE UNITED

The State House,
Tel:
Fax.
No. 255-22 2113425 DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz Tanzania.
PRESS RELEASE
Ujenzi wa reli kuunganisha
na
UJENZI wa
reli kuunganisha
Ujumbe wa
kampuni ya Barlington Northern Santa Fe (BNSF) kutoka
Marekani pia umemwambia Rais Kikwete kuwa ujenzi
huo unatarajiwa kukamilika 2013.
Ujumbe huo pia
umemwambia Rais kuwa kazi ya
ujenzi wa
reli hiyo mpya, utakwenda sambamba na matengenezo
makubwa na upanuzi wa Reli
ya Kati, kati ya Isaka na
Upanuzi huo utalenga
kuiwezesha Reli ya Kati kufikia kiwango cha kimataifa cha reli, kuongeza nguvu ya reli
hiyo kuweza kubeba mabehewa zaidi, na
kubeba mizigo mikubwa zaidi na
kupunguza muda wa safari.
Katika mazungumzo kati ya ujumbe
huo na
Rais Kikwete, Ikulu,
Ujumbe huo ulikuwa
ni pamoja
na Daniel Cooper na mashirika wake, Tom Vegh kutoka kampuni ya masuala ya
fedha ya Fox River
Financial Resources, ambayo inahusika
na masuala ya fedha kwa
ajili ya ujenzi wa reli
hiyo, pamoja na John Orrison kutoka kampuni ya BNFS.
Mazungumzo hayo pia
yamehudhuriwa na Waziri wa Fedha,
Zakia Meghji; Waziri wa Miundombinu,
Andrew Chenge na Waziri wa Mipango,
Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa.
Wakati maandalizi yanaendelea kwa
ajili ya ujenzi wa reli
ya Isaka-Kigali, na upanuzi wa
Reli ya Kati, maandalizi pia yanafanyika kwa ajili ya kuangalia
uwezekano wa ujenzi wa reli
kati ya Isaka-Kigali-Bujumbura.
Mbali na
hiyo, mipango pia inaandaliwa na kuangalia uwezekano
wa kuunganisha Isaka na mji
wa Mwanza, na kuunganisha Tabora na Kigoma
kwa reli bora zaidi.
Rais ameuelezea ujumbe huo kuhusu
furaha yake kusikia habari hizo, na
kusema kuwa Serikali yake inaiunga
mkono mipango hiyo kwa “asilimia
150”
“Ujumbe wangu ni mfupi tu – tunataka njia ya
reli. Na tunaunga mkono juhudi zenu
asilimia 150,” Rais ameuambia
ujumbe huo.
Rais pia ametaka kuangaliwa kwa uwezekano wa kuunganisha
Reli ya Kati na Reli ya TAZARA, na hivyo kuwezesha mizigo kutoka kusini
mwa Afrika kusafirishwa hadi Tanzania, na mizigo ya majirani wa
kaskazini wa Tanzania kusafirishwa kwa urahisi kwenda kusini mwa Afrika.
Ameuambia ujumbe
huo kuwa upanuzi na matengenezo makubwa katika Reli ya Kati utakwenda
sambamba na upanuzi mkubwa wa Bandari
ya Dar es Salaam.
Mwisho
Ikulu
25 Januari, 2008