PRESS
SECRETARY TO THE PRESIDENT
OF
THE UNITED

The State House,
Tel:
Fax.
No. 255-22 2113425 DAR ES SALAAM.
E-mail: press@ikulu.go.tz Tanzania.
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete ateua majaji
wapya wa Korti ya Rufani
Rais Jakaya Kikwete amewateua Majaji wanne wa
Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Taarifa iliyotolewa leo (Jumatatu, Februari 4,
2008) na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo inasema kuwa majaji walioteuliwa
ni Jaji Steven James Bwana, Jaji Bernard Michael Luanda, Jaji Mohammed Chande
Othman na Jaji Sauda Mjasiri.
Taarifa hiyo iliyotangazwa na Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais inasema kuwa uteuzi huo umeanza leo hii (Jumatatu, Februari
4, 2008).
Uteuzi huo umefanyika kwenye Siku ya Sheria Tanzania,
siku ambayo huashiria mwanzo wa kalenda ya mwaka wa shughuli za Mahakama
nchini.
Kabla ya uteuzi wake, Jaji Bwana alikuwa Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha.
Jaji Bwana ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama
Kuu mwaka 1999, pia amepata kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Jaji
wa Mahakama Kuu ya Visiwa vya Seychelles, na Katibu Sheria wa Jaji Mkuu wa
Tanzania.
Jaji Bwana pia alikuwa Jaji Mfawidhi wa kwanza Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Biashara.
Naye Jaji Luanda, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Biashara, mjini Dar es Salaam.
Jaji Luanda amepata kuwa Msajili wa Mahakama ya
Rufani Tanzania, na aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka
2000.
Jaji Mjasiri alikuwa katika Mahakama Kuu ya
Tanzania, Kitengo cha Biashara, Dar es Salaam kabla ya uteuzi wake.
Jaji Mjasiri ambaye amepata kuwa mwanasheria
katika Shirika la Sheria Tanzania (TLC), na mwanasheria wa Benki ya Biashara na
Maendeleo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (PTA), aliteuliwa kuwa Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania mwaka 2002.
Kabla ya uteuzi wake, Jaji Othman alikuwa katika
Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Jaji Othman amepata kuwa mwanasheria katika Chama
cha Msalaba Mwekundu (IRC), amepata kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali ya Visiwa
vya Timor Mashariki, na pia kuwa mwendeshaji mashitaka katika Mahakama ya
Kimataifa ya Rwanda (ICTR) mjini Arusha.
Aliteuliwa kuwa Jaji
wa Mahakama
Kuu ya
Ikulu
05/2/2008